image

Ni ipi hasa siku ambayo nitafute ujauzito

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu siku za kutafuta ujauzito

NI IPI HASA SIKU AMBAYO NITAFUTE UJAUZITO?

Kama ulipojifunza hapo juu kuwa zipo siku maalaumu ambazo yai hukomaa. Katika siku hizo mojawapo yai huletwa kwenye mirija ya falopia. Baada ya kukokotoa siku zako hapo juu sasa itakubidi kuongeza siku moja ama mbili nyuma. Hii ni kwa sababu makadirio ya siku hutofautiana. Na si lazima kkutafuta toto katika siku zote hizi. Unaweza kuruka kwa siku moja moja.

 

Jitahidi kufanya tendo la ndoa hasa katika siku hizo nne ulizozipata baada ya kukokotoa. Katika siku hizo jitahidi kufanya tendo siku ambayo itakuwa na sifa zifuatazo:-

 

1.Majimaji ya mwanamke ukeni yatakuwa ni mengi kuliko siku zilizopita. Mwanamke mwenyewe anaweza kujichunguza hali hii na kuigundua ila taabu. Anaweza kutumia kidole ama kitambaa safi kuchunguza uwepo wa majimaji haya katika ukeni kwake. Kumbuka hali hii isiambatane na shida nyingine za afya kama PID. Wakati mwingine inaweza kuwa ngumu kuchunguza hasa kwa wale wanaotumia uzazi wa mpango hasa hasa kwa kutumia vidonge vya homoni.

 

2.Joto la mwanamke litakuwa ni kubwa kuliko siku nyingine. Joto hili sio homa, na lisiambatane na sababu nyingine kama maumivu ya kichwa, ama kutokana na kulala sana, ama misongo ya mawazo. Kikawaida siku ambayo yai hutolewa joto la mwanamke linakuwa kubwa hivyo akishiriki siku hii ujauzito ni rahisi kuingia.

 

3.Siku ambayo mwanamke atakuwa na hamu sana ya kushiriki tendo. Wakato ambapo yai hutolewa kuna homoni huzalishwa kwa wingi. Homoni hizi zinaweza kusababisha mwanamke kutamani sana kushiriki tendo zaidi ya siku nyingine.

 

Pindi mwanamke atakapojigundua kuwa siku hii ameipata basi ni vyema kushiriki tendo ndani ya siku hii ama siku itakayofata haraka iwezekanavyo, maana yai la mwanamke linaweza kufa ndani ya muda mchach masaa 12 mpaka 24.

 

Kuna baadhi ya wanawake wanapata changamoto kutokana na kuwa na shida ya homoni katika mfumo wao wa uzazi. Hawa ni wale ambao siku zao hawazipati katika mpangilio sawa. Ni vyema wakafika kituo cha afya kupata matibabu ya tatizo hilo.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1217


Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh     👉2 Madrasa kiganjani     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

SABABU ZA KUTOKA KWA MIMBA (sababu za kuharibika kwa ujauzito)
Tafiti zinaonesha kuwa karibia asilimia 10% mpaka 25% ya wanawake wanaopata ujauzito, mimba zao hutoka. Soma Zaidi...

Dalili za Maambukizi na Uvimbe katika mirija ya uzazi
Posti hii inazungumzia kuhusiana na maambukizi na uvimbe katika  mirija ya uzazi. Mara nyingi hutumiwa sawa na ugonjwa wa uvimbe kwenye fupa nyonga (PID), ingawa PID haina ufafanuzi sahihi na inaweza kurejelea magonjwa kadhaa ya njia ya juu ya uzazi Soma Zaidi...

Madhara ya tumbaku na sigara
Post hii itakwenda kuangalia madhara ya tumbaku na sigara anayoweza kuyapata mvutaji Soma Zaidi...

Nimegundua ni mjamzito na kibaya zaid namtoto mchanga nimefanyiwa opaleshen naomba ushauli wako mkuu
Inatakiwa angalau nafasivkati ya mtoto na mtoto wapishane miaka miwili. Soma Zaidi...

Sababu za Ugonjwa wa kifafa cha mimba.
Posti hii inahusu zaidi sababu za kifafa cha mimba, kwa kawaida mpaka sasa hakuna taarifa zozote kuhusu sababu za kuwepo kwa kifafa cha mimba ila kuna visababishi vinavyofikiliwa kama ni Dalili za kifafa cha mimba kama ifuatavyo Soma Zaidi...

Mbinu za kupunguza Kichefuchefu
Point hii inahusu zaidi mbinu za kupunguza Kichefuchefu hasa kwa wagonjwa na watumiaji wa madawa mbalimbali yanayoweza kusababisha kichefuchefu. Soma Zaidi...

Sababu za mimba ya miezi 4-6 kutoka.
Posti hii inahusu zaidi sababu za mimba ya miezi kuanzia minne mpaka sita kutoka , Kuna kipindi mimba kuanzia miezi mimne mpaka sita utoka kwa sababu mbalimbali. Soma Zaidi...

Kwa nini hujapata siku zako za hedhi.
Unaweza kupitiliza siku zako za hedhi kwa sababu nyingi. Post hii itakueleza ni kwa nini umechelewa kupata siku zako. Soma Zaidi...

je maumivu ya nyonga na tumbo la chini ni dalili ya mimba?
Nina swali langu:-je maumivu ya nyonga na tumbo la chini ni dalili ya mimba? Soma Zaidi...

Namna ya kumtunza mtoto aliyezaliwa
Post hii inahusu zaidi namna ya kumtunza mtoto mchanga aliyezaliwa, ni njia zitoleeazo na wakunga Ili kumtunza mtoto mchanga aliyezaliwa. Soma Zaidi...

Dalili za kujifungua hatua kwa hatua
Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu dalili za ujauzito baada ya tendo la ndoa Soma Zaidi...

Damu, majimaji na uteute unaotoka kwenye uke wa Mjamzito, sababu zake na dalili zake
Unataka kujuwa sababu za mjamzito kutokwa na damu, utelezi ama majimaji kwenye uke wake. Na dalili gani zinaashiriwa na majimaji haya Soma Zaidi...