Mafunzo yatokanayo na Historia ya Nabii Yunus(a.s)

Mafunzo yatokanayo na Historia ya Nabii Yunus(a.s)

(i) Allah(s.

Jiunge nasi WhatsApp
Upate Update zetu

Mafunzo yatokanayo na Historia ya Nabii Yunus(a.s)

Mafunzo yatokanayo na Historia ya Nabii Yunus(a.s) Kutokana na Historia ya Nabii Yunusi(a.s) tunajifunza yafuatayo:

(i) Allah(s.w) ni mwingi wa kusamehe na mwingi wa kurehemu, hivyo waumini wamuelekee Allah kumuomba msamaha hata kama wamefanya kosa kubwa kiasi gani.



(ii) Toba inayokubaliwa pamoja na sharti nyingine ni ile inayoletwa kabla ya muda wa hukumu ya adhabu ya Allah (s.w) au kabla ya kufikwa na mauti:

Hawana toba wale ambao hufanya maovu mpaka mauti yamemhudhuria mmoja wao, (hapo) akasema: “Hakika mimi sasa natubu.” Wala (hawana toba) wale ambao wanakufa katika hali ya ukafiri. Hao tumewaandalia adhabu iumizayo. (4:18)


(iii) Katika kazi ya Da’awah (kulingania Uislamu) tusiwakatie tamaa watu bali tuendelee nao kwa kubadilisha mbinu mpaka mwisho wa uhai wetu au mpaka Allah(s.w) apitishe hukumu yake. Tumuige Nabii Nuhu(a.s) kwa subira (alilingania kwa miaka 950) na tusirudie kosa la kukosa subira la Nabii Yunus(a.s).



(iv) Matendo mema na ucha-Mungu, huwa ni sababu ya dua na toba ya mja kuwa kabuli mbele ya Allah(s.w).

“Basi isingelikuwa ya kwamba yeye (Yunus) alikuwa miongoni mwa waliokuwa wanamuabudu (Allah(s.w) vilivyo) bila shaka angalikaa tumboni mwaka (huyo samaki) mpaka siku watakayofufuliwa (viumbe)”. (37:143-144)



                   

Download Post hii hapa

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Sira Main: Dini File: Download PDF Views 1327

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉2 kitabu cha Simulizi    👉3 Kitau cha Fiqh    👉4 Bongolite - Game zone - Play free game    👉5 Madrasa kiganjani    👉6 Kitabu cha Afya   

Post zinazofanana: