Wajbu wa wazazi kwa watoto wao

Wajibu wa Wazazi kwa Watoto Wazazi wanawajibu kwa watoto wao.

Wajbu wa wazazi kwa watoto wao

Wajibu wa Wazazi kwa Watoto
Wazazi wanawajibu kwa watoto wao. Wajibu wa wazazi kwa watoto wao ni kuwapa malezi bora yatakayowawezesha kuinukia kuwa watu wema katika jamii watakao simamisha Ukhalifa katika ardhi. Malezi yanahusu yale yote anayofanyiwa mtoto tangu akiwa tumboni mwa mama mpaka kufikia umri wa kujitegemea. Wazazi wote wawili wanahusika kwa ukamilifu na malezi haya. Malezi ya mtoto tunaweza kuyagawa katika sehemu mbili - Malezi ya kimwili na malezi ya kimaadili.



Malezi ya kimwili:



Malezi ya kimwili ni yale yote anayofanyiwa mtoto iii akue katika afya njema. Malezi haya huanza mara tu mama anapoanza ujauzito. Baba ana wajibu wa kumtunza mkewe na kumpatia vyakula maalum ili mama na mtoto wake tumboni wawe na afya nzuri. Jukumu Ia mama ni kufuata masharti ya kulea mimba anayopewa na Daktari. Baada ya mtoto kuzaliwa wajibu wa baba na mama kwa mtoto wao unabainishwa katika Qur-an:



Na wanawake waliozaa wawanyonyeshe watoto wao miaka miwili kamili, kwa anayetaka kukamilisha kunyonyesha; na ni juu ya baba chakula chao (mama na mtoto wake) na nguo zao kwa sheria. Wala haikalflshwi nafsi yoyote ila kwa kadri ya wasaa wake. Mama asitiwe taabuni kwa ajili ya mtoto wake, wala baba (asitiwe taabuni) kwa ajili ya mtoto wake. Najuu ya mrithi ni kama hio. Na wote wawili wakitaka kumwachisha ziwa (kabla ya miaka miwili) kwa kuridhiana na kzshauriana, basi si kosajuu yao. Na kama mkitaka kuwapatia watoto wenu mama wa kuwanyonyesha (wengine wasiokuwa mama zao) basi haitakuwa dhambi juu yenu kama mkitoa (kuwapa hao wanyonyeshaji) mlicho waahidi kwa sharia. Na mcheni Mwenyezi Mungu na jueni kwamba Mwenyezi Mungu anayaona yote mnayoyatenda. (2:233).



Aya hii inatubainishia wazi kuwa hata katika umri wa kunyonya mtoto, wazazi wote wawili wanawajibika, kila mmoja katika nafasi yake. Katika kipindi chote cha kumlea mtoto jukumu kubwa Ia baba ni kuilisha familia, kuivisha na kuiweka katika makazi mazuri kwa kadiri ya wasaa wake. Mama naye ana jukumu Ia kuwatunza watoto kwa kuhakikisha kuwa wanakula vilivyo, wanakuwa wasafi wa mwili na nguo na wanaishi katika mazingira masafi. Haya ndiyo malezi ya kimwili ambayo humuwezesha mtoto kuwa na afya nzuri na kukua vyema.


Malezi ya Kimaadili:



Malezi ya kimwili ni muhimu sana, lakini yenyewe tu hayatoshelezi kumuinua mtoto atakayekuwa raia mwema mwenye kuwajibika ipasavyo kwa wazazi wake na jamii yake kwa ujumla.Uislamu haumtizami mwanaadamu kama mnyama, bali unamtazama kama Khalifa wa Allah (s.w) ambaye asili yake ni mwili unaotokana na udongo na roho takatifu inayotokana na Allah (s.w) kama tunavyojifunza katika Qur-an:


Na (kumbuka) Mola wako alipowaambia Malaika: "Hakika Mimi nitamuumba mtu kwa udongo mkavu unaotoa sauti, wenye kutokana na matope meusi yaliyovunda! Basi nitakapo mkamilisha na kumpulizia roho inayotokana na Mimi, basi muangukieni kwa kumtii ". (15:28-29).



Kutokana na aya hizi tunajifunza kuwa kilichomfanya mwanaadamu kuwa na hadhi juu ya viumbe vyote hata malaika ambao waliamrishwa na Allah (s.w) kusujudiwa si uzuri wa sura yake au umbile lake, bali ni ile Roho takatifu inayotokana na Allah (s.w). Lakini Si kila mwanaadamu atakayestahiki heshima hii ya kumsujudia na Malaika. Anayestahiki heshima hii ni yule tu atakayeishi kwa kufuata tabia na mwenendo anaoridhia Allah (s.w) au kwa kufuata maadili mema anayoyaridhia Allah (s.w) na kufanya juhudi za kusimamisha Ukhalifa ardhi. Atakayeishi kwa kufuata msukumo wa matashi ya mwili (unyama) wake na kuukataa mwongozo wa Allah (s.w) na mtume wake atakuwa duni kuliko vilivyo duni kama Allah (s.w) anavyotufahamisha:


Bila shaka tumemuumba mwanaadamu kwa umbo hub bora kabisa. Halafu tukamrudisha chini kuhiko wahio chini. ila wale wenye kuamini na kutenda mema, watakuwa na ujira usio kwisha. (95:4-6). Hivyo, wazazi sambamba na kuwalea watoto wao kimwili, hawanabudi kuwalea kimaadili. Malezi hayo huanzia pale kwenye kufanya tendo Ia ndoa (jimai) ambapo wazazi huleta dua ifuatayo:


Bismillah Allahumma jannib-na shaytwaani wajannibi sh-shaytwaani maarazaqtanaa.
Kwa jina ?a Allah, Ee Allah muweke shetani mbali nasi na muweke shetani mbali na hicho ulichoturuzuku ".
Mimba inapotunga wazazi wa Kiislamu huomba dua, Allah (s.w)) awape mtoto mwema kama tunavyojifunza kaitka Quran (7:189)
Kila mtoto huzaliwa Muislamu, kama tunavyojifunza katika Hadith ifuatayo:



Abu Hurairah (r.a) amesimulia kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu amesema: "Hapana mtoto asiyezaliwa katika (dini ya) asili (Uislamu). Kisha wazazi wake humfanya kuwa Myahudi au Mkristo au Mmajusi. Amezaliwa kama anavyozaliwa mnyama na miguu yake yote. Umemona (mnyama) yeyote aliyezaliwa kilema? Kisha akasema: "Umbile la Asili ndilo umbile Mwenyezi Mungu aliloumbia watu. Hakuna mabadiliko katika maumbile ya viumbe vyote vya Mwenyezi Mungu ". (30:30) - (Bukhari na Muslim)



Hadith hii iliyomalizia na aya ya Qur'an (30:30) inatukumbusha kuwa Uislamu ni dini ya maumbile inayolandana na umbile Ia binaadamu. Kwahiyo, wazazi wa Kiislamu hawanabudi kumbakisha mtoto wao katika dini yake ya asili kwa kufanya yafuatayo:



Kumuadhinia Mtoto
Mara tu mtoto anapozaliwa ni sunnah kumuadhinia sikio Ia kulia na kumkimia kwa sikio Ia kushoto. Hekima yake ni kumuombea mtoto awe mwema atakayesimamisha swala na kusimamisha Uislamu katika jamii.


Kumfanyia Mtoto Aqiqah
Ni sunnah vile vile kumfanyia mtoto aqiqah katika siku ya saba baada ya kuzaliwa kwake. Aqiqah ni mbuzi anayechinjwa kwa ajili ya mtoto aliyezaliwa anapofikia siku ya saba tokea kuzaliwa kwake. Sunnah hii ya Aqiqah imetiliwa mkazo kwani Mtume (s.a.w) amesema: Kila mtoto amefungika na aqiqah yake, itachinjwa kwa ajili yake siku yake ya saba na atapewa jina, na atanyolewa kichwa chake." (Ahmad, An-Nasai).



Katika kumtafuta mbuzi wa 'aqiqah ni vema kuzingatia masharti yafuatayo: Awe na umri usiopungua mwaka mmoja, awe bora kwa sura na siha na asiwe na kilema chochote. Ni sunnah vile vile kuigawa nyama ya aqiqah katika mafungu yafuatayo:
- Theluthi ya kwanza watakula watu wa familia ya mtoto.
- Theluthi ya pili itatolewa sadaqa kwa mafakiri na maskini.
- Theluthi ya tatu itatolewa zawadi kwa majirani, marafiki na jamaa wa karibu.



Ni sunnah kwa mtoto wa kiume afanyiwe Aqiqah kwa kuchinjiwa mbuzi wawili. Pia ni sunnah siku hiyo ya saba anyolewe nywele na zipimwe na kulinganishwa na uzito wa dhahabu au fedha, na kutolewa sadaqa kulingana na uzito huo wa dhahabu au fedha.



Kama haikuwezekana kumfanyia mtoto aqiqah siku ya saba unaweza kumfanyia siku ya kumi na nne (14) au siku ya ishirini na moja (21 ).
Hekima ya kumfanyia mtoto aqiqah, ni kumshukuru Allah (s,w) kwa kukuneemesha mtoto na kumuombea mtoto huyo kwa Allah kuwa amuhifadhi na kumchunga na mabaya na amfanye mja mwema atakayekuwa tayari kujitoa muhanga kwa mali na nafsi kwa ajili ya kusimamisha Uislamu katika jamii.


Kuwapenda na Kuwahurumia Watoto



Jambo jingine muhimu kwa wazazi katika kuwalea watoto wao ni kuwa na upendo na huruma juu yao. Ukali wa kupindukia na ukaripiaji wa mara kwa mara si malezi mazuri na kamwe mtoto haleleki vyema katika mazingira kama hayo. Mtume (s.a.w) aliye kiigizo chetu, alikuwa ni miezi mwema mno. Alikuwa na huruma na upendo mkubwa mno juu ya watoto wake na wajukuu zake kama tunavyojifunza katika Hadith zifuatazo:



Aysha (r. a) amesimulia: S/amuona mtu aliyeshabihiana kitabia na mwenendo na Mtume (s.a.w) kuliko Fatma. Alipokuja kwa Mtume (s.a.w), Mtume (s.a.w) alimsimamia, kisha alimchukua kwa mkono wake na kumbusu na kisha kumkalisha karibu yake. Na Mtume (s.a.w) alipokwenda kwake, Fatma alikuwa akimsimamia, kisha akimiwaa kwa mkono wake na kumbusu, na kumkalisha karibu naye. (Abu Daud).



Pia Mtume (s.a.w) amesisitiza kuwapenda na kuwahurumia watoto kwa kuwabusu kama Hadith zifuatazo zinavyotufahamisha:
Abu Hurairah ameeleza kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu alimbusu mjukuu wake, Hassan bin Au, mbele ya Aqra bin Habis ambaye alisema: Nina watoto kumi na s/ambusu hata mmoja wao. Mtume wa Mwenyezi Mungu alimwangalia na kusema: "Yule asiye na huruma hatahurumiwa ". (Bukhari na Muslim).



Aysha (r. a) ameeleza kuwa Mwarabu wa jangwani (Bedui) alikuja kwa Mtume (s.a.w) akasema: Nini! Unabusu watoto? Sisi hatuwabusu. Mtume (s.a.w) akasema: "Sina la kuwasaidia, kwani Mwenyezi Mungu (s.w) ameondoa huruma nyoyoni mwenu." (Bukhari na Muslim)



Hadith hizi mbili zinatusisitiza tuwalee watoto wetu kwa huruma na upendo. Kuwabusu watoto ni kielelezo cha upendo wetu kwao. Kuwaelimisha Watoto
Watoto wafunzwe tabia ya Kiislamu tangu mwanzo hasa pale anapoanza kuongoea na kuelewa lile analoelekezwa. Watoto wafikiapo umri wa miaka minne - mitano, wahudhurishwe pamoja na watoto wenzao kwenye vituo vya malezi vya Kiislamu. Watoto wafunzwe namna ya kuishi Kiislamu kwa kadiri ya umri wao. Wakifikia umri wa miaka saba wazoeshwe kutekeleza ibada maalumu kama vile swala na swaumu. Watoto wa miaka kumi na kuendelea walazimishwe kutekeleza maamrisho yote ya Allah (s.w) kwa kadiri ya uwezo wao na kukatazwa kuacha makatazo yake yote. Wakikaidi waonywe na kupewa adhabu.



Kuwapa Watoto Nasaha



Watoto wetu wanapokuwa wakubwa tuwaozeshe mapema kwa wanaume au wanawake wenye mwenendo na tabia ya Kiislamu na daima tusiache kuwapa nasaha njema. Hebu turejee Qur-an tuone nasaha ya Luqman kwa mwanawe:


Na (wakumbushe) Luqman alpomwambia mwanawe; na hali ya kuwa anampa nasaha. Ewe mwanangu! Usimshirikishe Mwenyezi Mungu, maana kushirikisha ndiyo dhulma kubwa. (31:13)


Ewe mwanangu! Kwa hakika jambo lolote lj/apokuwa na uzito wa chembe ya hardali, likawa ndani ya jabali au mbinguni, au katika ardhi, Mwenyezi Mungu atalileta bila shaka Mwenyezi Mungu ni Latfu (Mpole), Mjuzi wa kila jambo. (31:16)



Ewe Mwanangu! Simamisha swala, na uamrishe mema, na ukataze mabaya, na usubirijuu ya yale yatakayokusibu. Hakika hayo ni katika mambo yanayostahiki
kuaizimiwa. (31:17)


Wala usiwatazame (watu kwajeuri) kwa upande mmoja wa uso, wala usiende katika ardhi kwa maringo; hakika Mwenyezi Mungu hampendi kila ajivunae, afifaharishaye. (31:18)


Na ushike mwenendo wa katikati, na uteremshe sauti yako, bila shaka sauti ya punda ni mbaya kuliko sauti zote (mbele ya Mwenyezi Mungu (s.w). (31:19)
Pia turejee nasaha za Nabii Ibrahimu (a.s) na Yaaquub (a.s) kwa wana wao katika aya zifuatazo:


"(Kumbukeni habari hii) Mola wake (Ibrahimu) alipomwambia: Aslim (Nyenyekea); akanena 'Nimenyenyekea kwa Bwana miezi wa walimwengu (wote) (2:131)



"Na Ibrahimu akawausia haya wanawe; na Ya 'aquub! Hakika Mwenyezi Mungu amekuchagulieni Dini hii (Al-Islaam) basi msfe ila mfe mkiwa Waislamu ". (2:132)
Tahadhari juu ya Watoto Pamoja na kuwalea watoto wetu ipasavyo, hatuna budi kuchunga mipaka ya Mwenyezi Mungu (s.w) katika kufanya kazi hiyo. Huruma na upendo kwa watoto wetu kamwe kusitupelekee kwenda kinyume na maamrisho ya Mwenyezi Mungu (s.w) na Mtume wake.Muislamu anatakiwa ampende Mwenyezi Mungu (s.w) na Mtume wake kuliko hata anavyoipenda nafsi yake, sembuse nafsi nyingine. Mara nyingi, baadhi ya wazazi, kwa ajili ya kuwapenda na kuwahurumia watoto wao, huwaachia huru kwenda kinyume na maamrisho na makatazo ya Mwenyezi Mungu (s.w). Juu ya hili Allah (s.w) anatunasihi:


Enyi mlioamini! Yasikusahaulisheni mali yenu wala watoto wenu kumkumbuka Mwenyezi Mungu! Na wafanyao hayo, hao ndio wenye kuhasirika(63:9).


Enyi mlioamini! Kwa yakini baadhi ya wake zenu na watoto wenu ni maadui zenu, basijihadharini nao (64:14).


Bila shaka mali zetu na watoto wenu ni mtihani. Na kwa Mwenyezi Mungu kuna ujira mkubwa kabisa. (64:15).



Mali na watoto ni pambo la maisha ya dunia. Na vitendo vizuri vibakiavyo ndivyo bora mbele ya Mola wako kwa malipo na tumaini bora. (18:46).
Pamoja na kuwapenda na kuwahurumia wake zetu na watoto wetu na pamoja na kuipenda mali na vyote vingine vinavyopendeka, hatuna budi kuhakikisha kuwa upendo wetu juu ya Mwenyezi Mungu (s.w) na Mtume wake nakupigania dini yake unakuwa juu ya kitu chochote kile kama Mwenyezi Mungu (s.w) anavyotutanabahisha tena katika aya zifuatazo:


Enyi mlioamini! Msiwafanye baba zenu na ndugu zenu kuwa vipenzi (vyenu) ikiwa wanastahabu (wanapenda) ukafiri kuliko Uislamu. Na katika nyinyi atakayewafanya hao kuwa ndio vipenzi vyake, basi hao ndio madhalimu. (9:23)


Sema:Kama baba zenu na wana wenu na ndugu zenu na wake zenu na jamaa zenu na mali mlizochuma, na biashara mnazoogopa kuharibikiwa, na majumba mnayoyapenda, ni vipenzi zaidi kwenu kuliko Mwenyezi Mungu na Mtume wake na kupigania dini yake, basi ngojeni mpaka Mwenyezi Mungu alete amri yake, na Mwenyezi Mungu hawaongozi watu maasi. (9:24).



Jambo jingine muhimu Ia kuzingatia zaidi katika kuwalea watoto ni kutokuwa na upendeleo wala ubaguzi kati ya watoto. Wazazi wanawajibika sawa kwa watoto wao wote na kila mtoto ana haki sawa na mwengine katika kupendwa na kuhurumiwa na wazazi wake.




                   




Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 267


Download our Apps
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Kujiepusha na kukaribia zinaa
Si zinaa tu iliyoharamishwa bali hata yale yote yanayotengeneza mazingira na kuchochea kufanyika kwa zinaa nayo pia yameharamishwa. Soma Zaidi...

mtazamo wa uislamu juu ya dini
Soma Zaidi...

JIFUNZE FIQH
Fahamu darsa mbalimbali za fiqh kama swala, twahara, zaka pamoja na funga. Zijuwe sharti za swala, funga na zaka. Soma Zaidi...

HALI AMBAZO MTU AKIOMBA DUA HUJIBIWA
HALI AMBAZO MTU AKIOMBA DUA ITAJIBIWA. Soma Zaidi...

DUA 85 - 93
SWALA YA MTUME 85. Soma Zaidi...

tarekh11
KUKUTANA NA BAHIRA (MTAWA) WA KIYAHUDIMzee Abu talib alikuwa ni mfanya biashara, hivyoslikuwa akimchukuwa kijana wake kwenda kwenye biashara. Soma Zaidi...

quran na sayansi
2:UUMBWAJI KWA MAJI YA UZAZIUumbwaji wa mwanadamu umepitia hatua mbalimbali na haya yote yamefanywa kwa sababumaalumu ili tipate mazingatio. Soma Zaidi...

Imam Tirmidh na Jami'u At-Tirmidh
Soma Zaidi...

sunnah
Soma Zaidi...

Adabu za kusikiliza quran
ADABU ZA KUSIKILIZA QURANI 1. Soma Zaidi...

Mapambano ya Mtume Muhammad dhidi ya Wanafiki na hila zao Madina
Soma Zaidi...

JIFUNZE DINI YA KIISLAMU, quran, hadithi, tawhid, tajwid, sira na fiqh
Jifunze mengi kuhusu dini hapa Soma Zaidi...