HUKUMU ZA MIYM YENYE SAKNA : Mym sakina ni miym ambayo haina i’rab ( مْ).
HUKUMU ZA MIYM YENYE SAKNA :
Mym sakina ni miym ambayo haina i’rab ( مْ). Wataalamu wa tajweed wanataja hukuma zifuatazo kuhusu mym yenye sakina;-
i. إِدْغامُ الشَّفَ وِي Idghaam Ash-Shafawy
Hii hutokea pale ambapo miym yenye sakina ikukutana na miym yenye i’rabu yaani fataha, kasri au dhuma. Na inatakiwa mym yenye sakina ianze mwanzi kisha ifuatie mym yenye i’rabu, hivyo mym hii ya kwanza itaingizwa kwenye mym ya pili na kuwekwa shada ya pili na kusomwa kwa ghunnnah. Aina hii ya idgham pia huitwa إَدْغَامُ الْمُتَماثِلَيْن (Idghaamul-mutamaathilayni).
ii. إِخْ فَ اء الشَّفَ وِي Ikhfaaush-Shafawiy
Hukumu hii itapatikana pindi miym saakinah ( مْ) na herufi ya . ب, hivyo hapa mym sakina itafanyiwa ikhfaau kwenye ب, yaani mym ifafichwa kwa ghunnah.
iii. إظْهارُ الشَّفَ وي Idhwhaar Ash-Shafawiy
Hukumu hii hutokea wakati mym sakina inapokutana na herufi zozote isipokuwa م na ب, hivyoo hapa mym sakina itadhihirishwa yaani itatamkwa kama ilivyo pamoja na kuitenga na herufi inayofata bila ya kuleta ghunnah.
Umeionaje Makala hii.. ?
Ni zipi hizo herufi saba, na ni vipi viraa saba katika usomaji wa Quran
Soma Zaidi...Asbab nuzul surat al qadi. Hii ni sura ya 97 katika mpangilio wa mashaf. Surat al qadir imeteremshwa Madina na ina aya 5.
Soma Zaidi...Kutokana na kuishi kwao Misr kwa muda mrefu, Mayahudi waliathiriwa na ibada za kishirikina za Wamisr.
Soma Zaidi...Jifunze namna ya kusoma quran, pata mafunzo ya tajwid hapa
Soma Zaidi...