Mbu ni katika wadudu wanaopatikana maeneo yenye joto hususan maeneo ynye hali ya hewa ya kitropik.
Mbu ni katika wadudu wanaopatikana maeneo yenye joto hususan maeneo ynye hali ya hewa ya kitropik. Mbu anafahamika kwa kuwa ndiye msambazaji mkubwa wa malaria pamoja na matende na ngiri maji. Chakula cha mbu ni maji, bakteria pamoja na damu. Mbu dume huweza kumjua mwanamke kwa kutumia sauti ya mbawa. Mbu ni katika wadudu wadogo lakini wana maajabu makubwa. Katika mkala hii tutaangalia kwa ufupi mambo matano kuhusu mbu.
Tofauti na kuwa mbu ni mdogo lakini anaweza kunyonya damu iliyokuwa nzito kuliko mwili wake. Yaani sawa na mtu mwenye uzito wa kilo 70 kula chakula chenye uzito wa kilo 100. mara mbu anaponyonya damu mwili wake huchukuwa mpaka siku tatu kuweza kuimeng’enya damu ile na kuimaliza. Baada ya hapo mbu atakwenda kunyonya damu tena. Itambulike kuwa chakula cha mbu ni bakteria, maji pamoja na damu. Mbu jike hula damu pindi anapotaka kutaga. Wataalamu wanaeleza kuwa kuna aina 2000 za mbu.
Kabla ya mbu kutaga mayai yake anaanza kupima ardhi kama ina majimaji pamoja na joto la kutosha kwa maisha ya mayai yake. Mbu hutaga mayai juu ya maji, ardhi, miti na nyasi pamoja na maeneo mengine yaliyo na majimaji. Pia mbu anaweza kutaga yai lake hata pakiwa na maji kiasi cha tone moja tu. Nayai ya mbu ni chakula kwa samaki pamoja na watutu wengine hivyo mbu huwa makini sana wakati wa kutaga mayai yake.
Tofauti na wadudu wengine na ndege mbu anaweza kulizuia yai lake tumboni kulitaga pindia anapohofia usalama wa yai lake. Kuku na ndege wengine yai linapofikia kutagwa hana namna lazima akalitage, lakini hii ni tofauti kwa mbu. Yai la mbu linaweza kukaa kwa muda wa miaka miwili bila ya kufa na ndo maana ni vigumu kutokomeza kabisa mbu.
Yai la mbu lina rangi ya njano, tangi hii ni rahisi kulifanya yai hili lionewe na maadui walao mayai ya mbu. Hivyo ifikapo usiku yai la mbu hubadilika rangi na kuwa jeusi. Hali hii husaidia kuliepusha yai la mbu kuliwa na maadua. Pia yai la mbu halizami ndani ya maji, na linaweza kuelea hewani, njia zote hizi husaidia ulinzi wa yai hili lisidhuriwe.
Ijapokuwa mbu anakula binadamu lakini na yeye ni chakula kwa viumbe vingine kama popo. Hivyo popo hutusaidia katika mapambano dhidi ya wadudu hawa hatari. mbu pia anaweza kujuwa wati mtu yupo kwa kutumia pumzi anayopumua mwanadamu
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Posti hii inahusu zaidi vyanzo vya magonjwa yanayotokea kwenye sehemu za siri,kwa sababu siku kwa siku kuna magonjwa mengi yanayotokea kwenye sehemu za siri ila kuna vyanzo mbalimbali ambavyo usababisha kuwepo kwa magonjwa kwenye sehemu mbalimbali za siri
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu njia za kupambana na kisukari
Soma Zaidi...Post hii itakwenda kuzungumzia ugonjwa wa gout unaosababishwa na ongezeko la asidi mwilini.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu huduma kwa wanawake wenye mahitaji maalum, ni wanawake ambao wana shida ya akili, walionyanyaswa kijinsia, wakimbizi na wote wenye matatizo mbalimbali.
Soma Zaidi...Vidonda vya tumbo no tatizo linalotokea baada ya kuta za tumbo au utumbo mdogo kuwa na vidonda,hutokea baada ya ukuta wenye ute unaozuia kemikali za kuyeyusha chakula unaitwa mucus kuharibika. Vidonda vya tumbo (peptic ulcers) imegawanyika katika ma
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukuletea sababu za maumivu ya tumbo kitovu i
Soma Zaidi...Makala hii inakwenda kukufahamishavkuhusu saratani yavkibifu cha mkojo.
Soma Zaidi...Kuzama hufafanuliwa kama mchakato unaosababisha upungufu mkubwa wa kupumua kutokana na kuzamishwa kwenye chombo cha kuogelea (kioevu). Kuzama hurejelea tukio ambalo njia ya hewa ya mtoto huzamishwa kwenye kioevu, na kusababisha kuharibika kwa kupumua.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi hatua mbalimbali za Ugonjwa wa Ukimwi, kawaida Ugonjwa huu huwa na hatua kuu nne ila kila hatua huwa na sifa zake kwa hiyo tunapaswa kujua hatua za Ugonjwa huu na kujaribu kuzuia maambukizi yasisambae kabisa.
Soma Zaidi...