Sababu Ya Uislamu Kuwa Ndiyo Dini Sahihi Pekee

1.

Sababu Ya Uislamu Kuwa Ndiyo Dini Sahihi Pekee

1.3. Sababu Ya Uislamu Kuwa Ndiyo Dini Sahihi Pekee.
Uislamu ndio dini pekee inayostahiki kuchaguliwa na kufuatwa kama muongozo sahihi wa maisha na watu wote kwa sababu zifuatazo;



(a)Uislamu unaeleza ukweli juu ya maumbile na nafasi ya mwanaadamu hapa Duniani;
Uislamu unaeleza lengo la kuumbwa mwanaadamu kuwa ni ibada na kumtumikia Mwenyezi Mungu na kuwa msimamizi wa sheria na hukumu zake hapa ulimwenguni ili kupata radhi zake.
Rejea Qur'an (51:56) na (2:29).



(b)Sheria na kanuni za Uislamu zinaendana na kanuni za kimaumbile;
Uislamu ndiyo dini pekee inaenda na kuzingatia kanuni na taratibu zote za kimaumbile za kibailojia kifizikia na kikemia ya viumbe vyote vilivyo na visivyo hai ikiwa ni pamoja na maumbile au mazingira yanayotuzunguka.
Rejea Qur'an (3:83) na (30:30).



(c)Uislamu ndio dini inayotosheleza matashi yote ya mwanaadamu kimwili na kiroho;
Uislamu ni dini inayotoa muongozo namna ya mtu kumiliki hisia zake na kuendea mambo katika hali tofauti tofauti kama vile wakati wa furaha, shida, huzuni, misiba, n.k.
Rejea Qur'an (2:155-157).



(d)Uislamu ni njia kamili ya maisha;
Ni Uislamu pekee ndio mfumo kamili wa maisha ya kila siku ya mwanaadamu katika fani na nyanja zote za kibinafsi na kijamii kama vile kisiasa, kiuchumi na kiutamaduni.



(e)Uislamu una ibada maalum za kumjenga mwanaadamu kimaadili;
Uislamu umeweka muongozo katika kumuadilisha mwanaadamu kupitia ibada maalum kama vile swala, funga, hija, kutoa zakat na sadaqat na zinginezo za sunnah.

(f)Uislamu ni dini ya walimwengu wote na wa nyakati zote;
Uislamu umekuwa ni mwongozo wa maisha tangu binaadamu wa kwanza hadi wa mwisho katika Nyanja zote za maisha bila kujali taifa, ukoo, rangi na hadhi ya watu.
Rejea Qur'an (42:13).



(g)Uislamu ni dini ya kusimamia haki, uadilifu na usawa;
Ni dini ya Uislamu ndiyo inayotoa na kusimamia kwa usawa na uadilifu haki, hukumu na adhabu zote kwa watu wote bila ya upendeleo na ubaguzi wa rangi, taifa, hadhi na ukoo.
Rejea Qur'an (103:1-3), (9:33), (61:9) na (17:105).



                   

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 208

Post zifazofanana:-

NENO LA AWALI
Darasa la elimu inayohusu ujauzito na namna ya kulea mimba Soma Zaidi...

JITIBU KWA KITUNGUU THAUMU: faida za kiafya za kitunguu thaumu
Kitunguu thaumu ni katika viungo vya mboga na chakula. Soma Zaidi...

HADITHI ZA ALIF LELA U LELA: HADITHI YA MVUVI NA JINI
Soma Zaidi...

Ni zipi Nguzo za Udhu au Kutawadha
Soma Zaidi...

NGUZO ZA IMAN
Jifunze tawhid yaani kumpwekesha Allah subhaanah wata'aala Soma Zaidi...

ADABU ZA KUSOMA QURAN
Adabu wakati wa kusoma quran 1. Soma Zaidi...

darasa la lishe
Jifunze mengi kuhusu afya na lishe, ujuwe utaratibu wa lishe Soma Zaidi...

MAJIMAJI YA KWENYE UKE YANATUELEZA NINI?
Soma Zaidi...

English vocabulary test 01
Soma Zaidi...

Zijuwe hatuwa za ukuwaji wa ujauzito na dalili za ujauzito katika miezi mitatu, miezi sita na miezi tisa
Soma Zaidi...

chimbuko la sheria katika uislamu, hukumu za sheria na kuyatambua yaliyo halali na haramu
Soma Zaidi...

SYMPTOMS OF CANCER
Cancer occurs when body's cells grow without being controlled'in'the body. Soma Zaidi...