Mtume aliyemfuatia Nabii Adam(a.s) katika Mitume 25 waliotajwa katika Qur-an ni Idrisa(a.s).
Nabii Idrisa(a.s) ametajwa kwa ufupi katika Qur-an
βNa mtaje Idrisa katika Kitabu (hiki). Bila shaka yeye alikuwa mkweli sana (na) Nabii. Na tulimuinua daraja ya juu kabisa.β (19:56-57).
Na (mtaje) Ismail, na Idrisa na Dhul-kifli wote walikuwa miongoni mwa wanaosubiri.β (21:85)
Katika aya hizi Nabii Idrisa(a.s) ametajwa kuwa alikuwa Nabii wa Allah(s.w) aliyepea katika ukweli na subira na Allah akamnyanyua daraja ya juu kabisa kutokana na sifa zake hizo. Hatuna taarifa zaidi ya harakati za Nabii Idrisa(a.s) katika kuhuisha Uislamu na kuusimamisha katika jamii yake, bali itoshe tu kuwa mwanaharakati anayefanya kazi ya Mitume wa Allah ya kusimamisha Uislamu katika jamii hanabudi kujipamba na tabia ya ukweli na subira.
Inasemekana kuwa nabii Idrisa:-
1. Ndiye mtu wa kwanza kuandika
2. Ndiye mtume wa kwanza kutoa darsa
3. Ndiye mtu wa kwanza kushona nguo