image

Umuhimu wa kusimamisha uislamu katika jamii

1.

Umuhimu wa kusimamisha uislamu katika jamii

1.4.Maana ya Kusimamisha Uislamu katika jamii.
Ni pale ambapo waislamu katika jamii wataweza kuendesha kila kipengele cha maisha yao ya binafsi na jamii katika siasa, uchumi, utamaduni, n.k kwa kufuata kikamilifu muongozo wa Qur’an na Sunnah.
Rejea Qur’an (3:83), (10:99), (32:13), (61:8) na (64:2).
n b 1.5.Umuhimu wa Jihad katika kusimamisha Uislamu katika jamii.

i.Kusimamisha Uislamu (Jihad) katika jamii ni amri (faradh).
Kama ilivyoamrishwa swala, funga, zakat na hijja, Neno “kutiba” (mmelazimishwa) limetumika katika jihad kama lilivyotumika katika kufunga, kulipa kisasi na faradh zingine pia za kutekeleza Uislamu.
Rejea Qur’an (2:216), (2:183), (2:178,180) na (22:78).ii.Msamaha na Pepo hupatikana kwa kufanya juhudi (jihad) za maksudi katika kusimamisha Uislamu katika jamii.
Kutekeleza faradh kama swala, funga, zaka na hija na ibada zingine za sunnah za binfsi, itakuwa sio sababu ya msingi ya kupata msamaha na pepo ya Mungu, mpaka jitihada ya dhati katika kupigania Uislamu katika jamii ifanyike.
Rejea Qur’an (4:74), (9:111), (61:10-13), (2:154), (3:169-171), (3:142), (3:157), (2:214) na (9:16).iii.Mwenyezi Mungu (s.w) ameteremsha chuma (silaha) kuwa nyenzo ya kusimamisha Uislamu katika jamii.
Mitume wametumwa kusimamia haki na uadilifu katika jamii kwa kutumia miongozo ya vitabu vya Allah (s.w) na pia chuma (silaha) kimeteremshwa ili mitume na waumini wakitumie katika kusimamia haki na uadilifu ndani ya jamii.
Rejea Qur’an (57:25).
iv.Kusimamisha Uislamu katika jamii ndio lengo kuu la maisha ya Waumini.
Mwenyezi Mungu (s.w) ametubainishia kuwa chochote tutakachokipenda au tutakachokifanya nje na lengo la kusimamisha Uislamu katika jamii hatakuwa na radhi juu yetu. Rejea Qur’an (9:23-24).1.6. Kwa nini ni muhimu Kusimamisha Uislamu katika jamii?
Ni muhimu Uislamu kusimama katika jamii ili matunda yafuatayo yapatikane;
i.Waumini wataweza kumuabudu Mwenyezi Mungu (s.w) ipasavyo kwa mujibu wa Qur’an na Sunnah kwa kila kipengele cha maisha ya kila siku binafsi na jamii katika siasa, uchumi, elimu, utamaduni kama wanavyotekeleza swala, funga, hija, n.k.
Rejea Qur’an (51:56), (2:21-22), (7:54), (9:31), (2:85), (2:208), (2:193), (4:75-76), (9:38), (8:39), (22:40) na (47:7).ii.Kupatikana amani ya kweli na kuondoka hofu na mashaka katika jamii. Hii ni baada ya waumini kuchukua hatamu ya uongozi katika jamii kwa mujibu wa muongozo na sheria za Mwenyezi Mungu (s.w).
Rejea Qur’an (57:25), (2:257) na (5:90-91).iii.Waumini wataweza kuamrisha mema na kukataza maovu kikamilifu katika jamii pasina kikwazo chochote pindi watakapochukua nafasi ya kuiongoza jamii.
Rejea Qur’an (22:41) na (3:110).iv.Kuikinga jamii na majanga mbali mbali. Waumini watakapochukua nafasi za kuiongoza jamii ndio itakuwa sababu ya kutoweka maovu ndani jamii ambayo ndio sababu ya kupatikana majanga katika jamii.
Rejea Qur’an (8:25).                              

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01 Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 454


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitau cha Fiqh     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Madrasa kiganjani    

Post zifazofanana:-