Post hii inahusu zaidi dalili za ugonjwa wa kaswende kwa wajawazito, hizi ni dalili ambazo ujitokeza kwa watu wote, kwa sababu ugonjwa huu una dalili ambazo upitia kwa hatua mbalimbali kama tutakavyoona.
1. Kwa kuwa tangu mwanzoni nimejaribu kueleza kwamba ugonjwa huu upitia kwenye hatua mbalimbali,kwa hiyo tutaanza na hatua ya kwanza ambayo kwa kitaalamu huitwa primary symptoms, kwenye hatua hii mgonjwa anakuwa na vipele ambazo havina maumivu kwa kitaalamu huitwa chancres hivi vidonda hivyo ujitokeza baada ya wiki tatu baada ya maambukizi, hivi vidonda mara nyingi utokea sehemu ambayo sex imefanyiwa kama ni mdomoni vitajitokeza hapo kama ni kwa njia ya haja kubwa vitajitokeza hapo au kama ni kwa njia ya kawaida na penyewe vitajitokeza hapo, kwa hiyo vidonda hivyo kama havijapata matibabu utoweka ndani ya wiki tatu mpaka sita.
2. Kwa hiyo kama ikitokea mtu akapatwa na tatizo kama hili na anajua kabisa alifanya ngono bila kinga ni vizuri kabisa kupata matibabu mapema ili kuondoa tatizo kubwa kubwa zaidi, changamoto ni kwamba vidonda hivi mara nyingi huwa haviumi ndio maana watu wengi hawajishughulishi kupima badala yake ni kupotezea na ukizingatia havina maumivu yoyote, madhara ya kutotibu mapema usababisha hali ambayo sio nzuri kama tutakavyoona hapo baadaye.
3. Hatua ya pili utokea pale ambapo vidonda vya hatua ya kwaza kutotibiwa , hatua hiyo kwa kitaalamu huitwa primary symptoms,hivi vidonda ambavyo vilikuwepo vinatudi tena sio kwenye sehemu ambayo sex ilifanyika tu bali ni katika sehemu mbalimbali za mwili kama vile kwenye mikono hasa hasa kwenye sehemu ya viganja, kwenye miguu hasa kwenye ukanyagio,pia na rangi yake inakuwa kama ya nyekundu ila sio nyekundu iliyokaza, na pia vidonda hivi vinaweza kuwa hata mdomoni, hali hiyo utokea kwa sababu ya ugonjwa kueneza kwenye sehemu mbalimbali za mwili.
4. Katika hatua hii mgonjwa anaweza kushindwa kutembea kwa sababu ya kuwepo kwa vidonda kwenye nyayo za miguu na wakati mwingine hatua hii uambatana na homa, mwili mzima kuchoka,Madonda kwenye koo, kuvimba kwa lymph nodes kwa sababu ya maambukizi, pengine nywele kwenye kichwa unyonyoka , maumivu makali ya kichwa, kupungua uzito, na pia mwili kuishiwa nguvu.
Pengine watu uchanganya dalili hizi na mgonjwa wa HIV kwa sababu dalili za mgonjwa wa HIV hatua ya nne na tatu huwa na dalili kama hizi, mtu kuja kufikia hatua hiyo ni kwamba ugonjwa huu unakuwa umemaliza miaka kama kumi na tano mwilini na ndipo dalili za hapo juu zinaweza kutokea.
5 . Kwa hiyo jamii inapaswa kuelezwa wazi kuhusu ugonjwa huu kwa sababu kuna wakati watu wanaenda kupima baada ya kuona dalili kama hizi wakidhani ni maambukizi ya Virusi vya Ukimwi, na baadae unakuta mtua anapewa majbu kwamba hana maambukizi ya ukimwi na ni kweli anakuwa hana ila shida watu wengi hawapimi kaswende na yenyewe kama haijatibiwa inaweza kumfikisha mtu sehemu mbaya , kwa hiyo kupima kaswende ni lazima ili kuweza kuepukana na matatizo mbalimbali.
6. Pia hatua ya mwisho ni hatua ya tatu ambayo kwa kitaalamu huitwa latent phase, ni hatua ya mwisho utokea mara nyingi kama hatua ya pili haijatibiwa na kama matibabu hayajafikiwa mgonjwa anaweza kupoteza maisha, kwa hiyo kupima kaswende ni lazima ili kuweza kuepukana na vifo vya akina mama na watoto wao, twende hospitali dawa ipo na watu wengi wanapona.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: magonjwa Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1624
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉2 Kitabu cha Afya
👉3 Madrasa kiganjani
👉4 Kitau cha Fiqh
👉5 kitabu cha Simulizi
👉6 Simulizi za Hadithi Audio
Dalili na ishara za Ugonjwa wa akili.
Posti hii inazungumzia kuhusiana na Ugonjwa wa akili . Soma Zaidi...
MINYOO NA ATHARI ZAKE KIAFYA, NA NAMNA YA KUPAMBANA NA MINYOO NA DALILIZAKE.
Soma Zaidi...
Ni bakteria gani husababisha ugonjwa wa pumu
Post hii inakwenda kujibu swali linalosema je ni bakteria aina gani husababisha igonjwa wa pumu. Soma Zaidi...
Sababu za maambukizi kwenye nephoni
Posti hii inahusu zaidi sababu za maambukizi kwenye nephroni, ni vitu vinavyosababisha mabukizi kwenye nephroni. Soma Zaidi...
Namna Maambukizi kwenye milija na ovari yanavyotokea
Post hii inahusu zaidi namna Maambukizi kwenye milija na ovari ambayo yanatokea,Mara nyingi usababisha na bakteria wanaoweza kuingia kupitia sehemu mbalimbali. Soma Zaidi...
Dalili za fangasi kwenye mapafu
Posti hii inaonyesha dalili za fangasi kwenye mapafu. Soma Zaidi...
Njia za kutibu saratani
Posti hii inahusu zaidi njia mbalimbali za matibabu ya ugonjwa wa saratani,ni ugonjwa ambao unaweza kupona ikiwa umegundulika mapema katika hatua za mwanzo na kama ugonjwa huu umefikia hatua za mwisho Tiba yake huwa ni kupunguza makali ya ugonjwa. Soma Zaidi...
Madhara ya minyoo
Posti hii inaonyesha kiufupi kabisa madhara ya minyoo kwenye mwili wa binadamu.
Yafuatayo Ni madhara ya minyoo; Soma Zaidi...
Je vvu inaweza sababisha mate kujaa mdomoni
Je kujaa kwa mate mdomoni ni dalili ya kuwa na VVU, na je ni zipi dalili za Virusi Vya Ukimwi (VVU) mdomoni? Soma Zaidi...
Sababu za maumivu ya viungo na viungo kuwaka moto nini sababu zake
Soma Zaidi...
Dalilili za homa ya manjano
posti hii inahusu dalili za Homa ya Manjano ni maambukizi ya virusi yanayoenezwa na aina fulani ya mbu. Maambukizi hayo ni ya kawaida zaidi na kuathiri wasafiri na wakazi wa maeneo hayo. Soma Zaidi...
Jinsi ya kujikinga na mafua (common cold)
Posti hii inazungumzia dalili na namna ya kujikinga tusipate mafua .mafua kwa jina lingine hujulikana Kama baridi ya kawaida (common cold).baridi ya kawaida husababishwa na virusi kwenye pua na hutoa makamasi. Soma Zaidi...