Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa
HUKUMU YA NUN SAKINA NA TNWIN
SURA YA TATU
HUKUMU YA NUN SAKINA NA TANWIN
KUKUMU ZA NUWN SAAKINAH NA TANWIYN.
Nuwn saakinah: Ni herufi ya nuwn نْ isiyokuwa na i’raab ambayo huthibiti katika kutamkwa, kuandikwa, kusimama na katika kuunganisha. Tanwiyn: Ni nuwn saakinah iliyozidi inapatikana mwisho wa nomino kwa kutamkwa wakati wa kuunganisha na hutengamana na hiyo nomino wakati wa kuandika na kusimama.(al-hidaayah.com).
Wataalamu wa Tajwid wanaeleza hukumu nne pindi nuwn sakinah na tanwiyn zinapokutana. Hukumu hizo ni:-
1. الإÙظْهاَرْ AL-IDHWHAAR - KUDHIHIRISHA.
Maana yake ni kukibainisha kitu wazi. Katika hukmu za Tajwiyd ni kuitoa kila herufi katika makhraj yake bila ya kuweko na ghunnah. Nayo hutokea pale Nuwn saakinah au tanwiyn inapofuatiwa na mojawapo wa herufi sita za al-halq (koo) ambazo Ø¡ Ù‡ Ø Ø® ع غ
Bofya kitufe cha MFANO 01, MFANO02,kusikiliza mfano
Mifano.
www.al-hidaayah.com
II- الإÙدْغاَم AL-IDGHAAM – KUINGIZA, KUCHANGANYA.
Idghaam ni kuingiza kitu kwenye kitu. Katika hukmu za Tajwiyd ni kuingiza herufi saakin kwenye herufi yenye i’raab na kuzipelekea herufi mbili hizi kuwa herufi moja ya pili nzito. Na hutokea pale nuwn saakinah au tanwiyn inapofuatiwa na moja ya herufi sita za idghambazo ni ÙŠ ر Ù… Ù„ Ù† Ùˆ
Sharti za idgham.
Idgham sikuzote inafanyika kwenye maneno mawili tu. Herufi ya mwisho ya neno la kwanza iwe na atnwiyn au nun sakina na herufi ya kwanza ya neno linalofata iwe ni moja ya herufi za idgham zilizotajwa hapo juu.
Sasa ikitokea nun sakina au tanwiyn zimekutana na moja ya herufi hizi za idgam katika neno moja hapa kinachotakiwa ni kuleta idhhar kwenye nun sakina au tanwiyn. Na hii idhwhaari ndiyo inayoitwa idhwhaar mutlaqa yaani idhwhaar halisi.katika qurani kuna maneno manne tu ambayo kuna idhwhaar tutlaqa.
Aina za idgham.
1.idgham bighunnah
Idghaam bighunnah ni kuingiza nuwn saakinah au tanwiyn kwenye herufi za ÙŠ Ù† Ù… Ùˆ pamoja na kuleta ghunnah inayotokea puani. Na hii hutokea pale nun sakina na tanwiyn zinapokutana na moja ya herufi hizo nne.
2.Idghaamu bighayri ghunnah
Ø©" Ø¥Ùدْغَام٠بÙغَيْر٠غÙÙ† (Idghaamu bighayri ghunnah) ni kuitia na kuichanganya nuwn saakinah au tanwiyn katika herufi za ر Ù„ bila ya kuleta ghunnah inayotokea puani.
Makundi mengine ya idgham.
1.Idghaamu Kaamil
Hii huitwa idgham iliyokamilika ambayo pia inaweza kugawanyika katika makundi mawili ambayo ni;-
idgham kaamil bighunnah.: Hii hutokea pale nun sakina au tanwiyn zinapokutana na Ù† na Ù… . Hapa kutakuwa na idgham pamoja na kutia ghunnah yaani kunung’unisha nun sakina au tanwiyn.
Idghaamu Kaamil Bighayri Ghunnah: hii hutokea pale nun sakina au tanwiyn inapokutana na ر Ù„. Hapa kutakuwa na idgham ila bila ya kunung’unisha nun sakina au tanwiyn.
Mifano ya idgham kaamil
2.idghaamu naaqisw.
Hii hutwa idghamu iliyopunguwa, na hutokea pale nun sakina au tanwiyn inapokutana na Ùˆ ÙŠ. Imeiytwa ni pungufu kwa sababu inakuwepo idgham bila ya kupoteza sifa ya nun sakina au tanwin.
Mifano:
Bofya kitufe cha MFANO 03, kusikiliza mfano
III- الإقْلاَبْ AL-IQLAAB - KUGEUZA.
Maana yake ni kugeuza kitu na kinavyotakiwa kuwa au kupindua kitu. Katika hukmu za Tajwiyd ni kuigeuza nuwn saakinah au tanwiyn kwa kuitamka kama ni م (miym) pamoja na kuleta ghunnah.. (www.alhidaayah.com). Hukumu hii inapatikana pale tu nun sakina au tanwiyn inapokutana na ب (baa) tu. Hivyo herufi ya iqlab ni moja tu.
III- الإÙØ®ÙÙاء AL-IKHFAA - KUFICHA
Katika hukmu za Tajwiyd ni kuificha nuwn saakinah au tanwiyn katika herufi za ikhfaa. Hivyo nuwn saakinah au tanwiyn itatamkwa ikiwa baina ya idhwhaar na idghaam kwa kuipa ghunnah isiyokuwa na shaddah. Hukumu hii inapatikana pale nun sakina au tanwiyn inapokutana na moja ya herufi hizi ث ج د ذ ز س ش ص ض ط ظ ٠ق ك
Bofya kitufe cha MFANO 04,MFANO 05 na MFANO 06, kusikiliza mfano
‹ Nyuma › Endelea ‹ Books ‹ Apps ››
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Quran Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 3168
Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi
👉2 Kitau cha Fiqh
👉3 Simulizi za Hadithi Audio
👉4 Madrasa kiganjani
👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉6 Kitabu cha Afya
Hukumu ya tafkhim na tarqiq katika usomaji wa Quran tajwid
Tarqiq ni kuisoma herufi kwa kuipa wepesi na tqfkhim ni kuisoma herufi kwa kuipa uzito. Soma Zaidi...
Saratul-asr 103
Quran (EDK form 3: dhana ya elimu ya uislamu) Soma Zaidi...
HUKUMU ZA MADD YAANI KUVUTA HERUFI KWENYE USOMAJI WA QURAN
Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa Soma Zaidi...
Nini maana ya Iqlab katika hukumu za tajwid
Hapa utajifunza maana ya iqlab katika usomaji wa Quran kwa tajwid Soma Zaidi...
Maisha ya Mtume Muhammad s.a.w kabla ya utume
Sira na historia ya Mtume Muhammad s.a.w , sehemu ya 19. Hapa utajifunza maisha ya Mtume kabla ya utume. Soma Zaidi...
Mtume hakufundishwa quran na Jabir na Yasir
Soma Zaidi...
HUKUMU ZA MIIM YENYE SAKINA
SURA YA NNE HUKUMU ZA MIYM YENYE SAKNA HUKUMU ZA MIYM SAKINA: Mym sakina ni miym ambayo haina i’rab ( مْ). Soma Zaidi...
Sababu za kushuka kwa surat al-Fiil
SURAT AL-FIILSura hii imeteremshwa Makkah na ina Aya Sita pamoja na Basmallah. Soma Zaidi...
Kukosolewa Mtume (s.a.w) katika Qur-an ni Ushahidi Mwingine kuwa Qur-an ni Kitabu cha Allah (s.w):
(v)Kukosolewa Mtume (s. Soma Zaidi...
Ni zipi hukumu za nuni yenye sakina au tanwin?
Hapa utajifunza usomaji wa Quran pindi utakapokuta nuni yenyebsakina au tanwin Soma Zaidi...
Sababu za Kushuka Surat Al-Masad (tabat yadaa) na fadhila zake
4. Soma Zaidi...
Asbab nuzul surat at Tin, Sababu za kushuka surat at Tin (watin wazaitun)
Post hii itakwenda kukufundisha sababu za kushuka kwa surat at Tin (watin wazaitun). Soma Zaidi...