image

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Musa(a.s) na Harun(a.s)

Kutokana na Historia ya Nabii Musa na Harun(a.

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Musa(a.s) na Harun(a.s)

Mafunzo Yatokanayo na Historia ya Nabii Musa(a.s) na Harun(a.s)

Kutokana na Historia ya Nabii Musa na Harun(a.s) tunajifunza yafuatayo:

(i) Tunajifunza kuwa ni muhimu kuweka mipango katika kuhuisha na kusimamisha Uislamu katika jamii. Allah(s.w) anauwezo wa kukiamrisha kitu “kiwe” na kikawa pale pale, lakini bado tunaona ameweka mpango wa muda mrefu wa(ii) Vile vile mpango huu wa Allah(s.w) wa kuwakomboa Bani Israil,unatufunza kuwa kuibadilisha jamii ya kijahili kuwa ya Kiislamu ni jambo linalohitaji muda na subira.(iii) Elimu na siha ni nyenzo muhimu za kumuwezesha mtu kuwa khalifa katika ardhi. Nabii Musa alipewa siha nzuri na kuruzukiwa akili na elimu.(iv) Hakuna hila wala nguvu zinazoweza kuzuia jambo analotaka Allah(s.w) liwepo au lisiwepo katika jamii, yeye anazo namna nyinyi za kumlinda mja wake na vile vile anaweza kumuangamiza mbabe yeyote awaye.(v) Tabia njema na kuwatendea watu wema ni nyenzo muhimu katika harakati za kusimamisha Uislamu katika jamii. Nabii Musa(a.s)kwa wema wake aliletewa taarifa ya mipango ya Firaun dhidi yake; pia kwa huruma yake alipata hifadhi kwa mzee wa Madian.(vi) Hakuna binaadamu asiyeteleza na kumkosea Allah(s.w), lakini muumini anakuwa mwepesi wa kurejea kwa Allah (s.w).Musa(a.s) aliteleza kwa kuingilia ugomvi asioujua na kumuua mtu,alirejea kwa Mola wake haraka haraka–Qur-an (28:16).(vii)Muumini wa kweli hanabudi kuchukia vitendo vya dhuluma na kuwa tayari kuwatetea wanaodhulumiwa haki zao kwa kadiri ya uwezo wake.(viii)Ni muhimu kuwekeana mikataba ya kazi tunapoajiri au kuajiriwa. Nabii Musa(a.s) aliwekeana mkataba wa kazi na mzee wa Madian.(ix) Nyenzo muhimu ya kutuwezesha kusimamisha Uislamu katika jamii baada ya Elimu ni kusimamisha Swala za Faradh na sunah,Qiyamullayl na kuleta dhikiri kwa wingi – Qur-an(20:14), (73:1-10), (74:1-7).(x) Miujiza ni katika dalili za kuwepo Allah(s.w).(xi) Katika harakati za kusimamisha Uislamu katika jamii tunatakiwa tusimvamie tu kila mtu na kumuingiza kwenye harakati, bali tuanze na ndugu, jamaa na rafiki wa karibu ambao tunajua fika tabia na mwenendo wao. Nabii Musa (a.s) aliomba ndugu yake Harun awe msaidizi wake si kwa kuwa alikuwa ndugu yake tu, bali alimfahamu fika kwa ucha Mungu wake.(xii)Muumini mwanaharakati hahongeki kwa fadhila atakazofanyiwa na madhalimu ili arudi nyuma katika kusimamisha uadilifu. Musa(a.s) alilelewa katika nyumba ya mfalme,lakini hakuacha kudhihirisha kwa matendo udhalimu wa Firaun na serikali yake ikawa ndio sababu ya kuhukumiwa kifo.(xiii)Ni kawaida ya matwaghuti kufanya propaganda dhidi ya wanaharakati na kuwapachika majina mabaya. Firaun na serikali yake alimpakazia Nabii Musa(a.s) uwendawazimu na uchawi.(xiv)Hapana yeyote wa kumchelea katika kutekeleza amri ya Allah(s.w) ya kusimamisha Uislamu katika jamii. Musa na Harun(a.s) walimkabili Firaun na wakuu wake wa Dola waliozungukwa na majeshi na kuwafikishia ujumbe wa Allah(s.w).(xv)Hapana yeyote mwenye uwezo wa kutweza au kutengua maamuzi ya nafsi ya mwanaadamu.Wachawi walipobainikiwa na Haki na wakasilimu, Firaun hakuweza kuwaritadisha pamoja na adhabu kali aliyoitoa dhidi yao – Qir-an (26:49-51).(xvi)Toba inayokubalika ni ile inayoletwa haraka kabla ya kufikwa na mauti – Qur-an (4:18).(xvii)Kuishi nje ya shahada na kutarajia kufa ndani ya shahada ni muhali. Allah(s.w) ametuamrisha tuishi na shahada na tujitahidi kubakia nayo mpaka kufa kwetu– Qur-an (3:102).                              

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 505


Sponsored links
👉1 Madrasa kiganjani     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 kitabu cha Simulizi     👉4 Kitabu cha Afya    

Post zifazofanana:-

Si Yesu Aliyesulubiwa (yesu hakufa msalabani wala hakusulubiwa
Katika Qur,an tukufu, Mwenyezi Mungu aliye muweza na mjuzi wa mambo anathibitisha kuwa aliyesulubiwa si Nabii Isa(a. Soma Zaidi...

Kuporomoka kwa Dola ya Kiislamu
Soma Zaidi...

Mambo ya Msingi Aliyofanya Mtume(s.a.w) Katika Kuanzisha Dola ya Kiislamu Madinah.
Mambo ya Msingi Aliyofanya Mtume(s. Soma Zaidi...

tarekh 01
NASABA YA MTUME (S. Soma Zaidi...

Imam Muhammad Idris al-Shafii
Soma Zaidi...

Hija ya kuaga kwa mtume, na hutuba ya mwisho aliyotowa mtume katika hija
Mwaka mmoja baada ya msafara wa Tabuuk Bara Arab zima ilikuwa chini ya Dola ya Kiislamu. Soma Zaidi...

Historia ya kujengwa kwa Alkabah (Maka)
Kama tulivyoona katika maisha ya Mtume Ibrahim(a. Soma Zaidi...

Mtume kumuoa bi khadija
Sara na historia ya Mtume Muhammad s.a.w, sehemu ya 15. Hapa utajifunza kuhusu chimbuko la ndoa ya Mtume s.a.w na bi Khadija. Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII SHUAIB
Soma Zaidi...

Fat-h Makkah (Kukombolewa Makkah) baada ya mkataba wa hudaibiya
Fat-h Makkah (Kukombolewa Makkah). Soma Zaidi...

Ugonjwa wa Mtume(s.a.w) na Kufariki kwake
Miezi miwili baada ya Hijjat-al-Wada, Mtume(s. Soma Zaidi...

Mtume alipoanza kulingania uislamu na changamoto alizokumbana nazo kutoka kwa maadua wa uislamu
7. Soma Zaidi...