UWANJA WA TEKNOLOJIA

Sehemu ya nnne

.

2.KUFUNGUWA PROGRAM NYINGI KWA WAKATI MMOJA
Sababu ya pili inayofanya kompyuta yako au simu yako iwe slow yaan haina speed katika kufanya kazi ni kufunguwa program nyingi kwa wakati mmoja.

Hutokea wakati fulani mtumiaji wa kompyuta huwa anafunguwa program nyingi kwa wakatimmoja. Hii hali huweza kuifanya kompyuta yako iwe slow hasa ikiwa RAM na processor ni ndogo.

pia zipo software abazo kikawaida zenyewe ni mzito sana kufanyakazi katika kompyuta iliyo na RAM ndogo kwa mfano bluestacks appl player hii software yenyewe inahitaji kompyuta yenye uwezo mkubwa hivyo ukiifunguwa na software zingine kuna uwezo mkubwa kompyuta yako kuwa slow.

kulitatuwa tatizo
1.Funga program zote ambazo hauzitumii wakati huu. Unaweza kuzifunga kwa kuenda kwenye setting kisha task maneger, hapa utakuta orodha ya App ambazo zinafanya kazi. Chagua moja moja kisha uifunde (ende process).

2.Zuia background activities kwa program ambazo zinaran background. Ukienda setting kisha App maneger utakuta orodha ya App ambazo zinafanya kazi muda wowote. Chagua na uzifunge.

3.Hakikisha unapofungua program nzito kama bluestack au android studio na zinazofanana na hizi, usifungue pamoja na program zingine nzito kwa muda huohuo. Tahadhari hii ni muhimu kwa wale wanaotumia kompyuta zenye RAM ndogo.

5.Kwa wale wanaotumia simu pia hakikisha simu yako ina uwezo mkubwa kama unataka kufungua App nzito kama games. Pia hakikisha memori ya simu yako haijajaa mpaka mwisho na hakikisha simu yako ina nafasi ya kutosha kwenye RAM.         › WhatsApp ‹ Whatsapp