HISTORIA YA MTUME AL-YASA’A(A.S)

Mtume Alyasa’a(a.s) ametajwa mara moja tu katika Qur’an na kubainishwa kuwa ni miongoni mwa watu waliofadhilishwa na Mwenyezi Mungu.

“Na (tukamwongoa) Ismail na Alyasaa na Yunus na Lut. Na wote tukawafadhilisha juu ya walimwengu (wote katika zama zao)” (6:86).Kufadhilishwa kwa Mitume hawa hakukutokana na nasaba zao wala zama za kuletwa kwao duniani. Bali kwa ujumbe waliopewa na juhudi waliyoifanya katika kuutekeleza ujumbe huo na kuufikisha kwa kaumu zao. Haya yanathibitishwa na aya zinazofuatia:

“Hao ndio tuliowapa vitabu na hukumu (Ilmu) na utume. Kama hawa (makafiri) wakiyakataa hayo, basi tumekwisha yawekea watu wasioyakataa” (6:89).

“Hao ndio ambao Mwenyezi Mungu amewaongoa, basi fuata Uongozi wao” (6:90).