Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela
HADITHI YA TABIBU WA MFALME
Katika nchi ya Zouman iliyopo maeneo ya uajemi alikuwepo mfalme mkubwa sana. Mfalme huya alipenda kusoma na kucheza mpira wa farasi, alimwamini sana waziri wake. Mfalme huyu alikuwa na ugonjwa ambao matatibu wengi walijitahidi lakini walishindwa. Kila tabibu mzuri katika nchi yake alijaribu bila ya mafanikio. Mfalme alikata tamaa ya kupon augonjwa wake.
Ilitokea katika nchi ile kuna tabibu ambaye ni mjuzi sana lakini hakutambuwa kama mfalme ana tatizo hilo. Tabibu huyu aliitwa Douban. Alipo[ata taarifa za ugnjwa wa mfalme alikusanya mavitabu yote na utabibu na kuanza kustadili kuhusu ugonjwa wa mfalme wake. Na hatimaye akafanikiwa kugunduwa dawa itakayomtibu mafalme. Dawa ambayo ingemtibu mfalme hata bila ya kumgusa.
Siku ilofata alivaa nguo zake safi za kitabibu na akaenda ikulu kuomba kumuona mfalme. Kwa kuwa alijitambulisha kama tabibuilikuwa ni rahisi kwake kumuona mfalme. Alipiga magoti na kumueleza mfalme kilicho mleta. “nina dawa ya kutibu maradhi yako hata bila ya kukugusa kwa uwezo wa Allah” ni tabibu akimwambia mfalme. “ukitibu maradhi nilonayo nitakufanya tajiri na utakuwa ni katika watu wangu wa karibu” kwa furaha mfalme akimwambia tabibu Douban. “Ndio mkuu tutaanza tiba yetu kesho IN shaa Allah” ni maneno aliyoyasema tabibu.
Siku hiyo tabibu alivaa safi mavari yake na kuiweka dawa yake tayari kwa ajili ya kumtibu mfalme. Aliiweka dawa yake kwenye fimbo ya kuchezea mpira wa farasi. Kisha akamwambia mfalme atumie fimbo ile kuchezea mpira wa farasi na apige kwa nguvu mpaka jasho limtoke. Mambo yaka wa kama hivyo na mechi ikaanza. Mfalme alicheza kwa uwezo wake wote na akawa anapiga mpira kwa fimbo yenyedawa. Kila anapopiga ndio dawa inavyiongia kutoka kwenye fimbo kuingia mwilini mwake. Mechi ilipoisha akamwambia mfalme akifika nyumbani kwake aoge kisha alale. Mfalme alifanya vivyohivyo na alipoamka ailikuwa ni asubuhi. Alistaajabu kuona ampona kabisa maradhi yake.
Aliagiza tabibu Douban aletwe mbele yake ili amlippe alichomwahidi. Mambo yakawa vivyo hivyo aliletwa tabibu na kutoa heshima kwa mfalme. Mfalme alifurahi na kumpa utajiri yeye na familia yake. Tabibu Douban akawa ni katika watu wa karibu na mfalme. Baadhi ya viongozi wa nchi walimonelea wivi tabibu. Waziri mkuu alikuwa ni muhanga wa jambo hili. Alikuwa akikasirika sana kumuona tabibu na mfalme. Hakupenda ukaribu wao na alitafura mbinu na njama mbalimbali kuweza kuwatenganisha.
Sikumoja kaamuwa kutekeleza mpango wake, alimfata mfalme na akamweleza kuwa amegunduwa kuwa huyu tabibu anataka kukuuwa. “kama angetaka kuniuwa kwa nini amenitibu” ni swali la mfalme kwa waziri. “huenda ange kuuwa muda ule angejulikana, lakin sasa umemwamini muda si mrefu atatekeleza madhambi yake” waziri akimjibu mfalme. Mabishano haya yalichukuwa muda mfalme akimtetea tabibu na waziri akimkandamiza tabibu. Mwisho mfalme akamwambia tabibu “nakumbuka vizuri maneno ya waziri mfani alipomwambia mfalme Sinbad alipotaka kumkinga mwanae asiuliwe” . “ni maneno ganihayo ewe mfalme wangu” waziri akimuuliza mfalme kwa shauku. Mfalme akamjibu “alimwambia usiamini maneno ya mtu yeyote hata akiwa mkweo kisha akamsimulia hadithi hii”;
Je! umeipenda hii post?
Ndio Hapana Save post
Rajabu Tarehe 2024-05-10 14:53:23 Topic: Aliflela1 Main: Post File: Download PDF Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1100
Sponsored links
👉1 Kitabu cha Afya
👉2 Kitau cha Fiqh
👉3 Madrasa kiganjani
👉4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
👉5 Simulizi za Hadithi Audio
👉6 kitabu cha Simulizi
Safari ya kwanza ya sinbad
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad Soma Zaidi...
SAFARI YA NNE YA SINBAD
Download kitabu Hiki Bofya hapa SAFARI YA NNE YA SINBAD Basi ikafikia siku ya kuanza safari yangu ya nne ya kibiashara. Soma Zaidi...
NDOTO YA MGONJWA MTOTO WA MFALME
Download kitabu Hiki Bofya hapa NDOTO YA MGONJWA BINTI WA MFALME. Soma Zaidi...
Safari saba za sinbad
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za safari saba za Sinbad Soma Zaidi...
HADITHI YA SAMAKI WA RANGI NNE
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA SAMAKI WA RANGI NNE. Soma Zaidi...
Hadithi ya mwenye kutabiriwa mtoto wa tajiri
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...
HADITHI YA BINTI MWENYE KUFICHWA MTOTO WA MFALME
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA BINTI MWENYEKUFICHWA, MTOTO WA MFALME. Soma Zaidi...
HADITHI YA KISIWA CHA MAWE YANAYOLIA
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YAKISIWA CHA MAWE YANAYOLIA. Soma Zaidi...
Hadithi ya mzee wa tatu na mbwa wake mwekundu
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...
ALIF LELA U LELA: UTANGULIZI
ALIF LELA U LELA. Soma Zaidi...
HADITHI YA BINTI WA KWANZA NA MBWA
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA BINTI WA KWANZA NA MBWA. Soma Zaidi...
HADITHI YA CHONGO WA TATU MTOTO WA MFALME
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA CHONGO WA TATU MTOTO WA MFALME Mimi ni mtoto wa mfalme kama nilivyotangulia kusema na ni mtoto wa kipekee kwa baba na mama. Soma Zaidi...