Simulizii hii inapatikana katika kitabu cha pili cha hadithi za HALIF LELA U LELA....
MTIHANI PENZINI
Sikuwa na wasiwasi maana niliamini kuwa nitafanikiwa tu. Siku ile nilioga na kuvaa ngua safi na kuvaa viatu vikubwa vya kuchomeka. Nikatoka kuelekea tulipoahidiana. Nilipofika pale nikakutana na kundi la vijakazi wa kike. Mmoja wao akaniuliza ndiye wewe mgeni, wasiri? Nikamjibu ndio. Hapo wakaniambia niingie kwenye moja ya boksi la mbao kisha likafungwa vyema. Niliweza kujihisi kama nipo kwenye jeneza vile. Wakafunganya na mizigo yao mingine na tukaondoak zetu.
Walipofika getini kwnyw jumba la mfalme mabawabu (walinzi wa geti) wakataka kuchunguza kilichomo. Wale wajakazi wakasema kuwa wamebeba nguo za mke wa mfalme. Walinzi wakawaruhusu kupita. Walipofika geti la pili, wakaulizwa tena wakazungumza vilevile. Waliporuhusiwa kupita ghafla mfalme akatokea. Akasema nataka nichunguze mwenyewe vitu vinavyokwenda kwa mkewangu. Hapo nikajua sasa ndio mwisho wangu. Hapo nikaanza kuhisi mkojo unauma. Tumbo likanza kunguruma na woga ukanijaa. Nikaanza kushahadia naa kutubu madhambi yangu.
Mfalme akawaambia watue mizigo, na wafungue boksi mojamoja. Kwa mkono wake mfalme akaanza kufungua kila boksi na anapojiridhisha hufunga. Ndipo akafika kwenye boksi ambalo nimo. Alipotaka kufungua mjakazi mmoja akamwambia, “mtukufu, humu kuna nguo za ndani za Malkia, si vyema zikaonekana hadharani, tunakuomba radhi ufunue boksi hili ukiwa peke yako. Basi mfalme alionekana kukubali na hapo nafsi ikatulia kiasi. Mfalme akaagiza maboksi yote yaingizwe ndani.
Boksi ambalo nipo nikachukuliwa na kupelekwa kwengine. Baada ya mwendo wa hatua kadha upatao dakika kama 10 boksi likatuliwa na kufungulia. Hapo nikatoka nje na kupata hewa safi. Mke wa Sultani alipiga makofi kwa kunipongeza nna kuniambia nimefaulu mtihani wa kwanza. Hapo nikapiga magoti kumsalimu na kumshukuru kwa tumaini alilonipa. Aliniangalia kwa muda kama wa dakika 2 hivi na kisha kapiga tena makofi na kusema “umefaulu mtihani wa pili” sikujuwa ni mtihani gani.
Akanielekeza pa kukaa huku nikisubiria chakula. Kikaletwa chakula, na vinywaji. Niliishia kunywa maji na chakula. Nilikula kiasi kidogo. Sikutaka kula saana nikiwa ugenni. Niligundua vinywaji vile vinatofautiana rang na harufu. Kwakuwa sukjuwa kwa undani vinywaji vile nikaamuwa ninywe maji tu. Baada ya chakula akaja tena mke wa sultani. Alikaa mbele yangu na kupiga tena makofi na kusema “umefaulu mtihani wa tatu” na sasa nitakuozesha mdogo wangu, il a harusi hii itakuwa ya siri, usijefanyiwa fitina na waliokataliwa posa zao.
Nikaelekezwa chumba cha kukaa, mke wa Mfalme akaend kuzungumza na mfalme pamoja na watu wa familia yao.wakakubaliana mahari iwe vipande 500 vya dhahabu. Mke wa mfalme alitowa mahari ili kunitolea na harusi ikafanyika. Sitaki kueleza zaidi kuhusu hiyo harusi. Mambo yakawa kama hivyo, muuza mikanda nimekuwa ndugu na Sultani wa Baghadad.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Mankaa Tarehe 2024-09-10 14:07:20 Topic: Simulizi za Hadithi Main: Masomo File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 171
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi
👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉3 Kitau cha Fiqh
👉4 Madrasa kiganjani
👉5 Kitabu cha Afya
👉6 Simulizi za Hadithi Audio
Simulizi za Hadithi EP 6 Part 28: Hadithi ya mshona nguo (fundi cherehani)
Muendelezo...... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 1 Part 1: Simulizi ya kiapo cha Sultan
Simulizi hii inatoka kwenye kitabu cha kwanza cha hadidhi za HALIF LELA U LELA. Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 5 Part 1: Hadithi ya safari saba za Sinbad
Hadithi hii inapatikana katika kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA.... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 5 Part 12: Sehemu ya tano ya safari ya Sinbad
Muendelezo wa hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 6 Part 5: Nani ni binti?
Muendelezo wa hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha pili.... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 6 Part 26: Kaka wa tano wa kinyozi
Muendelezo.... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 9 Part : Nudhini na mtumwa
Muendelezo....... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 5 Part 4: Sehemu ya pili ya safari ya Sinbad
Muendelezo wa hadithi ya safari ya Sinbad iliyopo kwenye kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA..... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 5 Part 16: Hadithi ya safari ya saba ya Sinbad
Muendelezo wa safari ya Sinbad....... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 10 Part 3: Asubuhi yenye varangati
Muendelezo.... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 4 Part 13: Simulizi ya nyani kibadilika kuwa chongo
Mwendelezo wa hadithi zetu nzuri na za kusisimua kutoka katika kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA..... Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 7 Part 1: Aladini na taa ya mshumaa wa ajabu
Hii ni simulizi iliyopo ndani ya kitabu cha pili cha hadithi za HALIF LELA U LELA...... Soma Zaidi...