picha

Simulizi za Hadithi EP 5 Part 7: Sehemu ya nne ya safari ya Sinbad

Muendelezo wa hadithi ya safari ya safari ya Sinbad iliyopo kwenye hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza.....

SAFARI YA NNE YA SINBAD

 

Basi ikafikia siku ya kuanza safari yangu ya nne ya kibiashara. Tulianza safari ile usiku hata ikafika asubuhi tukiwa katikati ya maji. Njia ya safari hii sikuwa na uzoefu nayo na niliona mambo mapy. Niliweza kuona majabali yalofanana na watu, wanyama na vitu mbalimbali. Pia tuliweza kuona mawe ya ajabu ambayo huwa hayapati maji sikuzote. Tukiwa karibu ya kuingia kwenye kisiwa chetu cha kwanza kwa ghafla tulivamiwa na majiwatu makubwa na yenye nguvu sana.

 

Watu hawa walifanikiwa kututeka sote tuliokuwa mule ndani ya jahazi lile. Walitukamata wote na kutufunga kamba na kutuziba macho yetu kwa vitambaa hata tusione wapi tunakwenda. Walitupeleka tusikokujuwa na kwa kuelewa tu niliona kama tunarudinyuma. Waliturudisha nyuma kwa muda wa takribani masaa matatu kisha tukaelekea upande wa kushoto na kukiwacha kile kisiwa tulokuwa tukikiona kuliani. Tulikwenda kwamuda wa takribani masaa sita. Nikiwa nachukuwa hisia juu ya safari ili niligunduwa kumbe wanatuzungusha tuu lakini tunatupeleka pale kwenye kisiwa kile tulichokiona.

 

Hatimaye tukawasili na wakatufungua machoyetu na hapo nikapata tena kuona ardhi nzuri yenye udongo mweupe wa kupendeza. Wale watu wakawa wanagawana kila mmoja kucukuwa watu kadhaa katika sisi. Waligombaniana watu wote na kubakia mimi. Walichelea kunichagua kwa sababu nilikuwa nimekonda sana. Basi akatokea mzee mmoja wa heshima katika wao akanichukuwa. Basi wote tuliingizwa kwenye jumba moja na kuletewa chakula kilichofanana na machicha ya nasi. Bila ya kuchelewa wenzangu wakaanza kula chakula kile ila mimi nikachelea kukila hata kikaisha.

 

Baada ya muda tukaletewa majani mithili ya majani ya miwa lakini haya yana maji mengi na ni matamu sana. Mimi sikuyala kwa kuhofia usalama wangu. Niliweza kugunduwa ladha yake kwa kuhadithiwa na wenzangu. Nilikaa na njaa kwa muda wa siku mbili hata nikakosa nguvu. Yule mzee akamiletea samaki wa kuchoma pamoja na mayai ya kasa. Nilikula sana hata nikashiba. Nilipopata nduvu ziku ya tatu nikaona mabadiliko kwa wenzangu. Walikuwa wakinenepa sana kwa ghafla kila walipokula vyakula vile. Kitu cha kushangaza wakawa wanapoteza kumbukumbu na kuwa na akili ya kinyama kinyama.

 

Hali iliendelea hivi kwa muda wa wiki tatu hata akawa mmoja kati ya wenzangu hawezi kupita kwenye mlago kwa unene. Basi wale watu wakawa wanamchukuwa mtu mmojammoja kila wiki na kuondoka nae na asirudi. Nikawa nafatilia nini kinaendelea hata nikagunduwa kuwa wanakwenda kumchinja na kumuuza nyama kwenye kisiwa kingine. Niolijaribu kuwaeleza wenzangu lakini wamekuwa wanyama hakuna walijualo zaidi ya kula tu. Mimi niliendelea kula vyakula kwa kuiba na hali yangu ikazidi kudhoofu.

 

Yule mzee akaamuwa kunitoa bandani mule kwa kuamini nikiwa huru naweza kunenepa. Hali iliendelea hivyo hata nikapewa funguo ya kuwalinda wenzangu. Waliendelea kuchinjwa hata wakabakia watu kumi na mbili. Kuna siku kulikuwa na sherehe na watu wakaondoka na kuniacha mimi na yule mzee. Basi nilitoroka pale peke angu kwani ningemhukuwa yeyote asingekubali na kwa unene na uzito alonao asingeweza kukimbia hata kidogo. Basi nilitoroka kwenda mbali zaidi.

 

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Mankaa image Tarehe: 2024-09-10 Topic: Simulizi za Hadithi Main: Burudani File: Download PDF Views 860

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
👉1 Dua za Mitume na Manabii    👉2 Madrasa kiganjani    👉3 kitabu cha Simulizi    👉4 Tafasiri ya Riyadh Swalihina    👉5 Kitabu cha Afya    👉6 Bongolite - Game zone - Play free game   

Post zinazofanana:

Simulizi za Hadithi EP 5 Part 13: Sehemu ya sita ya safari ya Sinbad

Muendelezo wa safari ya Sinbad iliyopo ndani ya kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA...

Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 2 Part 2: Hadithi ya mzee wa kwanza na mbuzi wake

Simulizi za HALIF LELA U LELA zipo nyingi sana na husikiliwa na kusomwa na wakubwa kwa wadogo pia hadithi hizi zimeenea duniani Kate zikisikilizwa na maelfu ya watu mbalimbali.

Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 4  Part 13: Simulizi ya nyani kibadilika kuwa chongo

Mwendelezo wa hadithi zetu nzuri na za kusisimua kutoka katika kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA.....

Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 5 Part 2: Sehemu ya safari ya kwanza ya sinbad

Muendelezo wa stori ya safari ya Sinbad ambayo ipo kwenye kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA....

Soma Zaidi...
Simulizi za Hadithi EP 6 Part 10: Mapenzi kwenye mtihani

Simulizii hii inapatikana katika kitabu cha pili cha hadithi za HALIF LELA U LELA....

Soma Zaidi...