Faida za kula tikiti

Faida za kula tikiti

Ukubwa wa tikiti unasadifu yaliyopo, kwani kuna fgaida akubwa sana za kiafya katika kula tikiti

Jiunge nasi WhatsApp
Upate Update zetu

Faida za kula tikiti

8.Tikiti (watermelon). Tunda hili pia ni katika matunda yenye vitamin C na A kwa wingi. Tafiti za kisayansi pia zinaonesha kuwa tunda hili lina antioxidant ambazo ni pamoja na lycopene, carotenoid na cucurbitacin E. Hizi husaidia katika kuzuia mwili usipate saratani au kupunguza athari za saratani. Tikiti husaidia katika kupata choo kwa urahisi.

Antioxidant zilizopo kwenye tunda hili husaidia kuzuia saratani ya mfumo wa mmengenyo wa chakula na kuota kwa vimbe ambazo ni viashiria vya saratani. Lycopene husaidia katika kuimarisha afya ya moyo kwa kuwa zina uwezo wa kupunguza cholesterol na shinikizo la damu. Katika matunda yote tikiti linajulikana kuwa ndio tunda lenye maji mengi. Lina asilimia 92% ya maji.

Ndani ya tikiti kuna virutubisho kama vitamini C, Vitamin A, vitamini B1, B5, na B6. pia kuna madini ya potassium, magnesium. Vitamin C ni antioxidant ambayo husaidia katika kuzuia uharibifu wa seli kutokana na mionzi. Ndni ya tikiti kuna carotenoid hizi ni chembechembe ambazo mwili huweza kuzibadilisha na kuwa Vitamini A. pia chembecheme ziitwazo lycopene hizi ndizo zinazolipa tikiti rangi nyekundu. Chembechembe hizi zinafaida chingi za kiafya mwilini.

Tafiti za kisayansi zinaonesha kuwa tikiti lina chembechembe ambazo husaidia kuatika kupunguza athari za ugonjwa wa saratani. Mingoni mwa chembechembe hizo ni lycopene. Kitaalamu hizi huitwa anti-cancer. Hizi hupunguza athari za saratani kwa kuwa hupunguza uzalishaji wa IGF (Insulin-like Growth Factor) hii ni aina ya protini ambayo hutumika katika uzalishaji wa seli yaani cell division. Wataalamu wa sayansi wanaeleza kuwa IGF ina mahusiano makubwa na ugonjwa wa saratani. Pia ndani ya tikiti kuna cucurbitacin Eb hii husaidia katika kuzuia uotaji wa uvimbe wa saratani (growth of tumor).

Tikiti husaidia katika kupunguza athari za kupata maradhi ya moyo kama vile kiharusi, shambulio la moyo na presha. Tafiti zinaonesha kuwa lycopene husaidia katika kupunguza kiwango cha cholesterol na kupunguza shinikizo la damu.pia lycopene husaidia katika kupunguza unene wa ukuta wa mishipa ya artery (mishipa mikubwa ya damu). pia tikiti lina citrulline, ambazo ni amino acid hizi husaidia katika kutanua mishipa ya damu hivyo kupunguza presha (yaani shinikizo la damu). pia vitamini na madini mengine tulotaja huko juu ambayo yamo kwenye tunda hili husaidia katika afya ya moyo. Kama vitamini A, B6 na C pia madini ya magnesium na potassium.

Tikiti ni tunda safi kwa afya ya ngozi na nywele. Uwepo wa vitamini A na C kwenye tunda hili kunalifanya tunda hili liwe muhimu katika nyanya hizi za ubora wa ngozi na nywele. Vitamin C husaidia mwili wako kutengeneza collagen, hizi ni protini ambazo hizi huweza kufanya ngozi yako iwe laini na rahisi kukunyika na kuzifanya nywele zako ziwe na afya na mathubuti. Pia vitamin A kusaidia katika kutengenezwaji wa seli mwilini hivyo husaidia katika ukuaji wa nywele. Bila ya vitamini A ngozi yako itaonekana kavu na isiyo ya kawaida. Vitamini A na C husaidia katika kuzuia ngozi yako kuungua na jua.


                   

Download Post hii hapa

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Vyakula Main: Afya File: Download PDF Views 1075

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya    👉2 Kitau cha Fiqh    👉3 Bongolite - Game zone - Play free game    👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉5 Madrasa kiganjani    👉6 kitabu cha Simulizi   

Post zinazofanana:

Faida za kula viazi mbatata
Faida za kula viazi mbatata

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula viazi mbatata

Soma Zaidi...
Faida za kula uyoga
Faida za kula uyoga

Kula uyoga kwa faida kubwa, ja unazijuwa faida za kula uyoga kiafya

Soma Zaidi...
Faida za kiafya za kula panzi, senene na kumbikumbi
Faida za kiafya za kula panzi, senene na kumbikumbi

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula panzi senene na kumbikumbi

Soma Zaidi...
Madhara ya kula chakula chenye chumvi nyingi
Madhara ya kula chakula chenye chumvi nyingi

Posti hii inakwendavkukufundisha madhara unayoweza kuyapata unapokula chakula cgenye chumvi nyingi

Soma Zaidi...
Faida za kiafya za kula magimbi/ taro roots
Faida za kiafya za kula magimbi/ taro roots

Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula magimbi

Soma Zaidi...
Faida za kiafya za kula mihogo
Faida za kiafya za kula mihogo

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kula mihogo

Soma Zaidi...
Vyakula vya madini kwa wingi, na kazi za madini mwilini
Vyakula vya madini kwa wingi, na kazi za madini mwilini

Utajifunza vyakula vyenye madini kwa wingi, kazi za madini mwilini na athari za upungufu wake

Soma Zaidi...
Faida za kula Embe
Faida za kula Embe

Embe ni katika matunda atamu na yenye faida kubwa kiafya, soma makala hii hadi mwisho

Soma Zaidi...
Faida za kiafya za kunywa maziwa
Faida za kiafya za kunywa maziwa

Somo Hili linakwenda kukueleza kuhusu faida za kiafya za kunywa maziwa

Soma Zaidi...