Usaliti unaanza hapa

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

USALITI UNANZA HAPA

Baada ya kukaa pale siku moja nahodha akaamrisha chombo kiondoke pale na kurudi nyumbani. Ndugu zake na Zubeidah kumbwe hawakupendezwa na mafanikio ya ndugu yao. Hali hii iliwafanya kuwa na wifu na kijicho. Basi zubeidah akaongea na ndugu zake na kuwapa mali zile zote na kuwambia mimi shida yangu ni kufika salama na huyu kijana ambaye kwa sasa ni mchumba wangu na tutaoana punde tu tufikapo nyumbani. Mali zile wakagawana ndugu wawili hawa.

 

Hili pia halikutosha wakataka na wawaue kabisa, na kawafanya hivyo katika majira ya usiku. Waliwachukuwa wawili hawa na kuwatia baharini. Anakuja kushituka zubeida yupo baharini anakunywa maji ya chumvi na hatimaye kupoteza fahamu na asijue nini kiliendelea. Basi kwa furaha ndugu wale wakaanza kugawana tena mali zile.

 

Kwa upande wa Zubeidah alopokuja kupata fahamu ilikuwa ni wakati wa jioni na akajikuta amezungukwa na kundi la wananwke wenye sura nzuri za kuvutia waliojipamba vizuri sana. Mbele yake kuna kiti kirefu sana kilichopamba na magodoro yaliyochovywa kwenye dhahabu nyekundu. Miguu ya kiti hicho ni meno ya tembo yaliyopambwa vizuri. Kwa hakika kiti hicho kilikuwa na kila aina ya mapambo mazuri. Aliponyanyua kichwa akaona amekaa juu ya kiti hicho mzee wa heshima mwenye ndevu ndefu zilizo kaa vyema.

 

Zubeida kwa mshangao alionekana kufurahia mazingira yale na asijuwe nini kinaendelea. Alikuja msichana wa makamo hivi aliyependeza sana na akampaka maji ya marashi yaliyochanganywa na misk na kutiwa manukato mazuri sana. Zubeidah akarudisha kumbulkumnbu zake zote na akajuwa kwa mara ya mwisho alitumbukia kwenye maji sasa akawa anajiulia yupo wapi?. Yule mzee akamwambia “mwanangu furahia uwepo wako hapa kwa hakika hupo peponi wala kuzimu, hapa upo chini ya bahari na mbele yako ni mfalme mkuu wa majini yaendayo baharini na nchi kavu. Mzee yule akaagiza kuwa Zubeidah afanyiwe kila kinachostahiki kufanyiwa kisaha akatoweka.

 

Kwa shauku Zubeida alikuwa na maswali mengi sana, wakaja mabinti watatu waliokuwa na sura nzuri sana hata Zubeidah akajiona yeye si lolote wala si chochote, wakamchukuwa na kwenda nae bafunu. Huko maji yaliyo na umoto kwa mbali yalikwisha andaliwa. Kwa mara ya kwanza Zubeidaha anakwenda kuoga maji yaliyotiwa marashi pamoja na misk nyekundu, manukato mablimbali yenye kuvutia. Zubeidah alijihisi yupo ulimwengu wa raha. Kwa maringo na madaha wakamvua ngu Zubeidah na kumtumbukiza kwenye bafu lile na kuanza kumsuguwa.

 

Wakaendelea kumsuguwa kwa visugulio vyenye rangi ya silva vilivyochovywa kwenye marjani. Kwakweli utasema mwili wa Zubeidah umekuwa lulu iliyohifadhiwa vizuri. Uchafu wote mwilini mwa Zubeidah uliondoka hata akawa kama akawa kama aliyofanyiwa scrub na kumbakisha kama mtoto alozaliwa. Ngozi laini na nyusi za kupendeza. Hawakuishia hapo wakaendelea kumpmba na kumpaka manukato. Nguo safi za hariri zenye mapindo yalochovywa kwenye dhahabu, hakika siwezi kuelezea zaidi urembo walomchaguli a

Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya link hapo chini kuweza kuipakua.

Download Now Bongoclass

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Aliflela1 Main: Burudani File: Download PDF Views 1563

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
👉1 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    👉2 Kitabu cha Afya    👉3 Madrasa kiganjani    👉4 Kitau cha Fiqh    👉5 Simulizi za Hadithi Audio    👉6 Bongolite - Game zone - Play free game   

Post zinazofanana:

SAMAKI WA AJABU

Download kitabu Hiki Bofya hapa SAMAKI WA AJABU Walikwenda upane wa magharibu na mji wakauacha upande wa kusini.

Soma Zaidi...
Wanyama ambao hutolewa zaka

(ii) Wanyama wafugwao kwa ajili ya chakula Wanyama wafugwao wanaotolewa Zakat ni ngamia, ngo’ombe, mbuzi na kondoo.

Soma Zaidi...
HADITHI YA MKE NA KASUKU

Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA MKE NA KASUKU.

Soma Zaidi...
Safari ya nne ya Sinbad

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad

Soma Zaidi...
KIAPO CHA SULTANI

Download kitabu Hiki Bofya hapa KIAPO CHA SULTANI.

Soma Zaidi...
Kitabu Cha Hadithi ya kifo cha Damu

Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet.

Soma Zaidi...
Safari ya pili ya Sinbad

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad

Soma Zaidi...
Hadithi ya mzee wa kwanza na mbuzi wake

Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela

Soma Zaidi...