Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyeng'atwa na nyuko
3.HUDUMA YA KWANZA KWA ALIYENG’ATWA NA NYUKI
Kung’atwa na nyuki kunaweza kukahitaji huduma ya kwanza kwa haraka kama mgonjwa ana aleji na nyuki. Utamjuaje kama ana aleji na nyuki?. ni pale utakapomuona aliyeng’atwa na nyuki akivimba mwili, na anaweza pia kupoteza fahamu. Pia hali hizi zinategemea ni kiasi gani cha nyuki wamemg’ata mtu.
Utakapomuona mtu ameng’atwa na nyuki usimkimbie, kwanza msaidie, kuhakikisha kuwa nyuki hawamng’ati tena. Unaweza kuchukuwa blanketi ama shuka uakmfunika vyema. Hakikisha na wewe umefunika pua, mgomo na masikio. Kama nyuki wanaendelea kuja mmwagie maji mgonjwa ili kupoteza harufu ya nyuki.
Hakikisha kabla hujaanza kutoa huduma ya kwanza, kwanza unaangalia hali ya aliyeng’atwa, kama hali ni ya kawaida na hahitaji kwenda hospitali. Kama anahitaji kwenda hospitali haraka wasiliana na kituo kilicho jirani ama tafuta msaada, kwa watu walio karibu. Hakikisha maamuzi haya hayaathiri hali ya mgonjwa. Ili kumpa huduma ya kwanza aliyeng’atwa na nyuki:-
1.kwa upole tumia kitu chenye wembamba kisha toa miiba ya nyuki kwenye ngozi ya mgonjwa. Katu usitukie kucha zako, maana zitaipasua miipa na sumu itaingia ndani na katu hutaweza kuitoa tena.
2.Unaweza kutuia kisu, ama kituchenye ncha, ila hakikisha kuwa miiba ya nyuki haikatiki kwa ndani. Kwa mfano unapotumia kiwembe kuna uwezekano mkubwa ukaikata miib kwa ndani.
3.Muweke mgonjwa mahali pa ubaridi kama inawezekana
4.Osha maeneo aliyong’atwa kwa sabuni na maji
5.Unaweza kutumia dawa za kutuliza maumivu.
6.Zipo dawa kama losheni (calamine lotion) ila ni maalumu kwa aliyeng’atwa na nyuki, kama zipo mgonjwa apakwe.
7.Hakikisha unamtuliza moyo mgonjwa.
8.Kama hali ni mbaya bado mgonjwa apelekwe kituo cha afya
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Post hii inahusu zaidi namna ya kuwasaidia wagonjwa wa vidonda vya tumbo, ni njia ya kuwasaidia wagonjwa waliopata madonda ya tumbo
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi Aina kuu tatu za mvunjiko ni Aina za kuvunjika ambazo uwakumba watu mbalimbali na watu ushindwa kutambua hizi Aina tatu za mvunjiko, zifuatazo ni Aina za mvunjiko.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu sababu za mdomo kuwa mchungu
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi watu ambao hawapaswi kupewa chanjo, hawa ni wale ambao wana hali tofauti na ikitokea wakapata chanjo wanaweza kupata madhara badala ya kuwasaidia.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu huduma ya Kwanza kwa mtu aliyeng'atwa na nyoka
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea utaratibu wa maisha kwa aliye athirika
Soma Zaidi...Mtoto mdogo ni mtoto chini ya miaka mitano, yaan kuanzia pale anapozaliwa mpaka anapafikisha miaka mitano
Soma Zaidi...Ajali ya kichwa na ajali inayotolewa kwenye sehemu mbalimbali za kichwa, ambavyo husababishwa madhara kwa aliyepata ajali hiyo
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu madhara ya upungufu wa vyakula vya madini
Soma Zaidi...Katika post hii utajifunza sababu zinazowezabkuorlekea kibofu kuuma upande mmoja
Soma Zaidi...