image

Simulizi za Hadithi EP 9 Part : Bostani la kifalme baghadad

Muendelezo.....

KATIKA BOSTANI LA KIFALME BAGHADAD

Basi Nurdini na mke wake bila hata ya kujuwa wapi watafikia waliingia kwenye mashua na kuwasili Baghada wakati wa jioni. Walijikongoja hata wakafika kwenye geti kubwa sana na lenye mlango mkubwa ulio madhubuti sana. Keti hili lilikuwa ni mlango wa kuingi;ia kwenye bostani la kifalme, kwenye ikulu ndogo. Mfalme wa wakati huo wa Baghadad alikuwa na bostani lake ambapo haruhusiwi mtu yeyote kuingia bila ya ruhusa yake. Watu wote walikuwa wakiliogopa bostani hili kwani watu wengi wamepotea kwa kukiuka amri ya mfalme. Sasa Nurdini yupo hapa yeye na mkewe. Hawana yeyote wanayemjuwa. Njaa na uchovu kwa pamoja vinawapa wakati mgumu sana.

 

 

 

Waliamuwa kujitupa nje ya geti hili, na baada ya muda kidogo wakapitiwa na usingizi. Mlinzi wa bustani hili alijulikana sana kwa uhodari wake wa kulilinda vyema bostani hili. Mlizi huyu alitambulika kwa jina la Ibrahim. Alikuwa ni mzee mrefu mwenye ndevu nyingi nyeupe. Alikuwa na upara na hakupenda kuvaa kilemba mara kwa mara. Hakuwa ni mrefu lakini alikuwa na nguvu sana. Aliweza kulilinda bostani kwa miaka 13 sasa. Siku ya leo alitoka kidogo kwenda kununua mahitaji yake. Sasa wakati aliporudi anakuta kuna watu wawili wamelala pembeni ya geti.

 

 

 

Mzee huyu akaingia chakani na kukata mikwaju mikubwa miwili. Akiweka azma ya kwenda kuwatia adabu watu wale na iwe fundisho kwa watu wengine. Mzee alipikata fimbo yake akasogea karibu na watu hawa. Akanyanyuwa mikono akuiwa amekamata kiboko chake barabara. Alipokaribia kuwatandiak akajiwa na roho ya imanai. Akawaza huwenda watu hawa ni wageni ama hawatambui chochote. Na si jambo la kiungwana kumuadhibu mtu kwa kosa asiolijuwa kuwa ni kosa.

 

 

 

Hapo akaamuwa kwanza kuwakaguwa surazao. Alipo angalia my wa kwanza akakuta ni kijana mtanashati hivi mwenye shura nzuri. Aliweza kumfananisha na marehemu mtoto wake aliyefariki miaka mitatu liyopita kwa ajali. Alipomkaguwa mtu wa pili “loo! Alikuwa ni mrembo wa kike, mwenye sura ya kupendeza sana”. Mzee aliishiwa na nguvu zote za kutaka kuwaadhibu. Kwa upole akaanza kumuamsha Nurdini kwa kumtingisha. Kisha akamuamsha na yule bint. Mzee akaanza kuwauliza maswali ya kawaida sana kuhusu majina yao na je ni wageni amawenyeji.

 

 

 

Mzee alizungumza nao mawili matatu, huku macho yake hayaondoki kwa yule binti. Ilipofika jioni mzee akaona ni vyema kuwakaribisha ndnani ya bostani wapate chochote. Huu haukuwa ni uwamuzi rahisi kwani ni kukiuka amri ya mfalme. Ila mzee alijifariji kwani mara ya mwisho alipokamata matu mafalme akamwambia akikamata mtu wingine amfanye vyebyote atakavyo. Hivyo leo anaamuwa kuitumia kauli ile kwa kufanya vyovyote atakavo.

 

 

 

Mzee aligunduwa kuwa vijana hawa ni wacheshi sana maana walikuwa wakifurahi na kucheka. Walipoingia ndani Nurdini akakutana na kajibanda kakubwa kalikojengewa juu kama mlimani, kakiwa kamezungukwa na bostani kubwa la matunda, mauwa na vitu vingi vya kupendeza. Sautiza wadudu wa usiku vilisikika vyema kwa sauti za kupendeza sana. Mzee akawapatia avijana chakula wakala kwa pamoja kwa muda hivi. Ilikuwa ni usiku sana, Nurdini akaomba apewe mvinyo.

 

 

 

Hapo mzee akaleta juisi nzito a tende, iliyochanganywa na maziwa ya ngamia. Nurdini aliifurahiya japo hakikuwa kitu anachokitaka. Kisha akamwambia mzee nahitaji pombe. Mzee alishangaa sana na kubadilika sura “pombe haujui kana ni haramu, amelaaniwa mnywaji, muuzaji, mnunuaji, mtengenezaji na mbebaji” hivyo unataka nikuletee pombe na mimi nilanike? Nurdini alikuwa ni mwerevu, akamwambia mzee je kama hutakuwa mmoja kati ya hao waliolaaniwa utatuletea? Mzee akauliza kivipi?

 

 

Nurdini akamwambia ni farasi wako, neda mtaani kampe mtu yeyote pesa akununulie, atakapoleta mwambie aweke pombe kwenye farasi na aifunge vyema. Uatakaporudi mimi nitauchukuwa kutoka kwenyefarasi, ukifanya hivi hutaingia kwenye laana maana alienunuwa ni mwengine na aliyebeba ni farasi. Mzee alicheka sana aliposikia maneno haya. Akamkabidhi funguo Nurdini na kumwambia afunguwe moja ya chumba. Huko akakuta pombe nyingi tuu. Akachukuwa birika moja na kuja nalo nje,

 

 

 

Bila ya kupoteza muda yeye na mke wake wakaanza kunywa. Baada ya kunywa kidogo akajiangusha na kujifanya amelewa sana. Muda wote mzee alikuwa akimwangalia bimti anavyokunwa pombe, hata akabakia peke yake baada ya Nurdini kuanguka chali. Mzee uzalendo ukamshinda kaamuwa kujiunga na unywaji. Haikupita muda naye akalewa chakali. Binti akaomba ruhusa awashe taa. Akaambiwa awashe moja ila wenge la pombe akaenda kuziwasha zote karabai nane, loo mwanga mkali sana ukawaka pale kama vile kuna mwezi umeangauka kwenye bostani. Waliendelea kunywa na kuanza kuimba na kucheza kodogo kidogo hata mambo yakawakolea na wasijue tena kinachoendelea kati yao.

 

 

 

Mfalme akiwa ikulu alishangaa sana kwenye bostani lake taa zinawaka bila ya ruhusa yake. Kwanza alimuita waziri mky na kumkemea sana. Kisha aanzaa kumuhoji. Waziri mkuu akaanza kumtetea mzee ibrahimi, ila mwisho wa siku naye akaonekana yu makosani. Waziri akaamuwa aende mwenyewe akashuhudie nini kimetokea bila ya idhini yake. Mfalme hakwenda peke yake havyo akamchukuwa waziri mkuu wake.





           

Je! umeipenda hii post?
Ndio            Hapana            Save post

Mankaa Tarehe 2024-09-10 15:02:10 Topic: Simulizi za Hadithi Main: Masomo File: Download PDF     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 74


Sponsored links
👉1 kitabu cha Simulizi     👉2 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     👉3 Kitabu cha Afya     👉4 Simulizi za Hadithi Audio     👉5 Madrasa kiganjani     👉6 Kitau cha Fiqh    

Post zifazofanana:-

Simulizi za Hadithi EP 4 Part 20: Waliodhulumiwa kufanyiwa suluhisho
Ni mojawapo ya simulizi iliyopo kwenye kitabu cha kwanza cha hadithi za HALIF LELA U LELA.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 7 Part 9: Familia mpya
Muendelezo..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 10 Part 1: Carmaralzamani prince pekee
Muendelezo.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 10 Part 7: Taharuki
Muendelezo..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 7 Part 7: Upendo uliotafsiriwa
Muendelezo.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 2: Sultani mtoa buradani kufariki
Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha pili..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 28: Hadithi ya mshona nguo (fundi cherehani)
Muendelezo...... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 5 Part 10: Ndoa ya binti mfalme na Sinbad
Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza muendelezo...... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 26: Kaka wa tano wa kinyozi
Muendelezo.... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 6 Part 4: Kilema mtanashati asiye na mkono
Muendelezo wa hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha pili..... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 5 Part 16: Hadithi ya safari ya saba ya Sinbad
Muendelezo wa safari ya Sinbad....... Soma Zaidi...

Simulizi za Hadithi EP 5 Part 14: Hadithi ya kifo cha kujionea
Hadithi za HALIF LELA U LELA kitabu cha kwanza Muendelezo wa safari ya Sinbad Soma Zaidi...