image

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 19: Kinyozi

Hii ni simulizi iliyopo ndani ya kitabi cha pili cha hadithi za HALIF LELA U LELA.....

HADITHI YA KINYOZI

 

 

Baba yangu alikuwa ni mfanyabiashara mkubwa nchini Misri. Hakujaaliwa kuwa na watoto wengi, ni mimi tu ndiye niliyekuwa mtoto wa pekee katika jumba la Tajiri. Baba yangu alifariki na kuniwachia mali zake zote. Nilikuwa naishi na bibi pamoja na watumwa wa baba waliokuwa ni wafanyakazi wangu. Pia nilikuwa naishi na mama yangu. Sikuwa na mke hivyo nilikuwa nikila nyumbani. Sikuwa na hamu na mwanamke, yaani ni kama mtu aliyerogwa. Nilikuwa nikichukia sana mwanamke, niliamini kuwa nikiwa karibu na wanawake nitaweza kufilisika. Wanawake pekee niliokuwa nikiwaheshimu na kufurahia uwepo wao ni ndugu zangu na watu wengine wa karibu na familia yangu.

 

 

Hali hii ilinifanya niwaze sana kuendeleza biashara kuliko kucheza na wanawake hasa wale wa mitaani. Umri wangu ulizidi kwenda na hatimaye wakati wa kuoa ulifika. Nilitamani sasa kutafuta mchumba lakini moyo ulikuwa ukinisuta maana wale nilokuwa nawachukia sasa natakiwa nitafute nitakaeishi naye milele. Chuki yangu haikuisha hivyo ikawa vigumu kwangu kumpata mchumba kutoka mabinti waliyopo mtaani. Niliamini njia pekee ni kutoka nje ya mji n kwendatafuta mke vijijini ama mji mwingine.

 

 

Sikumoja katika pirika zangu za utafutaji , wakati wa jioni ulinikuta pembeni ya jumba moja la kitajiri. Niliwa pembeni nimekaa napiga mahesabu yangu ghafla dirisha kubwa likafunguliwa na nikaona ukumbi mkubwa sana kwenye jumba la tajiri. Bostani zuri sana lilionekana kwenye kumbi hilo kubwa. Nilipoangalia vyema kumbi lile halikuwa lenye kufunikwa juu, mwangaza mzuri ulikuwa ukipenya kwa juu. Niliamini itakuwa wemefunika kwa turubai la mpira.

 

 

Mauwa mazuri yalijibanga vyema, harufu mwanana ilikuwa ukipenya puani mwangu. Mauwa yalichanua vyema na kufanya ji ukimbi lingare na kuvutia mtazamaji. Ilitulia kidogo huku nikithaminisha uzuri ulioje wa bustani lile. Wakati nikiangalia zaidi ghafla sura nzuri ikatokea nyuma ya uwa moja kubwa. Loo! Ni mwanamke mmoja mzuri sana alikuwa nakuja huku akiwa amebeba keni la kumwagilia mauwa.

 

 

Nikatafuta sehemu nzuri ya kukaa nipate kumuona vyema. Nilianza kuvutiwa na urefu alio nao, kwani hakuwa mfupi mno na si mrefu mmo. Nilipata kuiona vyema sura iliyo na ngozi nyeupe, pua iliyo tokeza vyema, macho makubwa kama mwanamwari wa pakistani. Nikiwa mbali kidogo nilitamani kusogea jirani ili nillihofu kumshitua, nilipata mwanya wa kujibanza sehemu nikaanza kumuona vyema. Nikaanza kutazama kwenye maeneo kadha na kugundua makubwa mabayo wengi katika wanawake wa mtaani hawakuwa nayo.

 

 

Kirundo cha nywele kilionekana ndani ya hijabu, kirundo kilishuka mpaka mgongoni, nilianza kuhisi mapigo ya moyo kama yanabadilika. Wakati alipokuwa akinyanyua keni na kuanza kumwagilia mauwa nilipata kuona bangili kwenye mgono wake. Zilikuwa zikimeremeta sana. Niliamini kuwa bila shaka ni babguli za dhahabu. Ziliweza kugongana na kutoa mlio mzuri. Nilianza kunogewa na uwepo wa mwanamwari. Nilibahatika kuona nyusi zilizotiwa wanja na kunyooka kama mbalamwezi ya mwezi mwandamo.

 

 

Akiwa anaendelea kumwagilia mauwa ghafla nyuki akamuingia kwenye hijabu yake. Akiwa katika harakati za kumtowa nyuki alimuuma na kutoa miguno ya maumivu. Sauti ile ilikuwa ni kama moto uliomwagiwa petroli kwenye moyo wangu. Binti aliendelea kumtoa nyuki, hatimaye akapunguza baadhi ya mafazi yake kwa haraka. Nilianza kukodoa mimacho nipate kuona vya ndani. Ghafla dirisha likafungwa, na nisijuwe nini kimeendelea zaidi. Kwa unyonge na upole nilirudi nymbani na kujitupa kitandani.

 

 

Sikuthubutu kula wala kunywa, hamu ya kula, kuzungumza na kunywa ilitoweka yote. Ghafla nilionyesha dalili za kuumwa na nikaanza kuchemshiwa dawa. Bibi yangu akaja ndani na aliponiangalia tu akagunduwa kuwa kuna jambo linaendelea. Bibi akaendelea kunidodosa ili apatekujuwa undani ndipo nikamuhadithia vyete vilivyonikuta. Bibi akanieleza “usipatetabu mjukuu wangu, mimi binti yule ninamjuwa na hata kwao ninakwenda sana, nitaongea naye kisha nitakuja kupa jibu ni lini ukutane naye”. baada ya kusikia maneno yale nilifurahi sana na hapohapo nikapona.

 

 

Siku mbili zikapita bila ya bibi kunieleza chochote, hatimaye nikaanza kuumwa tena. Siku ya tano bibi akaja chumbani kwangu na kuanza kunipa habari za furaha. Bibi akanieleza kuwa “Nilikwenda kumfata yule binti, na nikamueleza kuhusu ugonjwa wako baada ya kukuona. Alichonijibu kuwa hata yeye alikuona na hakutaka ufahamu, alianza kukupenda tuka alipokuona. Naye toka mlipoonana hakuamka kitandani kwa kukuwaza na asijuwe wewe ni nani na atakupata wapi. Hakuweza kuamini kama wewee ni mjukuu wangu. Hivyo ameniomba mkutane kesho kabla ya kutoka watu msikitini, maana geti lao litafunguliwa kwa ajili yako lakini ukichelewa baba yake atarudi na hutopata nafasi tena”

 

 

Maneno ya bibi yakuwa kama mkuki wa furaha uliokita katikati ya moyo wangu. Kwa furaha nilimkumbatia bibi na kumbusu. Ilikuwa ni siku ya Al-hamisi, nilitamani iwe ijumaa. Siku ya ijumaa hatimaye ikifika na asubuhi baada ya kupata kifungua kinywa bibi akaja na kunieleza kuwa nishevu nywele zangu vizuri nipendeze. Nikaagiza kijana aende akaniletee kinyozi anayesifika. Basi ndipo nikaletewa kinyozi huyu mnayemona hapa. Na hapo ndipo mambo yalipoanza kuharibika.

 

 

 





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Mankaa Tarehe 2024-09-10 14:19:49 Topic: Simulizi za Hadithi Main: Masomo File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 40


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Kitabu cha Afya     👉3 Madrasa kiganjani     👉4 Kitau cha Fiqh     👉5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉6 Simulizi za Hadithi Audio    

Post zifazofanana:-

Simulizi za Hadithi EP 10 Part 1: Carmaralzamani prince pekee
Muendelezo.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 7 Part 11: Ndani mwa junba la Aladini
Muendelezo.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 2: Sultani mtoa buradani kufariki
Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha pili..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 5 Part 3: Uokozi kwenye kisiwa
Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza...... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 7 Part 2: Aladini kwenye pango la utajiri
Muendelezo..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 2 Part 1: Hadithi ya jini na mfanya biashara.
Hadithi hii ya jina na mfanya biashara imetoka katika kitabu cha kwanza cha simulizi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza karibu tusikilize simulizi nzuri na zakusisimua Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 23: Kaka wa pili wa kinyozi
Muendelezo..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 7 Part 8: Harusi ya aladini kufanyika na binti wa mfalme
Muendelezo...... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 7 Part 4: Mshenga wa Aladini
Muendelezo.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 7 Part 10: Jumba la Aladini
Muendelezo..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 4 Part 4: Simulizi ya chongo wa kwanza mtoto wa Mfalme
Tusikilizie simulizii inahusu chongo wa kwanza wa mtoto wa mfalme iliyopo ndani ya kitabu cha kwanza cha Hadithi za HALIF LELA U LELA..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 9 Part : Hatma ya Nurdini
Muendelezo.... Soma Zaidi...