SAFARI YA PILI YA SINBAD

SAFARI YA PILI YA SINBAD

Download kitabu Hiki Bofya hapa SAFARI YA PILI YA SINBAD Basi siku ile Sinbad mbeba mizigo aliwahi haraka sana na mapema zaidi, na akamkuta Sinbad wa baharini ameshakaa na watu wake wanamsubiri kuanza hadithi.

SAFARI YA PILI YA SINBAD

pic
Download kitabu Hiki Bofya hapa

SAFARI YA PILI YA SINBAD

Basi siku ile Sinbad mbeba mizigo aliwahi haraka sana na mapema zaidi, na akamkuta Sinbad wa baharini ameshakaa na watu wake wanamsubiri kuanza hadithi. Walipokusanyika watu wote vikaagizwa vinywaji na vileja na kuanza kula huku wakisikiliza hadithi. Sinbad wa baharini akaanza kusema โ€œbasi tambueni kuwa sfari hii ya pili nilikutwa na makubwa zaidi kuliko hii ya kwanza. Ha ilikuwa hivi:-

Basi tulipozungumza na nahodha kuwa wiki ijayo wataanza safari nilirudi nyumbani na kujiandaa kwa safari. Ndugu zangu walijaribu kunizuia lakini sikuwasikia โ€œsikio la kufa halisikii dawaโ€ wengine wakanambia najipeleka nikafe ila sikuwasikiliza. Maandalizi yalikamilika kwa siku mbili na nikawa nasubiria safari tu. Wiki ilipofika tukaanza safari kwa amani lakini siku ya tatu kabla ya kuingia kisiwa cha kwanza kufanya biashara hali ya hewe ikabadiliki ghafla.

Nikiwa na woga sana juu ya roho yangu nikabaki namuomba msamaha mwenyezi Mungu. Jahazi lilikwenda ovyo ovyo kwa muda wa masaa sita. Manahodha walifanya wawezapo hata wakaamua sasa kuachia hatima kwa Mwenyezi Mungu. Abiria tulianza kutapika na mimi nikiwa mmoja wapo. Kwamuda kadhaa nilipotelewa na kumbukumbu na sikufahamu zaidi. Nilikuja kupata fahamu chombo kilianza kutulia mbele yetu kukiwa na weupe kwa mbali. .

Nilikaa vizuri nipate lujua kinachoendelea. Manahodha walituambia kuwa kwa sasa tunaingia kisiwa cha roc. Kisiwa hiki hakuna wakazi na wanyama pia hakuna au ni wachache. Kuna hadithi ya zamani sana walokuwa wakisimulia mababu kuwa kuna roc aliyekuwa akila mali za watu kama mifugo na kujeruhi wakazi. Hivyo watu wamehama kisiwa hiki. Ni miaka mingi sasa na ni mababu tu wanasimulia hadithi hii. Huenda ni ngano tuu au ni kweli. Hivyo tutaingia hapa kwa ajili ya kupumzika kidogo na kuangalia kama tutapata maji maana safari ni ndefu. Basi tukaingia kisiwani pale na kuanza kuranda randa. Kwakuwa nilitapika sana sikuwa na nguvu za kutosha hivyo nikaelekea kwenye kivuli kikubwa na kujilaza. Nililala sana na nilipokuja kuamka sikuona watu wala jahazi. Kumbe nilisha kimbiwa, niliogopa sana na nisijue nitatokaje pale kisiwani ambapo hakuna watu wala chakula. Nilianza kujuta kwa kukubali kuja. Nilijua sasa hapa kisiwani nitakufa pekeangu kwa kukosa chakula.

Nilianza kukizunguka kisiwa chote kujua nini nitafanya. Jua nalo lilikuwa likizama. Katika kuzunguka nikaona kuna kitu cheupe kwa mbali. Nikaanza kukifata taratibu na nikakuta kama limpira kubwa sana na laiiini. Kuangalia vizuri sikufahamu nini kitu kile. Ghafla nikaona anga inafunikwa na kuna kivuli kikubwa kinaingia nilikimbia kwenda kujificha. Kumbe alikuwa ni ndege roc mkubwa sana yaani mguu wake mmoja ni kama shina la mti. Kumbe lile dude kubwa jeupe ni yai lake.

Basi kiza kilipoingia nilikwenda karibu na ndege yule nikavua kanzu yangu na kufifunga vizuri kwenye miguu ya yule ndege. Niliamini kuwa akiruka atanibeba na kunitoa kwenye kisiwa kile. Basi nilifanya hivyo na kuendelea na imani yangu hiyo. Mambo yakawa kama nilivyotaka asubhi ndege yule aliruka na kunibeba, kwa kuwa sikuwa mzito sana hakujua kama amebeba kitu lamda alijua ni guo tu.


                   

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Aliflela1 Main: Post File: Download PDF Views: 1869

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 Kitau cha Fiqh     ๐Ÿ‘‰2 Dua za Mitume na Manabii     ๐Ÿ‘‰3 web hosting     ๐Ÿ‘‰4 Simulizi za Hadithi Audio     ๐Ÿ‘‰5 Tafasiri ya Riyadh Swalihina     ๐Ÿ‘‰6 ai web app    

Post zinazofanana:

Hadithi ya chongo wa kwanza mtoto wa mfalme

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...
SAFARI YA SITA YA SINBAD

Download kitabu Hiki Bofya hapa SAFARI YA SITA YA SINBAD.

Soma Zaidi...
HADITHI YA WAZIRI ALIYE ADHIBIWA

Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA WAZIRI ALIYEADHIBIWA.

Soma Zaidi...
HADITHI YA KINYOZI MSIRI WA MFALME

Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA KINYOZI MSIRI WA MFALME.

Soma Zaidi...
Wanyama ambao hutolewa zaka

(ii) Wanyama wafugwao kwa ajili ya chakula Wanyama wafugwao wanaotolewa Zakat ni ngamia, ngoโ€™ombe, mbuzi na kondoo.

Soma Zaidi...