Chanzo cha Mapato katika serekali ya Kiislamu wakati wa Makhalifa

Chanzo cha Mapato katika serekali ya Kiislamu wakati wa Makhalifa

Pato la Serikali



Moja ya shughuli muhimu katika uendeshaji wa Serikali ni namna Serikali ilivyopata mapato yake na ilivyotumia. Wakati wa Mtume(s.a.w) vyanzo vya pato la Serikali vilikuwa zaka, jizya, kharaj, khums na fay. Katika kipindi cha makhalifa wanne vyanzo vya pato la Serikali viliongezeka kama ifuatavyo;


Ushr; Ushr ni kodi ya mazao kutoka katika ardhi ya Waislamu iliyotekwa kivita na kugawiwa askari waliopigana au ardhi ya Serikali iliyoandaliwa kwa kilimo au mifugo. Kwa ardhi inayotegemea mvua ya asili, mabwawa na mito ya asili kima chake ni 1/10 (10%) ya mazao na kwa mashamba yanayomwagiliwa kiwango cha ushuru ni 1/20 (5%) ya pato la mwaka.


Kharaj au kodi ya Ardhi: Kodi hii iliwahusu wasio waislamu ambao ardhi yao ilitekwa kivita lakini wenyewe wameruhusiwa kuedelea kutumia ile ardhi iliyotekwa ambayo ni mali ya dola ya Kiislamu. Kodi hii iliwekewa kima maalum baada ya tathmini ya ardhi na ililipwa kwa mwaka.


Jizya; ilikuwa chanzo kingine cha pato la Taifa. Kodi hii iliwahusu wasio waislamu tu, waliojulikana kwa jina la “Dhimmi”. Serikali ya Kiislamu inachukua dhamana ya kuwalinda wasio Waislamu, wao na mali zao. Wasio Waislamu wanalipa kodi hii ya jizya ikiwa ni malipo ya kazi ya ulinzi wanayofanyiwa na Serikali. Kodi hii pia iliwekewa kiwango maalum na haikuwahusu vikongwe, watoto, walemavu na wanawake.


Zaka na Sadaqa nazo zilibakia kuwa vyanzo vya msingi vya pato la Serikali.


Ngawira ni mali inayopatikana kwa kumshinda adui. Hii nayo ilitumika kama chanzo cha pato la Serikali. Wapiganaji walichukua
asilimia 80 au (4 /5) na pato la serikkali lilikuwa asilimi 20 au ( 1/5) ya ngawira.


Fay kilikuwa ni chanzo kingine cha pato la Serikali katika kipindi cha Makhalifa. Fay ni mali iliyotolewa na adui hata bila ya kupigana.


Zaraib ni kodi za muda zilizotozwa na serikali kwa maslahi ya nchi
Mapato mengine ya Serikali yalitokana na wakfu, kodi za madini,kodi ya mali inayoingia nchini au inayopitishwa, n.k.


Kwa vyanzo hivi Serikali iliweza kukusanya mapato yaliyowezesha kuendesha Serikali bila matatizo. Palikuwa na Baitil-Mali(Hazina). Mali ya Serikali ilitumika kwa mujibu ya maelekezo ya mafungu yake, maendeleo ya nchi na wananchi kwa ujumla.


Maendeleo ya nchi yaliyopatikana wakati wa Makhalifa ni pamoja na ujenzi wa mifereji(Canals). Katika Ukhalifa wa ‘Umar(r.a)ulijengwa mfareji kutoka mto Euphrates hadi Basra kuliko kuwa na ukame wa maji. Mfreji huu uliitwa kwa jina la Gavana wa Basra, “Canal Abi Musa”. Mifereji mingine iliyojengwa kutoka Mto Euphrates ni “Canal Maakal na Canal Saad” iliyopeleka maji sehemu mbali mbali zilizokuwa kame.


Mfereji mwingine maarufu ni ule uliounganisha mto Nile na Red See (Bahari ya Shem) ambao uliitwa kwa jina la “Canal Amirul-Muuminina”.


Maendeleo mengine yaliyofanywa kutokana na pato la Serikali katika kipndi cha Makhalifa ni ujenzi wa barabara na madaraja, majengo ya ofisi, nyumba za wafanyakazi,ngome na kambi za jeshi, nyumba za wageni, majengo madhubuti ya Baitul- Mali na magereza. Visima na vituo kadhaa baina ya Makkah na Madina vilijengwa. Miji nayo ilianzishwa na maarufu katika hiyo ni Basra, Kufa, Fustat na Mosul.


Kazi ya ujenzi wa misikiti na upanuzi wa misikiti ya Makkah na Madinah ilishamiri katika kipindi cha Makhalifa. Misikiti elfu nne (4,000) inakadiriwa kujengwa katika Ukhalifa wa ‘Umar(r.a). Misikiti ya Makkah na Madina ilipanuliwa kwa kununua nyumba za majirani katika kipindi cha ‘Umar na ‘Uthman(r.a).




                   


Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea


Je umeipenda post hii ?

Ndio            Hapana            Save post
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Sira Main: Dini File: Download PDF Views 1708

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉2 Madrasa kiganjani    👉3 Simulizi za Hadithi Audio    👉4 kitabu cha Simulizi    👉5 Kitau cha Fiqh    👉6 Kitabu cha Afya   

Post zinazofanana:

Yusufu(a.s.) Akutana na Ndugu Zake

Njaa ilitokea na ikawa hapana sehemu nyingine yoyote yenye chakula ila Misri.

Soma Zaidi...
Jinsi tukio la Karatasi lilivyotokea wakati wa Mtume siku chache kabla ya kifo chake

Tukio la kartasiTukio la ‘kartasi’ lililonakiliwa katika vitabu vya Muslim na Bukhari kuwa siku tatu kabla ya kutawafu Mtume (s.

Soma Zaidi...
KIKAO CHA KUMFUKUZA MTUME MUHAMMAD KUTOKA MAKKAH (MAKA), KIKAO ALICHOHUDHURIA IBLISI

KIKAO CHAKALIWA KUJADILI HATMA YA MUHAMMAD KATIKA MJI WA MAKAHiki ni kikao kizito hakijapata kutokea toka muhammad katika ji wa maka.

Soma Zaidi...
Nasaba ya mtume

Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu)

Soma Zaidi...
Muhutasari wa sifa za wanafiki

Kwa kuzingatia aya zote tulizozipitia juu ya wanafikitunaweza kutoa majumuisho ya sifa za wanafiki kama ifuatavyo:- (1)Hutenda kinyume cha imani wanaodai kuwa nayo.

Soma Zaidi...