Haikufundisha Mtume Muhammad quran kwa lengo la kurekebisha tabia za waarabu

Haikufundisha Mtume Muhammad quran kwa lengo la kurekebisha tabia za waarabu

Haikufundisha Mtume Muhammad quran kwa lengo la kurekebisha tabia za waarabu

(viii)Dai la Kurekebisha Tabia ya Waarabu:



Miongoni mwa wale wanaosema kuwa Muhammad (s.a.w) ndiye aliyetunga Qur-an wapo wanaodai kuwa Muhammad (s.a.w) alifanya hivyo kwa nia nzuri ya kutaka kujenga tabia na mwenendo mzuri miongoni mwa ndugu zake Waarabu. Yaani, Muhammad (s.a.w) alichukizwa sana na tabia mbaya walizokuwa nazo


Waarabu wa zama zake na hivyo akaona lazima ajitahidi kuziondoa. Na ili afanikishe lengo lake hilo akaona atunge Qur-an na asingizie kuwa inatoka kwa Allah (s.w). Dai hili pia halina nguvu kwa sababu zifuatazo:



Kwanza, kujenga mwenendo mzuri wa tabia za watu ni jambo jema ambalo laweza kutekelezwa pasi na kutumia udanganyifu na uovu mwingine. Ni kipi kilichomfanya Muhammad (s.a.w) atumie uwongo na udanganyifu ili awafundishe watu kuwa wa kweli na waaminifu?



Pili, Qur-an imeitaja dhambi ya kuzua uwongo kuwa ni miongoni mwa madhambi makubwa:


"Na nani dhalimu mkubwa kuliko yule amtungiaye uwongo Allah au mwenye kusema: "Nimeletewa wahyi," na hali hakufunuliwa chochote; na yule asemaye: "Nit ateremsha (ufunuo) kama ule aliouteremsha Allah." Na kama ungewaona madhalimu watakapokuwa katika mahangaiko ya mauti, na Malaika wamewanyooshea mikono yao (na kuwaambia): "Zitoeni roho zenu! Leo mtalipwa adhabu ifedheheshayo kwa sababu ya yale mliyokuwa mkiyasema juu ya Allah pasipo haki na kwa vile mlivyokuwa mkizifanyia kiburi Aya zake." (6:93)



Aya hii inasema hakuna dhalimu mkubwa kuliko yule mtu ambaye atamzulia uwongo Allah au atakayesingizia kuwa amepata wahyi kutoka kwa Allah na ilhali hakupata.Halafu aya hii inataja jinsi watu wa aina hiyo watakavyofedheheshwa na jinsi watakavyopapatika wakati wa kutolewa roho zao.



Lau kama Muhammad (s.a.w) angekuwa ndiye aliyeitunga halafu akamsingizia Allah (s.w), asingeiweka aya kama hii katika Qur-an kwa sababu angehisi kuwa anajitukana mwenyewe na kujilaani mwenyewe. Pia kwa kuhofia kuwa yaweza kutokezea siku ambayo watu watamgundua angehakikisha kuwa anaiandika aya hii kwa namna ambayo haitamfedhehesha hapo atakapojulikana.



Angeweza kwa mfano kusema: "Hapana lawama kwa wale ambao, ikiwa hapana budi kusema uwongo kwa ajili ya Allah." St. Paulo kwa mfano ameandika hivi katika Biblia:
Lakini ikiwa kweli ya Mungu imezidi kudhihirisha utukufu wake kwa sababu ya uongo wangu, mbona mimi ningali nahukumiwa kuwa ni mwenye dhambi." (Warumi 3:7)
Aidha madai kuwa Muhammad (s.a.w) alitunga Qur-an ili aitumie katika kurekebisha mwenendo wa tabia za watu pia yanatenguliwa na ukweli kwamba Qur-an haikushuka yote mara moja bali ililetwa kidogo kidogo kwa muda wa miaka 23. Na katika kipindi hicho Qur-an ilitoa ahadi ya kujibu maswali yote yatakayoulizwa wakati Qur-an bado inashuka.


Na kama mtayauliza, maadam inateremshwa Qur-an mtabainishiwa " (5:101)
Watu waliitumia fursa hiyo iliyotolewa na Qur-an kuuliza maswali mbali mbali kama vile juu ya ulevi, kamari, hedhi, ngawira, roho na hata juu ya watu kama Dhur-qarnain. Katika kuyajibu maswali hayo


Qur-an imetumia msemo "Wanakuuliza juu ya jambo kadhaa. Sema: Lipo namna kadhaa." Kwa mifano halisi tazama Qur-an 2:189, 2:215, 2:217, 2:219, 2:220, 2:222, 5:4, 7:187, 8:1, 17:85, 18:83, 20:105 na 79:42.



Tatizo linalojitokeza hapa ni kwamba Muhammad (s.a.w) asingeweza kujua kuwa maswali aliyowaruhusu watu kuuliza yatakuwa yanahusu marekebisho ya mwenendo na tabia za watu. Kwani inadaiwa kuwa haitakuwa jambo la busara kwa rais anayetaka kuzungumzia hali ya chakula nchini mwake kuwaita waandishi wa habari na kuwaruhusu waulize maswali yoyote yanayowatatiza. Rais huyo atakuwa na hakika gani kuwa watauliza juu ya hali ya chakula na siyo juu ya wafungwa wa kisiasa?




                   


Bongoclass
Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya hapa chini kuipakua sasa!

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Quran Main: Dini File: Download PDF Views 1143

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Bongolite - Game zone - Play free game    👉2 Simulizi za Hadithi Audio    👉3 Kitabu cha Afya    👉4 kitabu cha Simulizi    👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉6 Kitau cha Fiqh   

Post zinazofanana:

quran na sayansi
quran na sayansi

2:UUMBWAJI KWA MAJI YA UZAZIUumbwaji wa mwanadamu umepitia hatua mbalimbali na haya yote yamefanywa kwa sababumaalumu ili tipate mazingatio.

Soma Zaidi...
Sababu za kushuka surat an-Nas na surat al Falaq
Sababu za kushuka surat an-Nas na surat al Falaq

Sura mbili hizi pia hujulikana kwa jina la al muawidhatain ambazo ni surat an Nas na surat al falaq.

Soma Zaidi...
Sura za makkah na madinah
Sura za makkah na madinah

Quran (EDK form 3: Dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
As-Sab nuzul
As-Sab nuzul

Sababu za kuteremshwa baadhi ya sura Katika darsa hii tutaangalia sababu za kushuka kwa aya na sura ndani ya quran.

Soma Zaidi...
sura ya 11
sura ya 11

Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa

Soma Zaidi...
Hukumu za Tajwid katika usomaji wa bismillah (basmalah)
Hukumu za Tajwid katika usomaji wa bismillah (basmalah)

Hapa utajifunza kanuni za tajwid katika kusoma bismillah au basmalah.

Soma Zaidi...
HUKUMU ZA IDGHAM
HUKUMU ZA IDGHAM

Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa

Soma Zaidi...
Fadhila za kusoma surat al Kahaf siku ya Ijumaa
Fadhila za kusoma surat al Kahaf siku ya Ijumaa

Je unajuwa ni kwa nini unatakiwa usikose kusoma surat al Kahaf siku ya ijumaa. Makala hii itakujibu swali hili

Soma Zaidi...