Makala hii inakwenda kukuletea somo linalozungumzia maumivu ya tumbo chini ya kitomvu, na tumbo la ngiri kwa wanaume, na tumbo la chango kwa wanawake
NINI HUSABABISHA MAUMIVU YA TUMBO CHINI YA KITOMVU KWA WANWAKE NA WANAUME?
Watu wengi wamekuwa wakilalamikajuu ya maumivu makali ya tumbo chini ya kitomvu. Tatizo hili linaweza kuwapata wanawake na wanaume pia. Kwa upande wa wanawake tatizo hili limekuwa ni kawaida hasa wakati wa kukaribia kuingia siku zao. Kawaida maumivu haya hayana shida sana kiafya lakini ikzidi uangalizi wa dakatari unahitajika. Je na wewe ni muhusika wa maumivu haya? Makala hii itakuwa ni jibu lako.
Makala hii inakwenda kukuletea somo linalozungumzia maumivu ya tumbo chini ya kitomvu. Ni katika maumivu amaboyo kwa wanaume mara nyingi huhusishwa an ngiri na kwa upande wa wanawake huhusishwa na chango hasa pale wanapokaribia kuingia katika siku zao. Makala hii itakuletea sababu za maumivu ya tumbo chini ya kitomvu kwa wanwake na wanaume.
Maumivu ya tumbo kitomvuni
Eneo hili la kitomvuni kitaalamu hufahamika kama umblical region. Eneo hili la tumbo linahusisha viungo kama tumbo la chakula, utumbo mdogo, utumbo mkubwa na kongosho. Hivi ni katika viungo muhimu sana katika mmengenyo wa chakula, na afya ya mtu kwa ujumla.
SABABU ZA MAUMIVU YA TUMBO KITOMVUNI
1.Kuwepo na uvimbe kwenye njia ya chakula (digestive track) kitaalamu hufahamika kama gastroenteritis. Hali hii inaweza kusababishwa na virusi, bakteria ama parasite. Mgonjwa anaweza kusikia maumivu na yanaweza kuwa ni makali sana. Mara nyingi maumivu haya yanapoa yenyyewe bila hata kuhitaji matibabau ha huondoka ndani ya siku chache. Ila ni vyema kumuona daktari kwa uchunguzi zaidi.
2. Kuvimba kwa appendix. Maumivu ya tumbo kwenye kitomfu yanaweza kuashiria ugonjwa wa appendix, kitaalamu hufahamika kama appendicitis. Kama utahisi maumivu makali ya tumo kitomvuni kisha ghafla yanahamia upande wa kulia wa tumbo kwa chini, huashiria tatizo hili.
3.Vidonda vya tumbo
Yes maumivu ya tumbo kitomvuni yanaweza kuwa yamesababishwa na vidonda vya tumbo, huwenda vipo kwenye tumbo la chakula ama sehemu ya juu ya utumbo mdogo inayotambulika kama duodenum.
3. Matatizo kwenye kongosho
Huu ni ugonjwa unaosababisha kuvimba kwa kongosho kitaalamu huitwa Pancreatitis. Maradhi haya yanaweza kuja ghafla sana bila ya kuonyesha ishara za awali.
5.Kuwa na ngriri ya henia
Ugonjwa huu huwapata wanaume, na hutokea pale ambapo baadhi ya tishu za tumboni zinapoingia kwenye misuli ya tumboni karibu na kitomvu. Kwa watu wazima upasuaji hufanyika ili kutibu tatizo.
6.Kama kuna kizuizi katika utumbo kinachozuia chakula kutembea. Tatizo hili likichelewa kutibiwalinaweza kuwa hatari zaidi. Tatizo hili huweza kusababishwa na:-
1.Mashambulizi ya bakteria
2.Henia
3.Uvimbe
4.Kama kulitokea shida wakati wa kufanyiwa upasuaji.
7.Matatizo katika mishipa mikuu ya damu kwenye tumbo (aortic aneurysm). hili ni tatizo la kiafya linalosababishwa na kudhoofu na kutanuka kwa kuta za mishipa mikuu ya damu. Hali hii inaweza kuhatarisha maisha ya mtu kama mishipa ya damu itapasuka na kupelekea damu kuingia tumboni, hii inaweza kupelekea maumivu makli. Maumivu haya yanaweza kuathiri na viungo vingine.
8.Kama kutakuwa na shida wakati wa mzunguko wa damu katika tumbo (mesenteric ischemia). hii hutokea endapodamu inayotembea kwenye utumbo mdogo itapata usumbufu, kwa mfano ikiganda. Mgonjwa anaweza kusikia maumivu makali ya tumbo. Maumivu haya huandamana na dalili kama:-
1.Kuongezeka kwa mapigo ya moyo
2.Kuona damu kwenye choo
Umeionaje Makala hii.. ?
Hapa utajifunza muda mabao dalili za VVU na UKIMWI huonekana, na kwa muda gani mgonjwa ataishi na UKIMWI bila ya kutumia ARV
Soma Zaidi...Tofauti na maradhi yaliyotajwa hapo juu pia tafiti za kisayansi zimethibitisha kuwepo kwa maradhi mengine hatari yanayosambazwa na mbu, kama vile ngirimaji pamoja na matende.
Soma Zaidi...Hapa utajifunza sababu za kuwepo na maumovu ya tumbe kitomvuni.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi Magonjwa vya kurithi ambayo mara nyingi utokea kwenye jamii ni magonjwa ambayo yanaweza kutokea kwenye familia na wanafamilia walio wengi wakaweza kupata ugonjwa huo Magonjwa yenyewe ni kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi watu walio katika hatari ya kupata Maambukizi ya ugonjwa wa ukimwi,ni kutokana na kazi zao pamoja na mazingira yao kwa hiyo wako kwenye hatari ya kupata Ugonjwa wa ukimwi.
Soma Zaidi...Saratani ya kibofu cha nyongo ni Saratani inayoanzia kwenye kibofu cha nyongo. Nyongo yako ni kiungo kidogo, chenye umbo la peari upande wa kulia wa tumbo lako, chini ya ini lako. Kibofu cha nyongo huhifadhi nyongo, Kioevu cha usaga
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi mtu aliyekula chakula chenye sumu, chakula chenye sumu ni chakula ambacho kikitumiwa na mtu yeyote kinaweza kuleta madhara kwenye mwili wa binadamu hata kifo.
Soma Zaidi...Somo hili linakwenda kukueleza kuhusu vyakula hatari kwa mwenye vidonda vya tumbo
Soma Zaidi...Je unapata dalili zisizoeleweka ni ni za mimba ama laa. Hapa nitakujuza hali baadhi ya wanawake zinazowatokea.
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi matibabu ya vidonda vya tumbo nyumbani, ni njia ya kawaida ya kujitibu vidonda vya tumbo kama tulivyoona.
Soma Zaidi...