HADITHI YA CHONGO WA PILI MTOTO WA MFALME

Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA CHONGO WA PILI MTOTO WA MFALME.

HADITHI YA CHONGO WA PILI MTOTO WA MFALME


Download kitabu Hiki Bofya hapa

HADITHI YA CHONGO WA PILI MTOTO WA MFALME.

Kwanza utambuwe kuwa mimi nimekuwa chongo si kwa sababu ya ajali ama bahatimbaya kama iliyompata mwenzangu huyu. Mimi ni kwa sababu ya ujeuri wangu wa kutaka kujuwa mambo yasiyo nihusu. Hadithi yangu ni hii:-

Kama nilivyotangulia kusema mimi ni mtoto wa mfalme na ni wa kipekee katika uzawa na baba yangu akanichagulia jina la Agib. Baba yangu alinipa taaluma nyingi sana. Ila kwa upand wangu nilipenda kuwa mfanya biashara. Hivyo nilikuwa nikisafiri kwa kufanya biashara maeneo mengi ya dinia. Tulikuwa tukiuza vitu mabalimbali. Kwa ufupi nilikuwa nimejaaliwa kwa kuwa na nuru ya biashara. Nilikuwa nikiuza sana na kupata faida nzuri.

Siku moja tulikuwa tumetoka kibiashara kwa njia ya majini. Nahodha alikuwa mjuzi sana wa safari hizi na safari yetu ilikuwa nzuri sana. Tulifanya biahsra katika visiwa kadhaa na kuelekea upande wa kusini kutoka kisiwa tulichotoka. Upepo ulikuwa mzuri kwa muda wa siku nzima. Hali ilibadilika pale ilipofika asubuhi. Upepo ulikuwa mbaya sana na chombo kilikuwa ninakwenda uelekeo usiojulikana. Nahodha na wenzie walijitahidi kutuwa nanga lakini kamba ilikuwa fupi. Basi wakakiachia chombo kiende tu.

Ilipofika asubuhi nyingine tupepo ulitulia na tukaona mbele kuna mlima uliotanda kiza kinene sana. Nahodha alipoulizwa alisema hana ujuzi na eneo hilo lakini anachoweza kusema ni kuwa mlima uliopo mbele yetu ni mlaima wa sumaku hivyo misumari yote iliyopo kwenye chombo chetu itatoka na kuvutwa kwenye mlima. Hivyo nahodha akatutaka kila mmoja ajiandae na ajali hiyo.

Mambo yalikuwa hivyo hivyo baada ya muda kadhaa misukari ikaanza kungโ€™oka na kwenda kunata kwenye mlima. Jabir tukaanza kungโ€™angโ€™ania mbao. Kwa upande wangu mbao nilioipata ilikuwa ni madhubuti hivyo niliogelea naye kwa muda wa siku kadhaa. Mapaka siku ya 5 nikaona kuna kisiwa kidogo. Nikajitahidi nai kufika pale nikaona kuna mti wa mpera nikafika hini pale na kuanza kula mapera.

Nilikaa pale kwenye mti ule kwa muda mpaka nikapitiwa na usingizi. Nilipoamka nikaona kuna msafara mkubwa sana unakuja kuelekea pale nilipo. Nikapanda juu ya mpera ule na kujificha pale. Msafara ule ukaja mpaka pembeni kidogo ya mpera ule kwa futi 50 wakachimba chini na kufungua mlango pale chini na msafara wote ukaingia pale. Baada ya muda wa masaa kama matatu walitoka wote kasoro mtu mmoja tu ndiye aliyebaki mule ndani.

Walipoondoka nilisubiri kama masaa 2 nikafungua pale na kuingia ndani. Nilipofika nikamkuta kijana wa umri wa miaka 10 ivi. Nikamsalimu na kumuuliza kilichomsibu hata wenzake wakamuacha mulendani. Akaanza kunieleza stori yake kama ifuatavyo;-


                   

Jiunge nasi WhatsApp kupata update zetu

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Aliflela1 Main: Burudani File: Download PDF Views 710

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 Madrasa kiganjani    ๐Ÿ‘‰2 Bongolite - Game zone - Play free game    ๐Ÿ‘‰3 Kitabu cha Afya    ๐Ÿ‘‰4 Simulizi za Hadithi Audio    ๐Ÿ‘‰5 kitabu cha Simulizi    ๐Ÿ‘‰6 Kitau cha Fiqh   

Post zinazofanana:

Safari ya majibu juu ya maswali mawili

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...
HADITHI YA KINYOZI MSIRI WA MFALME

Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA KINYOZI MSIRI WA MFALME.

Soma Zaidi...
Kutokana nyani mpaka kuwa chongo

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...
Hadithi ya mzee wa kwanza na mbuzi wake

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...
Alif lela u lela 1

Alif lela u lela ni hadithi zilizosheheni utamu na machungu pamoja na visa vya wachawi na majinim soma sasa.

Soma Zaidi...
Kisiwa cha uokozi

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi za safari saba za Sinbad

Soma Zaidi...
MALIPO YA WEMA NI WEMA

Download kitabu Hiki Bofya hapa MALIPO YA WEMA NI WEMA Basi baada ya kupita kwa muda Zubeidaha akapewa chai na chakula safi na akawekwa kwenye kiti kilicho kizuri na akaambiwa msubiri atakuja sasa hivi.

Soma Zaidi...
Hadithi ya mzee wa tatu na mbwa wake mwekundu

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...
NDOTO YA MGONJWA MTOTO WA MFALME

Download kitabu Hiki Bofya hapa NDOTO YA MGONJWA BINTI WA MFALME.

Soma Zaidi...
Hadithi ya tabibu wa mfalme

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...