HATUA ZA KUJIKINGA NA VIDONDA VYA TUMBO
Unaweza kupunguza hatari yako ya vidonda vya tumbo ikiwa unafuata mikakati sawa inayopendekezwa kama tiba ya nyumbani kutibu vidonda. Inaweza pia kusaidia:
Jilinde dhidi ya maambukizo. Haijulikani wazi jinsi bakteria aina ya H. pylori inavyoenea, lakini kuna ushahidi fulani kwamba inaweza kupitishwa kutoka kwa mtu hadi mtu au kupitia chakula na maji.
Unaweza kuchukua hatua za kujikinga na maambukizo, kama vile H. pylori, kwa kuosha mikono yako mara kwa mara kwa sabuni na maji na kwa kula vyakula ambavyo vimepikwa kabisa.
Chukua tahadhari dhidi ya dawa za kupunguza maumivu. Ikiwa unatumia kila wakati dawa za kupunguza maumivu ambazo zinaongeza hatari ya vidonda vya tumbo, chukua hatua za kupunguza hatari hiyo. Kwa mfano, kunywa dawa yako pamoja na chakula.
Zungumza na daktari kupata dawa ambayo itakupa utulivu wa maumivu bila ya kusababisha hatari zaidi.
Epuka au punguza kunywa pombe wakati unatumia dawa. Kama tulivyoona unywaji wa pombe unaweza kuhatarisha zaidi vidonda vya tumbo kwa kuchochea uzalishwaji wa asidi tumboni.
Ikiwa unahitaji dawa za kutuli za maumivu na zile za NSAID, unaweza kuhitaji pia kuchukua dawa za ziada kama vile antacid, PPI, blocker acid au cytoprotective agents. Kikundi cha NSAIDs kinachoitwa COX-2 inhibitors kinaweza kuwa na nafasi ndogo ya kusababisha vidonda vya tumbo, lakini vinaweza kuongeza hatari ya mshtuko wa moyo.