Muendelezo wa hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza...
SAFARI YA TANO YA SINBAD
Baada ya watu kukusanyika siku ilofata sinbad akaanza kusimulia stori ya safari yake ya tano. Akaanza kusema kuwa “niliamua kutokuenda tena safari yoyote ya majini. Hali ilikuwa hivyo lakini baada ya miezi mingi nikapata wazo la kutengeneza jahazi langu ambalo litakuwa ni madhubutizaidi. Kwa mali nilizo nazo wakati huu nikaanza kuandaa jahazi kubwa na la kisasa lililo madhubuti sana. Muda ulitimia na jahazi kubwa na la kisasa zaidi lilikamilika.
Nikaanza kualika wafanyabiashara wakubwawakubwa na walio wazoefu zaidi. Tuliandaa bidhaa zetu na tukamtafuta nahodha aliye mahiri na safari hizi. Maandalizi yalipokamilika tukaanza safari usiku kwa kulingana na uwepo wa upepo.
Kwa hakika safari ilikuwa njema, tuliweza kupita kwenye mikondo mikubwa na tukaingia visiwa kadhaa. Kwa hakika nahodha huyu alikuwa ni hodari na ni mzoefu, kwani hatukupita kisiwa ila alikuwa akitueleza habari zake. Hata visiwa visivyoishiwa na watu alikuwa akitueleza habari zake. Tulipita kenye kisiwa cha mawe yanayolia. Tukamueleza nahodha atuambie habari za mawe yale kaanza kutusimulia hadithi hii;
Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetuUmeionaje Makala hii.. ?
Simulizi ni nzuri sana maana zinafundisha na hazibagui mkubwa wala mdogo... tusikilize na kusoma kisa cha tabibu wa mfalme....kutoka katika kitabu cha kwanza cha HALIF LELA U LELA...
Soma Zaidi...Simulizi za HALIF LELA U LELA zipo nyingi sana na husikiliwa na kusomwa na wakubwa kwa wadogo pia hadithi hizi zimeenea duniani Kate zikisikilizwa na maelfu ya watu mbalimbali.
Soma Zaidi...Kojawapo ya simulizi iliyopo kwenye kitabu cha pili cha hadithi za HALIF LELA U LELA.....
Soma Zaidi...Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha pili.....
Soma Zaidi...Simulizii hii inapatikana katika kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA
Soma Zaidi...Hadithi hii inapatikana katika kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA....
Soma Zaidi...