Muendelezo.....
TAHARUKI YA MFALME
Basi mfalme na waziri wake wakaenda mpaka kwenye bostani. Loo walikuta na geti lipo wazi. Waakingia bila hata ya tatizo. Walishangaa sana kukuta kuna watu watatu wakiwa katika furaha kubwa sana wakiimba na kunywa. Mfalme na waziri wake wakanyata ili wasionekane na mtu wasijewakavuruga burudani ya watu hawa. Basi wakanyata kwa kufuata miti ya matunda. Mfalme akapanda juu ya mti kuchunguli kupitia kwenye dirisha.
Loo alishangaa sana kumuona mzee ibrahimu akiwa amelewa. Hakika hajapatapo kumuona mzee Ibrahimu akiwa katika hali hii kwa miaka 13 sasa. Basi baada ya kushangaa kwa uda akashuka ili apate kutafakari. Akamwambia waziri wake Jafari panda na wewe ujionee maajabu ya watu hawa. Jaafari alipopanda alishangaa zaidi. Wakaanza kushauriana nini wafanye, ili wapate kujuwa hasa ni kitu gani kimewatokea watu hawa na mzee Ibrahim. Wakaamuwa wakabadili mavazi yao waingie kama watu wasiojulikana ili wapate kufahamu ukweli wamambo.
Wakati wanatafuta cha kufanya, mfalme akamuona kijana mmoja mvuvi aliyejulikana kwa jina la Karim. Mfalme akamwambia waziri amsubiri palepale asiondoke mpaka arudi. Waziri hakufahamu wapi mfalme anakwenda hata hivyo pia hakumuoona yile mvuvi. Karim hana ajualo alipofika karibu na geti akalikuta lipo wazi. Akaingia mule ndani kwa siri ili kavue samaki kwenye kajibwawa ka mfalme kwa siri wakati ule wa usiku.
Alipofika kwenye kibwawa akatupa nyavu yake kisha akaanza kusubiri inase samaki wengi. Kumbe mfalme alikuwa nyuma yake. Alipohakikisha samaki ni wengi akatoa nyavu yake. Loo kugeuka nyuma anamuona mfalme. Alijitupa chini ya muguu kuomba msamaha. Mfalme akamsamehe kisha wakabadilishana mavazi. Mfalme akachukuwa samaki wawili na kumuachia akarimu aondoke na samaki wake. Mflme akiwa katika mavazi ya Karim alirudi akiwa na samaki wake mpaka alipo Waziri wake. Akamsalimia, kwa hakika waziri alijuwa anaongea na Karimu. Loo kumbe alikuwa ni mfalme. Hapo mfalme akasema “kama wewe ambaye hujalewa umeshindwa kunijuwa vipi Ibrahim ambaye amelewa atanijuwa.
Basi mfalme akamwambia tena waziri wake amsubiri palepale asiondoke. Sasa mfalme akijifanya ni mvuvi akagonga hodo kwenye lile geti kwa sauti ya juu akijifananisha na Karim. Mzee Ibrahim akauliza nani wewe. Akajibu mfalme ni mimi karim, nimekuletea samaki. Sasa mzee ibrahi anafahamiana na Karim na huwa wanauziana samaki. Kijana Nurdin aliposikia samaki uchu ukamtoka. Akamlazimisha mzee aagize samaki aletewe. Wakaltwa samaki ila yule mrembo alipowaona ni wazima kwenye ndoo ya maji akaomba akaangiwe kwanza.
Mzee Ibrahimu bila ya kuelewa akamuagiza mvuvi akawakaange kisha aje nao. Mfalme akatoka hadi alipo waziri wake. Kisha akamueleza kuwa ameambiwa awakaange. Waziri akataka kulifanya yeye jukumu lake, ila mfalme akakataa alitaka kutimiza amri kama mvuri. Hivyo akaagiza aletewe kila kitu kinachohusika katika kukaanga mpaka chumvi. Alipoletewa aliwakaanga vyema sana kwa umakini mkubwa kisha akawapelekea kwa Mzee Ibrahim. Nurdini alifurahi sana na akampatia mvuvi kiasi kikubwa cha dhahabu ambapo ni mara 100 ya malipo halisi ya samaki wale.
Mfalme akiwa katika umbo la mvuvi alishukuru sana. Yule mtumwa (mke wa Nurdini) alifurahi zaidi na akaanza kuimba tena na kupiga gitaa. Mfalme alifurahi sana na kuonyesha furaha yake dhahiri. Bila ya kujuwa hili wala lile Nurdini akamwambia “mvuvi wewe ni mkarimu sana, umeleta samaki na ukawakaanga, ilaonyesha umependezwa sana na mtumwa wangu huyu. Kuanzia sasa nakupatia iwe kama zawadi yako. An-neese aliposikia maneno hayo alilalamika sana kwa kutumia mashairi, alionyesha dhahiri kuwa hakupenda uamuzi ule, hakupenda kutengena na Nurdini wake. Mfalme ilibidi aulize hasa nini kimetokea kati yao ama ana deni?
Kufikia hapo Nurdini akaanza kuhadithi kila ambacho kilichotokea. Kutoka baba yake akiwa karibu na Mfalme mpaka kununuliwa mtuwa. Kifo cha baba yake hata kukimbiwa na marafiki. Mwisho mpaka anakuja Baghadad na kukutana na mzee Ibrahimu. Mfalme akiwa anasikiliza maneno haya alikuwa akivijwa na machozi. Hakika yalukuwa ni maeneno yenye kutia huruma na simanzi.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Mankaa Tarehe 2024-09-10 15:02:55 Topic: Simulizi za Hadithi Main: Masomo File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 65
Sponsored links
👉1 Kitau cha Fiqh
👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉3 kitabu cha Simulizi
👉4 Madrasa kiganjani
👉5 Kitabu cha Afya
👉6 Simulizi za Hadithi Audio
Simulizi za Hadithi EP 9 Part : Barua ya mfalme wa baghadad
Muendelezo..... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 9 Part : Hatma ya Nurdini
Muendelezo.... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 4 Part 11: Kisa cha Kalid na Jalid
Tuendelee kusikiliza na kusoma visa, hadithi, na simulizi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza tuwe pamoja mpka mwisho...... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 7 Part 14: Jaribio la pili kwa Aladini
Muendelezo.... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 6 Part 6: Hadithi ya Ndoa ya siri
Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha pili muendelezo.... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 1 Part 2: Simulizi ya kisa cha mfugaji na mkewe
Simulizii hii ni inatoka katika kitabu cha kwanza cha HALIF LELA U LELA Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 4 Part 17: Hadithi ya Malipo ya wema ni wema
Mwendelezo wa hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza..... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 3 Part 4: Kisa cha waziri aliyeadhibiwa
Simulizii hii inapatikana katika kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 6 Part24 : Kaka wa tatu wa kinyozi
Muendelezo Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 6 Part 15: Baba tajiri na kifo chake
Muendelezo....... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 10 Part 2: Ni ndoto ama kweli???
Muendelezo..... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 4 Part 4: Simulizi ya chongo wa kwanza mtoto wa Mfalme
Tusikilizie simulizii inahusu chongo wa kwanza wa mtoto wa mfalme iliyopo ndani ya kitabu cha kwanza cha Hadithi za HALIF LELA U LELA..... Soma Zaidi...