Kujielimisha kwa Ajili ya Allah (s.w).
Elimu ndiyo zana aliyotunukiwa mwanadamu ili aitumie kutekeleza majukumu yake kama Khalifa wa Allah (s.
- Kujielimisha kwa Ajili ya Allah (s.w).
Elimu ndiyo zana aliyotunukiwa mwanadamu ili aitumie kutekeleza majukumu yake kama Khalifa wa Allah (s.w) hapa ulimwenguni. Mara tu baada ya Nabii Adam (a.s) kuumbwa na kabla hajaruzukiwa chochote na hata kabla ya kukaribishwa kwenye neema za bustanini (Peponi) alifunzwa mambo yote ya msingi yatakayomuwezesha kuwa Khalifa hapa Ulimwenguni:
“Na (Allah (s.w)) akamfundisha Adam m ajina ya vitu vyote...” (2:31).
Naye Mtume Muhammad (s.a.w) Wahyi na amri ya kwanza aliyoipokea kutoka kwa Mola wake ni kusoma kwa ajili ya Allah (s.w). Hivyo kila Muislamu analazimika kuitekeleza kwa hima amri hii ya kwanza ili aweze kumuabudu Mola wake inavyostahiki na aweze kuwa Khalifa wake hapa ulimwenguni.Aidha kila Muislamu analazimika kujielimisha mambo ya msingi yatakayomuwezesha kuwa Muumini wa kweli na kumuwezesha kuendesha maisha yake yote ya kibinafsi na kijamii kwa mujibu wa Qur-an na Sunnah.
Ni wazi kuwa Muislamu mwenye kujipamba na tabia ya kujielimisha katika mambo muhimu ya maisha kwa lengo la kupata ufanisi katika kumuabudu Allah (s.w) na kusimamisha Ukhalifa katika jamii; atakuwa tofauti kiutendaji na kiuchaji na yule aliye mvivu wa kujielimisha kama tunavyojifunza katika Qur-an:
“Je, wanaweza kuwa sawa wale wanaojua na wale wasiojua?” Wanaotanabahi ni wale wenye akili tu.” (39:9).
“Allah atawainua daraja wale walioamini miongoni mwenu;na waliopewa elimu watapata daraja zaidi...” (58:11)
Ukizingatia kuwa kutafuta elimu ni faradh kwa kila Muislamu mwanamume na mwanamke, mkubwa na mdogo, aya hizi zatosha kuwa
kichocheo kwa kila Muumini kujibidiisha kwa kujielimisha kwa ajili ya Allah(s.w) kwa kadri ya uwezo wake na kila wakati awe anaomba dua ifu atayo:
“... Mola wangu! Nizidishie elimu.” (20:114)
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
👉1 ai web app 👉2 web hosting 👉3 Dua za Mitume na Manabii 👉4 Madrasa kiganjani 👉5 Bongolite - Game zone - Play free game 👉6 Kitau cha Fiqh
Post zinazofanana:
Dalili na ishara za jeraha kwenye ngozi
Posti hii inaonyesha dalili,sababu na mbinu za kutoa huduma ya kwanza kwa aliyepata jeraha kwenye ngozi kwa kuingiliwa na kitu Kama mwiba,Pini,sindano n.k
Soma Zaidi...Njia anazotumia Mwenyezi Mungu (s.w) kuwafundisha na kuwasiliana na wanaadamu
Ni zipo njia wanazotumia Allah katika kuwasiliana na kuwafundisha wanadamu? (EDK form 1: Dhana ya elimu katika Uislamu).
Soma Zaidi...Kuamini vitabu vya mwenyezi Mungu (s.w)
Nguzo za Imani (EDK form 2: Dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...