image

Madai ya Makafiri dhidi ya kuwepo kwa Allah (s.w) na Udhaifu wa Madai hayo.

2.

Madai ya Makafiri dhidi ya kuwepo kwa Allah (s.w) na Udhaifu wa Madai hayo.

2.1.Kumuamini Mwenyezi Mungu (S.W).

?Madai ya Makafiri dhidi ya kuwepo kwa Allah (s.w) na Udhaifu wa Madai hayo.
Makafiri wa zamani na wa zama hizi wakiwemo Charles Darwin, Friedrich Engles, n.k wanadai kuwa imani ya uwepo wa Mungu Muumba dhana tu haina dalili yeyote. Miongoni mwa hoja (madai) zao wanazotoa ni hizi zifuatazo;(a)Mwenyezi Mungu hayupo kwa sababu haonekani na wala hadirikiki kwenye milango ya fahamu. Rejea Qurโ€™an (17:90-92).
Milango ya fahamu kama vile macho katika kumuona, pua katika kumnusa, masikio katika kumsikia, ngozi katika kumhisi au kumgusa pia, n.k.

Udhaifu wa hoja hii,
Milango ya fahamu ina udhaifu mwingi sana na kikomo pia, kama vile macho au pua huweza kuona au kunusa vitu vilivyo karibu tu na visivyokuwa na kizuizi, kuna vitu vingi vinavyotuzunguka lakini hatuvioni kama upepo, sauti, n.k.(b)Mwenyezi Mungu amefanywa kuwepo na wanadamu kutokana fikra na mawazo duni na uduni wa maendeleo ya sayansi na teknolojia.
Hii ni baada ya mwanaadamu kushindwa kutatua matatizo katika mazingira yake na hivyo kuibukia kujiundia muingu.Udhaifu wa hoja hii,
Historia inaonyesha kuwa hakuna zama mwanaadamu aliishi bila ya ujuzi wa kukabiliana na mazingira yake, Mwanaadamu wa kwanza kuumbwa alipewa ujuzi (elimu) ya kukabilana na mazingira yake na hatimaye kushushiwa muongozo kamili wa maisha kutoka kwa Muumba wake.
Rejea Qurโ€™an (2:31,38).
(c)Hapana Mungu Muumba bali vitu vyote vimetokana na mabadiliko ya kimaada.
Wanadai kuwa maumbile na viumbe vyote vinatokana na mabadiliko kidogo kidogo ya kimaada (evolution) baada ya muda mrefu kupita kutoka hali moja kwenda nyingine. Mfano binaadamu kutoka pweza, mjusi, sokwe na hatimaye mtu kamili.Udhaifu wa hoja hii,
Nadharia hii haina ushahidi wowote wa kisayansi, kiuchunguzi na utafti bali ni dhana tu aliyoibuni Darwin ili kupotosha uhalisia na ukweli juu ya chanzo cha maumbile. Hadi leo hii hakuna mwanasayansi yeyote anayeweza kuthibitisha nadharia hii.(d)Kama Mungu Muumba yupo, ni ipi nasaba (ukoo) yake au ametokana na nini?
Makafiri wa zamani na sasa wanasingizia kutoamini kuwepo Mungu kwa kuwa hawajui nasaba, ukoo au asili yake anatokana na nani au na nini.

Udhaifu wa

hoja hii,
Kwa kutumia mantiki, Muumba wa vitu vyote ndiye chanzo na asili ya vitu vyote. Hivyo ni lazima asiwe na nasaba, mwanzo au mwisho pia. Na asitokane na vitu au maumbile yale.
Rejea Qurโ€™an (112:1-4).(e)Vitu havikuumbwa bali vimetokea kwa bahati nasibu (by chance) na vitatoweka kwa bahati nasibu pia muda wake ukifika.
Makafiri wa zamani na sasa wanadai kuwa asili ya maumbile yote yametokana na bahati nasibu (by chance), hivyo vitatoweka kama vilivyoibuka.Udhaifu wa dai hili,
Hakuna uwezekano wa kuwepo maumbile bila ya Muumbaji na msimamizi mwenye ujuzi na uwezo wa hali ya juu na mtegemewa wa kila kitu, kwani kila kitu kinachoonekana kimeumbwa na kimewekwa kwa lengo maalum.                              

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 631


Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 Madrasa kiganjani     ๐Ÿ‘‰2 Kitabu cha Afya     ๐Ÿ‘‰3 kitabu cha Simulizi     ๐Ÿ‘‰4 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-