Musa(a.s) Ahamia Madiani

Musa(a.s) Ahamia Madiani

Mchana wa siku moja Musa(a.

Jiunge nasi WhatsApp
Upate Update zetu

Musa(a.s) Ahamia Madiani

Musa(a.s) Ahamia Madiani


Mchana wa siku moja Musa(a.s) alimuona mtu wa Firauni amemuelemea Muisrail akimtwanga makonde mazito. Musa alichukizwa na kitendo kile, hivyo alipoombwa msaada alijikuta amemtwika Mmisri huyo ngumi nzito na kumuuwa palepale. Hapo Musa(a.s) akashituka na kuleta toba:



Mola wangu! Bila shaka nimedhulumu nafsi yangu, basi nisamehe; naye (Allah) akamsamehe. Kwa hakika yeye ni Mwingi wa kusamehe, Mwingi wa kurehemu. (28:16)

Akasema: Mola wangu! Kwa kuwa umenineemesha, basi sitakuwa kabisa msaidizi wa watu wabaya. (28:17)



Habari ile ya kuuliwa mtu na Musa(a.s) ilifika kwa Firaun na ikatoka shauri kuwa Musa(a.s) akamatwe na kuuliwa. Musa(a.s) alipopata habari za kuaminika kutoka kwa mtu mwema,kuhusu hukumu ile, aliamua kutorokea nchini Madian katika mji awa Al-Bid uliopo kilometa 480 hivi mashariki ya Misr. Alipofika Madian hakuwa na pakwenda bali alijipumzisha kisimani ambapo aliwasaidia wasichana wawili kuwanywesha wanyama wao. Wasichana wale hawakuweza kupigana vikumbo na wanaume katika kunywesha wanyama wao, wakawa tu wanabakia pembeni wanaangalia. Kitendo kile kilimfurahisha Mzee wa Madian na akaagiza Musa(a.s) aitwe ili apate ujira wa kazi ile.



Basi akamjia mmoja katika (wasichana) wale wawili, anakwenda na huku anaona haya, akasema: โ€œBaba yangu anakuita ili akulipe ujira wa kutunyweshea..........(28:25)

Musa alipofika kwa yule mzee alimsimulia hali halisi kuhusu dhulma, ukandamizaji na ukiukwaji wa haki za binadamu uliopo nchini Misri, pamoja na kisa kilichompelekea yeye kuhamia Madiani. Yule mzee akamtuliza Musa(a.s), akasema: Usiogope umekwisha kuokoka na watu madhalimu (28:25)




Akasema: Mimi nataka nikuoze mmoja wapo katika binti zangu hawa wawili kwa kunitumikia miaka minane na kama ukitimiza kumi hiari yako, lakini mimi sitaki kukutaabisha utanikuta Inshaa-Allah miongoni mwa watu wema .(28:27)



Musa(a.s) aliafiki suala hilo, na mmoja katika wale mabinti aliridhia kuolewa na Musa(a.s) kwa mahari ya kutoa nguvukazi:
โ€œAkasema(Musa: โ€œMapatano) hayo yamekwisha kuwa baina yangu na baina yako; muda mmoja wapo nitakaoumaliza, basi nisidhulumumiwe; na Mwenyzi Mungu ni Mlinzi juu ya haya tunayoyasema.โ€(28:28)



                   

Download Post hii hapa

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Sira Main: Dini File: Download PDF Views 1241

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 Kitau cha Fiqh    ๐Ÿ‘‰2 Madrasa kiganjani    ๐Ÿ‘‰3 Simulizi za Hadithi Audio    ๐Ÿ‘‰4 kitabu cha Simulizi    ๐Ÿ‘‰5 Bongolite - Game zone - Play free game    ๐Ÿ‘‰6 Kitabu cha Afya   

Post zinazofanana:

Historia ya Vijana wa Pangoni
Historia ya Vijana wa Pangoni

Makafiri wa Kiquraish walikuwa na tabia ya kumghasi Mtume(s.

Soma Zaidi...
Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Lut (a.s)
Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Lut (a.s)

(i) Tujitahidi kwa kadiri ya uwezo wetu kuondoa maovu katika jamii kwa mikono yetu na ikiwa hatuwezi tuyakemee kama alivyofanya Nabii Lut(a.

Soma Zaidi...
Ni nani alikuwa sahaba wa mwisho kufariki
Ni nani alikuwa sahaba wa mwisho kufariki

Katika somo hili utakwenda kujifunza kuhusu nani alikuwa wamwisho kufariki katika masahaba wa Mtume kwa mujibu wa historia

Soma Zaidi...
Mafunzo yatokanayo na vita vya uhudi
Mafunzo yatokanayo na vita vya uhudi

Dola ya uislamu madinah (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Mji wa Makkah na kabila la kiqureish
Mji wa Makkah na kabila la kiqureish

Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...