VIRUSI VYA KORONA au CORONA (CORONAVIRUS)

virusi vya corona
Virusi vya korona ni katika aina za virusi ambavyo asili yake ni kutoka kwa wanyama na kuja kwa binadamu. Virusi hivi vipo katika aina nyingi. Na vimeshatambulika toka zamani. Na sasa aina nyingine ya virusi hivi vya corona vimejulikana na mpaka sasa vimesababisha maafa na mamia ya watu wameathirika.


<

NI NINI VIRUS VYA CORONA?
Corona ni neno la kilatini lenye maana ya taji (crown). Na hii ni kutokana na kuwa virusi hivi vina umbo hili na taji (crown) ambayo kwa kilatini ndio corona. Virusi hivi husababisha matatizo katika mfumo wa upumuaji. Virusi hivi vinaweza kusababisha maradhi kama SARS yaliyogundulika kwa mara ya kwanza China mwaka 2003 na kuuwa zaidi ya watu 800, maradhi ya MERS yaliyogunduliwa saud arabia mwaka 2012 na kusababisha vifo vya zaidi ya watu 850 na 2400 kuathirika.


<

NINI ASILI NA CHANZO CHA VIRUS HIVI?
Asili ya virusi hivi ni kutoka kwa wanyama kuja kwa watu. Yaani virusi hivi vinapatikana kwenye wanyama kama ngamia, popo, samaki, ngombe na wengineo. Kisha virusi hivi husambaa kutoka kwa wanyama kwenda kwa watu. Baada ya hapo kutoka kwa mtu kwend kwa mtu kwa njia ya hewa ama kugusana. Tafiti zilizofanyika nchini china ambapo ndipo chimbuko la ugonjwa wa virusi vya corona unaotambulika kama 2019-nCoV inathibitishwa kuwa asili ya virusi vya kurona vilivyosababisha ugonjwa wa 2019-nCoV kuwa virusi vimeanzia kwenye vyakula vya baharini, yaani samaki.


<

NI YAPI MARADHI YANAYOSABABISHWA NA VIRUSI VYA CORONA
Mpaka sasa kuna maradhi matatu yananayojulikana kuwa yamesababishwa na virusi vya corona. Na maradhi haya yote huathiri mfumo wa upumuaji na kusababisha mgonjwa kuumwa na homa, kukohoa pamoja na kushindwa kupumua vizuri. Maradhi hayo ni kama:-
A. SARS uligundulika China mwaka 2003 na kuuwa watu 800
B. MERS uligundukika Saud Arabia na kuuwa watu 850
C. 2019-nCoV mpaka kufikia 3/2/2020 umeua watu 361


<

AINA YA VIRUSI VYA CORONA VINAVYOSABABISHA UGONJWA WA MERS
MERS ni neno linalimaanisha Middle East Respiratory Syndrome Coronavirus (MERS-CoV) kwa mara ya kwanza virusi hivi vimegunduliwa mwaka 2012 katika nchi ya Saud Arabia na vilisababisha madhara kwenye nchi zaidi ya 25 ikiwemo Marekani. Miongoni mwa dalili za virusi hivi ni homa kali, kukohoa pamoja na kushindwa kupumua.


<

AINA YA VIRUSI CORONA VINAVYOSABABISHA UGONJWA WA SARS
SARS ni ufupisho wa maneno Severe acute respiratory syndrome (SARS-CoV) huu ni ugonjwa katika mfumo wa upumuaji unaosababishwa na virusi vya corona. Kwa mara ya kwanza virusi vya corona wanaosababisha ugonjwa huu waligundulikwa mwaka 2003. baada ya hapo ugonjwa ulisambaa katika nchi za marekani, ulaya na bara la asia.


<

VIRUSI VYA CORONA VINAVYOSABABISHA UGONJWA WA 2019-nCoV
2019-nCoV ni ufupisho wa maneno 2019 Novel Coronavirus huu pia ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vya corona unaoathiri mfumo wa upumuaji. Ugonjwa huu umeibuka china na kusababisha maafa na kuathiri watu wengi. Ugonjwa huu una dalili kama homa, kukohoa na kushindwa kupumua. Unaambukizwa kwa njia ya hewa na kugusana. Ugonjwa huu hutokea siku mbili mpaka 14 toka kuvipata virusi hivi.


<

UGONJWA WA VIRUSI VYA CORONA UJULIKANAO KAMA 2019-nCoV
Kina mengi bado hayajulikani kuhusu ugonjwa huu na bado wataalamu wa afya wanazidi kuuchunguza ugonjwa huu. Ugonjwa huu husambazwa zaidi kwa njia ya hewa pindi mgonjwa anapopiga chafya ama kukohoa. Unaweza kupata virusi hivi kwa umbali wa futi sita toka kwa mgonjwa. Pia unaweza kuupata kwa njia ya kugusana.


<

Kwa sasa hakuna chanjo ya kuzuia ugonjwa huu. Njia salama kwa sasa ya kujikinga na ugonjwa huu ni kuwa mbali na muathirika wa ugonjwa huu. Pia zipo njia ambazo zimeelekezwa, njia hizi husaidia kujikinga na maradhi yanayoambukizwa kwa kugusana kama haya ya corona. Njia hizo ni kama:-
A. Osha mikono yako kwa sabuni baada ya kutoka chooni, baada ya kupinga kua yako, kabla ya kula, baada ya kupiga chafya au baada ya kukohoa. Uoshe kwa maji ya kuchirizika angalau kwa muda wa sekunde 20.
B.Kama maji yatakosekana kuna dawa za kuoshea zenye alcohol, ni njema kutumia endapo utakosa maji na sabuni
C.Jiepushe kugusa macho, pua na mdomo kwa mkono mchafu
D.Ukiwa mgonjwa bakia nyumbani
E.Unapokwenda kwenye maeneo hatarishi ziba mdomo na pua yako kwa mask ama na unapopiga chafya ama kukohoa jizibe kwa kitambaa ama nguo na si kwa mkono.


<

Pia kwa sasa hakuna matibabu maalumu ya virusi hivi. Waathirika wanapewa tiba mbadala za kupunguza athari hizo za ugonjwa. Pia kwa wagonjwa waathirika zaidi tiba maalumu ya kulinda viungo vya ndani hutolewa.


<

ATHARI ZA UGONJWA WA 2019-nCoV
Mpaka kufikia jumatatu ya tarehe 3 mwezi wa pili mwaka 2020 yapata watu 361 wamefariki kwa ugonjwa huu na kuacha waathirika maeflu. Hii inaonesha asilimia 2 tu ya waathirika ndio wamefariki. Hii ni tofauti na ugonjwa wa MERS ambao karibia robo ya waathirika walifariki. Na mpaka kufikia tarehe hiyo tajwa hapo juu 3/2/2020 watu wapatao 2,110 wapo katika hali mbaya.