Mtume (s.
Mtume (s.a.w) ametuagiza katika Hadith maarufu kuwa tuswali kama alivyokuwa akiswali. Hivyo katika sehemu hii tutajitahidi kuonesha utekelezaji wa swala hatua kwa hatua kwa kurejea Hadith Sahihi za Mtume (s.a.w):
1. Nia na Takbira ya kuhirimia
Nia ni kudhamiria moyoni kuwa unaswali, swala unayoikusudia kisha unaanza swala kwa kusema: โAllaahu Akbarโ Allah ni Mkubwa kwa kila haliโ. Wakati wa kuhirimia swala ni sunnah kuinua viganja vya mikono,mkabala na mabega. Kuhusu unyanyuaji wa mikono mkabala na mabega imeripotiwa kuwa Mtume (s.a.w) alikuwa akifanya hivyo katika sehemu nne tofauti:
1. Wakati wa kuhirimia swala (kuanza swala).
2. Wakati anaposema Allaahu Akbar kwa ajili ya rukui.
3. Wakati anaposimama kutoka kwenye rukuu.
4. Wakati anaposimama kutoka kwenye tahiyyatu ya kwanza ili kuendelea na rakaa ya tatu.
Hii tunaipata katika Hadith aliyosimulia Abdullah bin โUmar kuwa: โMtume (s.a.w) aliposimama kwa ajili ya swala alinyanyua mikono yake mkabala na mabega yake na kisha kuhirimia (kusema Allahu Akbar). Alipotaka kurukuu alinyanyua mikono kama alivyofanya kwanza na aliposimama kwa ajili ya itidali alifanya hivyo hivyo na alisema Allah anamsikia yule anayemsifu. (Bukhari, Muslim na Bayhaqi).
Nafaโa(r.a) ameeleza kwamba Ibn โUmar (Abdullah)(r.a) aliposimama kwa ajili ya rakaa ya tatu alikuwa akinyanyua mikono; jambo ambalo alilihusisha na Mtume (s.a.w). (Bukhari, Abu Dawud, Nasai).
Baada ya kuhirimia swala mwenye kuswali hushusha mikono yake na kuiweka kifuani, mkono wa kulia ukiwa juu ya mkono wa kushoto kwa mujibu wa Hadith zifuatazo: Hulab At-Tai(r.a) amesimulia: โNilimuona Mtume (s.a.w) akiswali hali ameweka mkono wake wa kulia juu ya mkono wa kushoto juu ya kifua chake.โ (Ahmad na At-Tirmidh)
Naye Wail bin Hijr (r.a) ameripoti: โNiliswali pamoja na Mtume (s.a.w) na aliweka mkono wake wa kulia juu ya mkono wa kushoto juu ya kifua chakeโ. (Ahmad na At-Tirmidh).
Imamu Abu Dawud na Nasai wamepokea kutoka kwa Ibn Khuzaimah kuwa Mtume (s.a.w) alipokuwa akiswali alikuwa akiweka mkono wake wa kulia juu ya kiwiko (wrist) cha mkono wa kushoto na sehemu ya mkono inayofuatia kiganja .
Umeionaje Makala hii.. ?
Haki na uadilifu katika uislamu (EDK form 3:Dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Mambo haya yanaweza kuharibu funga ya mtu ama kupunguza malipo ya funga.
Soma Zaidi...Nguzo za uislamu,kutoa zakat na sadaqat (EDK form 2; dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...Nguzo za uislamu (EDK form 2: dhana ya elimu ya uislamu)
Soma Zaidi...ุนููู ุฃูุจูู ููุนูููู ุดูุฏููุงุฏู ุจููู ุฃูููุณู ุฑูุถููู ุงูููู ุนููููู ุนููู ุฑูุณูููู ุงูููููู ุตูู ุงููู ุนููู ู ุณูู ููุงูู: "ุฅููู ุงูููููู ููุชูุจู ุงููุฅูุญ...
Soma Zaidi...