Khalifa na Utungaji Sheria, na utiifu juu ya sheria na usimamiaji wa haki

Khalifa na Utungaji Sheria, na utiifu juu ya sheria na usimamiaji wa haki

Jiunge nasi WhatsApp
Upate Update zetu

Khalifa na Utungaji Sheria, na utiifu juu ya sheria na usimamiaji wa haki

Khalifa na Utungaji Sheria



Khalifa kama ilivyokwishaoneshwa sio mtungaji wa sheria kama ilivyo kwa marais wa leo na mabunge yao. Khalifa ni mtekelezaji wa sheria za Mwenyezi Mungu na msimamizi mkuu wa sheria za Mwenyezi Mungu. Katika kipindi cha Ukhalifa vyanzo vya sheria vilibakia kuwa Qurโ€™an, Sunnah na Ijmaa na baadaye Umar, Khalifa wa pili, aliongeza Qiyas. Kwa hali hii Ufalme katika Dola ya Kiislamu ulibaki kuwa ni wa Mwenyezi Mungu tu.


Siku za mwanzo za ukhalifa kuliundwa tume ya sheria (Ofisi ya Mufti) ilipotokea haja. tume hii iliitwa na kupitisha uamuzi. Tume ya sheria ya Khalifa ilifanya kazi kwa kutegemea vyanzo vya sheria vilivyotajwa katika masuala ya kawaida, maamuzi ya tume yalikidhi haja. Lakini yalipotokea masuala yasiyo ya kawaida na yenye umuhimu wa kitaifa ilikaa majlis ya Answar, Muhajirin, wawakilishi wa Aus na Khazraj na kupitisha maamuzi; kwa mfano baada ya kutekwa kwa Iraq na Syria wapo maswahaba waliotaka ardhi igawiwe kwa askari waliopigana. Majlis iliyojumuisha Ansar, Muhajirin na watu mashuhuri watano watano kutoka makabila ya Aus na Khazraj ilifanyika kuamua suala hili.


Baada ya mjadala mrefu Khalifa Umar alifanikiwa kuwaelewesha wajumbe wa majlis kwa kunukuu aya nyingi kuthibitisha kuwa katika ardhi hata vizazi vijavyo vina hisa kwa hiyo ardhi isigawiwe kwa askari waliopigana lakini waachiwe wenyewe waliotekwa na kodi itakayotokana na ardhi hii wagawiwe askari katika mfumo wa kiinua mgongo cha kila mwaka.


Hivyo ni dhahiri mkono wa Khalifa haukuwa juu ya sheria bali chini ya sheria ya Mwenyezi Mungu, kwa namna hii haikuwezekana kupendelea kundi au mtu yeyote au kuipinda sheria kwa kumpendelea kundi fulani. Hivyo kulikuwa na usawa kamili mbele ya sheria. Hali kadhalika katika masuala ya kodi kulikuwepo usawa na haki za kiraia. Hali hii ilipelekea mshikamano miongoni mwa waumini, uhuru wa maoni, haki katika jamii na kubwa kabisa ni kuwavumilia wafuasi wa dini nyingine.




                   


Download Post hii hapa

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Sira Main: Dini File: Download PDF Views 589

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 Simulizi za Hadithi Audio    ๐Ÿ‘‰2 Bongolite - Game zone - Play free game    ๐Ÿ‘‰3 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    ๐Ÿ‘‰4 Kitabu cha Afya    ๐Ÿ‘‰5 Kitau cha Fiqh    ๐Ÿ‘‰6 kitabu cha Simulizi   

Post zinazofanana:

Sifa au vigezo vya dini sahihi
Sifa au vigezo vya dini sahihi

Dini sahihi anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Historia ya Vijana wa Pangoni
Historia ya Vijana wa Pangoni

Makafiri wa Kiquraish walikuwa na tabia ya kumghasi Mtume(s.

Soma Zaidi...
Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Salih(a.s)
Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Salih(a.s)

Mafunzo tuyapatayo hayatofautiani na yale yatokanayo na Historia ya Nabii Hud(a.

Soma Zaidi...
Maandalizi ya Kimafunzo aliyoandaliwa Mtume Muhammad
Maandalizi ya Kimafunzo aliyoandaliwa Mtume Muhammad

(i) Suratul- โ€˜Alaq (96:1-5)โ€œSoma kwa jina la Mola wako aliyeumba Aliyemuumba mwanaadamu kwa โ€˜alaq.

Soma Zaidi...
Kuandaliwa kwa Muhammad kabla ya kupewa utume
Kuandaliwa kwa Muhammad kabla ya kupewa utume

Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Mtume (s.a.w) alivyoandaa ummah wa kiislamu makkah
Mtume (s.a.w) alivyoandaa ummah wa kiislamu makkah

Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Lut (a.s)
Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Lut (a.s)

(i) Tujitahidi kwa kadiri ya uwezo wetu kuondoa maovu katika jamii kwa mikono yetu na ikiwa hatuwezi tuyakemee kama alivyofanya Nabii Lut(a.

Soma Zaidi...
Mafunzo ya sura zilizochaguliwa
Mafunzo ya sura zilizochaguliwa

Quran (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Maandalizi ya hijrah ya mtume na waislamu kuhamia madinah
Maandalizi ya hijrah ya mtume na waislamu kuhamia madinah

Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...