picha

NDOA YA SINBAD NA BINTI WA MFALME

Download kitabu Hiki Bofya hapa NDOA YA SINBAD NA BINT MFALME.

NDOA YA SINBAD NA BINTI WA MFALME

pic
Download kitabu Hiki Bofya hapa

NDOA YA SINBAD NA BINT MFALME.

Siku hazikuenda kipolepole hatimaye wiki ikafika na harusi ikafanyika. Sherehe kubwa isiyo na kifani ilifanyika na hata wafalme wa jirani walihudhuria. Niliozeshwa binti yule na kukabidhiwa nyumba ndani ya ikulu. Nilipata kukabidhiwa na mali na mambo mengine kadhaa. Sherehe za kimila pia zikafanyika kwa ajili ya kukabidhiwa cheo cha mfalme ajae yaani baada ya kufa mfalme huyu nitakuwa mfalme mpya. Yote haya yalifanyika japo sikuwa na furaha nayo.

Ni miezi miwili sasa imefika na mishaanza kuzoea mazingira ya kulinda muda wote na kuzungukwa na watu. Nilitembelea uwanja wa kujifunzia farasi nikakuta watu wanaendesha farasi bila ya kuweka kiti chha farasi. Basi nikatumia taaluma nilonayo na kuwatengezea viti vya farasi. Jambo hili lilifanya nipendwe sana na watu na mawaziri kwa kuleta kitu kipya zaidi. Mapenzi ya mfalme na mimi yalizidi kuongezeka siku hadi siku. Watu walikuwa wakinikubali sana hasa ninapokuwa nawasimulia hadithi za kuhusu baghadad na safari za majini na mikasa iliyowahi kunikuta.

Ni miezi mitano sasa toka kumuoa binti mfalme. Binti mfalme alinipa habari za furaha kuwa ana ujauzito. Nilizipeleka habari zile kwa babamkwe na mama mkwe. Kwa hakika siwezi kusimulia namna ambavyo furahayao ilivyokuwa. Habari ziliwafikia mawaziri na watu wengine. Wote walikuwa wakiniupongeza. Binti mfalme alizidi kuniona mimi ni mtu muhimu sana kwenye maisha yake kwa kumfanya awe mama mtarajiwa wa familia ya mifalme.

Hatimaye miezi ya kujifunguwa ya binti mfalme imefikia na sasa amepelekwa kwa wakunga. Nikiwa nipo mlangoni kusubiria habari za furaha nilishitushwa na kilio kikubwa sana kilichotoka ndani. β€œInnaa lillahi wa innaa ilaihi rajiun” niliposikia maneno haya yakisemwa nikajua mtoto wangu amefariki dunia. Nilianza kulia sana, na muda si mrefu mkunga mmoja akatokea nje na kuniambia kuwa binti mfalme amefariki dunia na mtoto wake amepona. Nililia zaidi na kutamani ardhi inifukie.

Furaha za kupata mtoto sikuweza kuzipata kamwe nikikumbuka kuwa nakwenda kuzikwa na me wangu. Mila haikuwacha kufuata mkonowake sasa mwili wa marehemu ukawa unaanza kuandaliwa na nikamuona baba mkwe akija kwa unyonge na kunipa maelekezo na kunipatia nguo mpya na kuniambia hizi zitakuwa ndio sanda yako. Sina la kukusaidia lamba nitakuongezea mkate wa nane. Maana huwa aliye hai anapozikwa na mwenza anapewa kichupa cha maji na mkate mikate 7 hivyo nitakupendelea kukupa mikate nane.

Maneno haya yaliendelea kuniumiza hasa pale watu walipokuja kunihani na kuniaga kwa mara ya mwisho. Sasa ndipo nikaanza kujuta kukubali kutembea majini safari hii. Nilitamani hata ningekuwa kama wale wenzangu nilowaaza kule wanachinjwa maana taabu nitakayoiona na kuzikwa nikiwa hai ni kubwa. Basi likaandaliwa jeneza moja kubwa sana na mimi na mke wangu tukaingizwa na kubebwa kuelekea mazikoni. Walikwenda kwa muda wa masaa 2 na nusu kisha wakaanza kupandisha juu kwa mwendo wa nusu saa. Nikawasikia wanazungumza kuwa wamefika tayari.


                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 2018-08-01 Topic: Aliflela1 Main: Burudani File: Download PDF Views 1856

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
πŸ‘‰1 Bongolite - Game zone - Play free game    πŸ‘‰2 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    πŸ‘‰3 ai web app    πŸ‘‰4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    πŸ‘‰5 Kitabu cha Afya    πŸ‘‰6 web hosting   

Post zinazofanana:

Malipo ya wema ni wema

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...
HADITHI YA CHONGO WA PILI MTOTO WA MFALME

Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA CHONGO WA PILI MTOTO WA MFALME.

Soma Zaidi...
MWANZO WA USALITI

Download kitabu Hiki Bofya hapa USALITI UNANZA HAPA Baada ya kukaa pale siku moja nahodha akaamrisha chombo kiondoke pale na kurudi nyumbani.

Soma Zaidi...
SAMAKI WA AJABU

Download kitabu Hiki Bofya hapa SAMAKI WA AJABU Walikwenda upane wa magharibu na mji wakauacha upande wa kusini.

Soma Zaidi...
SAFARI YA TANO YA SINBAD

Download kitabu Hiki Bofya hapa SAFARI YA TANO YA SINBAD Baada ya watu kukusanyika siku ilofata sinbad akaanza kusimulia stori ya safari yake ya tano.

Soma Zaidi...
Hadithi ya tabibu wa mfalme

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...
HADITHI YA TABIBU NA MFALME

Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA TABIBU WA MFALME Katika nchi ya Zouman iliyopo maeneo ya uajemi alikuwepo mfalme mkubwa sana.

Soma Zaidi...
HADITHI YA MFALME NA WAZIRI WAKE

Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA MFALME NA WAZIRI WAKE Basi tambueni enyi rafikizangu kuwa mimi na waziri wangu huyu hatutokani na familia za kifalme wala mimi baba yangu hahusiani hata kidogo na ufalme.

Soma Zaidi...
SAFARI YA SABA YA SINBAD

Download kitabu Hiki Bofya hapa SAFARI YA SABA YA SINBAD Walipokusanyika siku ilofata Sinbad akawaambia kuwa kilichofanya nikavunja ahadi yangu ya kutosafiri tena ni kauli ya Sultani Nilipopunzika kwa muda wa miezi miwili nilipata habari kuwa Sultani

Soma Zaidi...
Safari ya majibu juu ya maswali mawili

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...