Haki na wajibu wa mtoto kwa wazazi na katika jamii

Haki na wajibu wa mtoto kwa wazazi na katika jamii

Wajibu wa Watoto kwa Wazazi



Wajibu wa watoto kwa wazazi wao ni kuwatii katika kiwango cha hali ya juu, kuwaheshimu na kuwahurumia hasa wanapokuwa wazee. Kuwatii wazazi ni kitendo kinachochukua nafasi ya juu sana katika Uislamu. Utii kwa wazazi huchukuwa nafasi baada tu ya Kumtii Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Msisitizo wa kuwatii wazazi, kuwaonea huruma na kuwafanyia ihsani uko wazi katika Qur-an:


Na Mola wako amehukumu kuwa msimuabudu yeyote ila Yeye tu. Na (ameagiza) kuwafanyia wema (mkubwa) wazazi. Kama mmoja wao akifikia uzee pamoja nawe, au wote wawili, usiwaambie hata A/i! Wala usiwakemee. Na useme nao kwa msemo wa heshima kabisa. Na uwainamishie bawa ?a unyenyekevu kwa (kuwaonea) huruma na useme: 'Mola wangu! Warehemu (wazee wangu) kama walivyonilea katika utoto ". (17:23-24).



Wazazi, hasa mama, wamestahiki kutiiwa kwa kiwango cha hali ya juu, kuwafanyia ihsani na kuhurumiwa na watoto wao hasa wanapokuwa wazee, iii iwe kama malipo ya kazi ngumu ya kuwalea watoto wao. Mtoto hana malipo ya kumlipa mzazi wake kwa kumzaa na kumlea mpaka kufikia utu uzima wake. Malipo anayotakiwa na Mwenyezi Mungu (s.w)


awalipe wazazi wake kwa taabu zote walizochukua katika kumlea ni kumshukuru Mwenyezi Mungu (s.w) na wazazi wake kwa kumtii Mwenyezi Mungu (s.w) na Mtume na kisha kuwatii wazazi wake, kuwafanyia ihsani na kuwahurumia kama tunavyojifunza katika Qur-an:


Na tumemuusia mwanaadamu (kuwafanyia ihsani) wazazi wake - mama yake amechukua mimba yake kwa udhafujuu ya udhafu na kumnyonyesha katika kipindi cha miaka miwili - (tumemuusia) ya kwamba unishukuru Mimi na wazazi wako, marejeo yenu ni kwangu. (31:14)


Na tumemuusia mwanaadamu afanye wema kwa wazazi wake,.Mama yake amechukua mimba yake kwa taabu. Na ku be ha mimba yake hata kumwachisha ziwa, (uchache wake) ni miezi thelathini (46:15). Pia mtoto mwema, pamoja na kuwatii na kuwahurumia wazazi wake kwa kuwapa kila msaada wanaohitajia, huwaombea dua wakiwa hai au wakiwa wametangulia kufa kwa kusema:


Mola wetu! Unighufirie mimi na wazazi wangu wote wawili na wanaoamini Siku ya Hisabu. (14:41). Utii kwa wazazi unatakiwa uendelezwe hata baada ya kufa kwao kama tunavyojifunza katika hadithi: Abu Usaydi as-Said (r.a) amesimulia: Tulikuwa karibu na Mtume (s.a.w) wakati alpomjia mtu wa ukoo wa Salimah na kumuuliza: Ee Mtume wa mwenyezi Mungu! Kuna utii


mwingine uliobakia kwa wazazi baada ya kutawafu kwao? "Ndio" alUibu Mtume. "Kuwaombea dua, kuwaombea msamaha na maghfira kwa Mwenyezi Mungu (s.w), kutekeleza wasia wao, kuwa na uhusiano mwema na wale mliofahamiana kutokana na wao na kuwaheshimu rafiki zao ". (Abu Daud, Ibn Majah)



Pia katika hadithi iliyosimuliwa na Ibn Umar mtume (s.a.w) amesema:
Utii wa hali ya juu kwa wazazi ni mtu kufanya urafiki na marafiki wa baba yake baada ya kufa kwake. (Muslim).
Hata hivyo, kiwango cha utii na huruma ya mtoto kwa wazazi wawili kinatofautiana. Mama anastahiki kupata nafasi ya kwanza ndio baba afuatie kama tunavyojifunza katika hadithi:



Abu Hurairah amesimulia kuwa mtu mmoja aliuliza: Ee Mtume wa Mwenyezi Mungu! Ni nani hasa anayestahiki upendo wangu wa hali ya juu? 'Mama yako ", alijibu Mtume. Kisha akauliza tena: Nani anayefuatia? "Mama yako ", alijibu Mtume. Akauliza tena: Nani anayefuatia? 'Mama yako ' alj/ibu Mtume. Katika maelezo mengine al/ibu Mtume: Mama yako, kisha mama yako, kisha mama yako, kisha baba yako, kisha jamaa zako wa karibu, (Bukhari na Muslim).




                   


Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 284

Post zifazofanana:-

chimbuko la sheria katika uislamu, hukumu za sheria na kuyatambua yaliyo halali na haramu
Soma Zaidi...

Sifa za waumini katika quran
Soma Zaidi...

Dhana ya haki na uadilifu katika uislamu
HAKI NA UADILIFU KATIKA UISLAMU. Soma Zaidi...

Nini maana ya Kibri, madhara yake na kujiepusha na kibri
17. Soma Zaidi...

JINSI YA KUDOWNLOAD VIDEO YOUTUBE
NJIA RAHISI YA KUDOWNLOAD VIDEO YOUTUBE Teknolojia ya mawasiliano ni muhimu katika kuhakikisha kuwa ulimwengu unafikika kama kijiji kimoja na hapa ndipo unapata maana halisi ya neno UTANDAWAZA yaani kwa lugha ya kimombo ni globalization. Soma Zaidi...

DUA 11 - 20
11. Soma Zaidi...

Kiapo ya Mtume Ayub na utekelezwaji wake
Mkewe Ayyuub(a. Soma Zaidi...

Juhudi za Waislamu Katika Kuhuisha Harakati za Kiislamu Zama za Nyerere hadi leo
i. Soma Zaidi...

Kisa cha Israa na Miraji na kufaradhishwa swala tano
Safari ya Mi'rajKatika mwaka wa 12 B. Soma Zaidi...

Mipaka katika kumtii mzazi, na mambo yasiyopasa kumtii mzazi
Soma Zaidi...

Hadithi inayotaja nguzo tano za uislamu
' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ' ': ' ' ' '?... Soma Zaidi...

Chemsha bongo namba 23
18. Soma Zaidi...