Posti hii inahusu zaidi mambo yanayohitajika kabla ya kuanza upasuaji ni mambo muhimu ambayo yanapaswa kufanyika kwanza na baadaye upasuaji unaweza kuendelea.
Mambo yanayopaswa kufanyika kabla ya kuanza upasuaji.
1.Kwanza kabisa mazingira yanapaswa kuandaliwa.
Kuhakikisha kuwa chumba kimeandaliwa vizuri na kumfanya mgonjwa ajisikie huru, kuhakikisha kubwa hakuna alama yoyote ya kuwepo kwa maambukizi na kuwepo usalama katika chumba hicho na kuhakikisha kwamba kila mgonjwa anakuwa na utofauti na mwingine katika maandalizi hii inategemea na hali ya mgonjwa na Ugonjwa alio nao.
2.Kuandaa vifaa vyote vinavyohitajika wakati wa upasuaji.
Hivi vifaa vinaandaliwa na mhudumu maalumu ambaye amechaguliwa kuandaa vifaa hivyo na kuhakikisha kubwa vifaa vinaandaliwa kadri ya ugonjwa alionao au kadri ya hali ya mgonjwa kwa hiyo kila hospitali inapaswa kuwa na vifaa vya kutosha ambapo akitoka mgonjwa huyu anaingia mwingine na seti za vifaa vinavyotumika ni tofauti tofauti ili kuweza kuepuka Maambukizi.
3. Kumwandaa mgonjwa.
Hii ni hatua ya msingi sana ambapo wahudumu wanapaswa kumwandaa mgonjwa na kumhakikishia kuwa upasuaji utaenda vizuri na kumwambia kwa nini wanafanya upasuaji na kuhakikisha kuwa mgonjwa anasaini fomu maalumu kwa ajili ya kukubali kuwa upasuaji ufanyike na kupima vipimo vyote kama vile mapigo ya moyo, upumuaji, msukumo wa damu na joto la mwili kabla ya kufanyika upasuaji wowote ule.
4.Maandalizi ya wahudumu.
Na wahudumu wenyewe wanapaswa kujiandaa kwa kila mtu na kazi yake kuhakikisha kuwa dawa zinazohitajika zimepatiwa kwa mgonjwa , kuhakikisha kuwa fomu imesainiwa na kuandaa mavazi na kujua historia ya mgonjwa kama upasuaji ni wa kwanza au vipi na kuandaa dawa kwa ajili ya kumpatia dawa kadri ya uchaguzi wa mgonjwa au ushauri wa wahudumu.
Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.
Download NowUmeionaje Makala hii.. ?
Zijue kanuni 100 za afya ambazo watu wengi hawazijui. Laiti wangelizijua kwa hakika wangefaidika sana.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi madhara ambayo tunaweza kuyapata katika matumizi ya toilet paper au tisu kwenye sehemu za siri.
Soma Zaidi...Makala za afya zilizopata kusomwa zaidi kutoka bongoclass kitengo cha afya
Soma Zaidi...Tumekusha kuona na kujua kuwa mbu anaweza kuambukiza maradhi mengi na ya virusi kama zika.
Soma Zaidi...