Kuingia Kwa Uislamu Tanzania na Afrika Mashariki
Namna Uislamu ulivyoingia Tanzania na Afrika Mashariki
- Kupitia misafara ya Wafanyabiashara tangu karne ya 8 A.D kutoka Bara Arab, India, Asia na Ghuba kuja Pwani ya Afrika Mashariki.
- Kufikia karne ya 9 A.D, wahamiaji wengi toka Bara Arab, India na Asia wengi wao wakiwa waislamu, walifanya makazi Pwani ya Somalia na kuufundisha Uislamu kwa wenyeji.
- Kuna alama na ishara za kale za kuonesha kuwepo Uislamu katika Pwani ya Afrika Mashariki zikiwemo magofu ya;
1. Msikiti wa Kaole β Bagamoyo
2. Msikiti wa Kizimkazi β Dimbani Mkoa wa Kusini Unguja, uliojengwa mwaka 500 A.H (1107 A.D)
3. Misikiti ya Kilwa Kisiwani n.k.
- Ibn Batuta alipotembelea Afrika Mashariki mnamo mwaka 1332 A.D, tayari miji mingi ya Pwani hasa Kilwa ilikuwa na Waislamu wengi zaidi.
- Kutokana na mchanganyiko wa Waarab na wenyeji wa Pwani, kulizuka lugha ya Kiswahili na Kibantu na kuzidi kuenea.
- Miji ya Unguja, Tanga, Dar es Salaam, Mombasa, Lamu, Malindi na Mikindani ilikuwa ndio vituo vikuu vya kueneza Uislamu miji ya bara ya Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Zaire, Msumbiji, Malawi na Burundi.
- Misafara ya Wafanyabiashara kutoka miji ya Pwani walipofanya makao ya biashara walijenga misikiti kama kituo cha elimu ya Dini ya Kiislamu.
- Hivyo, kutokana fursa ya mchanganyiko huo, waislamu wengi wakawa wafanyabiashara na wamiliki wa kubwa wa maduka, magari, n.k.
Hali ya Uislamu uliofundishwa enzi za Ukoloni
- Historia inaonesha kuwa Uislamu Afrika Mashariki haukuenezwa kwa lengo la kutawala maisha ya jamii, bali ilikuwa ni kitu cha ziada na cha mtu binafsi na lengo kuu likiwa ni biashara.
- Mambo mengi ya msingi katika kuusimamisha Uislamu katika nyanja za uchumi, siasa, jamii hayakupewa umuhimu zaidi ya fiqh ya kufunga, kuswali na sitara kuwa na nafasi kubwa zaidi.
- Mambo mengi yaliyozuliwa kama matanga, dhikiri za kitwariqa, maulidi, khitima, n.k. ndio yalipewa umuhimu na nafasi kubwa.
- Qurβan ilifundishwa sio kwa lengo la kuwa mwongozo wa maisha kibinafsi na kijamii bali kupata thawabu na baraka, kufukuzishia majini na mashetani, kuimbishwa bila kujua maana ya ujumbe wake, n.k
Nafasi ya Uislamu Tanganyika na Afrika Mashariki wakati wa Ukoloni
- Pamoja na kuwa waarabu wengi walikuja na Uislamu Tanganyika, athari ya uvaaji sitara na mila zingine ziliwaathiri sana wenyeji.
- Waislamu walifanya jitihada za kueneza mafundisho ya Uislamu kwa njia za mihadhara, makongamano, n.k. ambapo wakristo wengi walisilimu.
- Waislamu kupitia taasisi na jumuiya mbali mbali, kama vile EAMWS
walianzisha vituo vya elimu kama vile; madrasa, shule za msingi na sekondari.
- Viongozi wengi wa serikali walikuwa ni waislamu kwa sababu ndiyo watu wa mwanzo kujua kusoma na kuandika kwa herufi na tarakimu za kiarabu.
- Sehemu kubwa ya uchumi ilikuwa chini ya miliki ya waislamu waliokuwa ndio wafanya biashara wakuu.
- Waislamu walianzisha vyama vya siasa kama TAA (Tanganyika African
Association), n.k kama vyombo vya kuongozea serikali.
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Sira Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 2139
Sponsored links
π1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
π2 Madrasa kiganjani
π3 Simulizi za Hadithi Audio
π4 Kitabu cha Afya
π5 Kitau cha Fiqh
π6 kitabu cha Simulizi
Kuzaliwa kwa Musa(a.s) na kukua kwake na maisha ya ujana wake na kupata Elimu
Musa(a. Soma Zaidi...
Sababu ya uislamu kuwa ndiyo dini sahihi pekee
Dini anayostahiki kufuata mwanadamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
MJADALA JUU YA NDOA YA MTUME S.A.W NA BI KHADIJA (HADIJA)
LAKINI UMRI WANGU MKUBWABaada ya kuwaza na kufikiri muda mrefu, bibi Khadija (Radhiya Llahu anha) akafikia uamuzi wa kutaka kuolewa na Muhammad (Swalla Laahu alayhi wa sallam). Soma Zaidi...
Malezi ya mtume
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2 dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
NUHU(A.S) NA WATU WAKE NA UOVU WALIOKUWA WAKIUFANYA WATU WAKE
Mtume aliyemfuatia Nabii Idrisa(a. Soma Zaidi...
Nabii Yunus(a.s) Amuomba Allah(s.w) Msamaha
Ndani ya tumbo la samaki, Nabii Yunus(a. Soma Zaidi...
HISTORIA YA NABII ISMAIL
Soma Zaidi...
Mtume alipoanza kulingania uislamu na changamoto alizokumbana nazo kutoka kwa maadua wa uislamu
7. Soma Zaidi...
Kuibuka kwa kundi la khawarij baada ya vita vya Siffin
Soma Zaidi...
Imam Nasai na kitabu cha Sunan
Soma Zaidi...
Kuandaliwa kwa Muhammad wakati na baada ya kupewa utume
Bara arabu zama za jahiliyyah (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
tarekh 07
KUPASULIWA KWA KIFUA MTUMEWAKATI AKIWA MTOTO. Soma Zaidi...