Kusimamisha Swala.
Kusimamisha Swala.
Maana ya Kusimamisha Swala Kusimamisha swala ni tofauti na kuswali. Kuswali ni kufanya vitendo vya swala kama vile kusimama, kurukuu, kuitidali, kusujudu, n.k.
Kusimamisha swala ni kuitekeleza swala kwa kuchunga na kutekeleza kwa ukamilifu yafuatayo:
(i) Sharti zote za swala.
(ii) Nguzo zote za swala.
(iii) Kuwa na khushui (unyenyekevu) wakati wote wa kutekeleza sharti na nguzo za swala.
Mtu akiswali bila ya kuzingatia na kutekeleza kwa ukamilifu mambo haya matatu, ataonekana kuwa kaswali, lakini atakuwa hajasimamisha swala na atastahiki kuadhibiwa vikali na Mola wake kama tunavyojifunza katika aya ifuatayo: Basi adhabu kali itawathibitikia wanaoswali, ambao wanapuuza swala zao (kwa kutozisimamisha), ambao hufanya ria (107:4-6).
Kupuuza swala ni pamoja na kutotekeleza ipasavyo sharti za swala, nguzo za swala, na kutokuwa na unyenyekevu wakati wa kutekeleza sharti na nguzo za swala. Hivyo, swala inayokubalika mbele ya Allah (s.w) ni ile iliyosimamishwa kama tunavyojifunza katika aya zifuatazo: Hakika wamefuzu waumini ambao katika swala zao ni wanyenyekevu. (23:1-2) Na ambao swala zao wanazihifadhi. (23:9) Kuhifadhi swala ni kutekeleza kwa ukamilifu sharti na nguzo zote za swala.
Umeionaje Makala hii.. ?
Suala la omba-ombaTukiliangalia suala la omba-omba kwa upana kidogo, ambalo hivi sasa linaongelewa katika vikao mbalimbali vya kitaifa na kimataifa, tutaona kuwa ni Uislamu pekee unaotoa namna bora ya kulishughulikia suala hili.
Soma Zaidi...Hii ni orodha ya mambo ambayo hayawezi kuharimu funga yako endapo utayafanya.
Soma Zaidi...Huu ni utaratibu unaotakiwa kufanyika baada ya kuzika.
Soma Zaidi...Kwa nini ni muhimu kuswali? Post hii itakwenda kukufundisha kuhusu umuhimu wa kusimamisha swala.
Soma Zaidi...Hapa utajifunza jinsi ya kuozesha hatuwa kwa hatuwa. Pia utajifunza masharti ya kuoa na masharti ya kuolewa.
Soma Zaidi...