Home Afya Shule ICT Burudani Dini Maktaba Maswali Madrasa Apps Blog Legacy Login

SAFARI SABA ZA SINBAD


image


Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za safari saba za Sinbad


SAFARI SABA ZA SINBAD

Katika nchi ya Baghdad kulikuwepo na kijana aliyejulikana kama Sinbad mbeba mizigo. Kijana huyu alijaaliwa kuwa na uwezo mkubwa wa nguvu za kuweza kubeba mizgo. Pia alikuwa na uwezo mzuri wa kiakili. Sinbad aliipenda sana kazi yake pia watu walimpenda kwa kuwa alikuwa akifanya kazi zake kwa umakini.

 

Ilitokea sikumoja alipokuwa katika kituo chake cha kufanyia kazi alikuwa mtu mmoja asiyemfahamu kabisa na kumpa kazi ya kupeleka mzigo wake sehemu husika. Mtu yule alitoweka baada ya kutoa maelekezo na kumpatia pesa yake. Sinbad baada ya kupewa maelekezo aliuchukuwa ule mzigo na kuanza kuukokota kwenye mkokoteni wake kuupeleka alikoelekezwa.

 

Njiani Sinbad alikutana na geti liliozungukwa na mauwa mazuri yenye kuvutia ndege, wadudu na wanyama kwa harufu na utamu wake. Sinbad alisimama kidogo eneo hili ili apate kushangaa uzuri ulioje wa eneo hili. Akilini alijiambia kuwa bila shaka ndani ya eneo hili kuna nyumba kubwa yenye bosi mkubwa.

 

Sinbad akiwa katika hali hiyo alituwa mzigo wake chini na kuanza kufuta jasho lake. Alisogea kidogo kwenye geti lile na kuona ndani kuna mambo ya kuvutia. Sinbad alikuwa ni kijana mwenye adabu na heshima lakini leo alisahau mambo yote hayo na akaanza kuchungulia ndani kwa watu. Alipokuwa hatoshelezi macho yake aliamua kuingia kwenye geti lile ili aone zaidi.

 

Sinbad hakuamini macho yake kama yanamuonesha sahihi, aliona nyumba kubwa yenye kila akijuacho kuwa kinahitajika, na aliona pia ambavyo havijui. Aliona nyumba iliyozungushiwa malumalu na lulu zikiwa zinaningi’inia kama mauwa mazuri yaliyopambwa. Rangi za nyumba utadhani ni dhahabu iliyochovywa. Kawahakika Sinbad alistaajabu sana. Kisha akaanza kuzungumza maneno yaloonesha kumalaumu mwenyezi Mungu kwa kuwapa watu wengine mali nyingi kama anazoziona pale. Pa aliendelea kumlaumu mwenyezi mungu kwa kumfanya yeye apate rizki kwa jasho jingi lakini watu wengine wapo wamekaa na bila jasho wanapata rizk.

 

Sinbad alilalamika sana hata akasikiwa na mwenye nyumba. Basi akaamrisha aletwe, akiwa natetemeka kwa woga Sinbad alipelekwa mbelel za Mkuu wa nyumba. Kisha akamwambia akae. Sinbad hakuamini kama meambiwa akae maana alifikiri atapewa adhabu kali. Basi mkuu wa nyumba akamuuliza “unaitwa nani kijana” “naitwa Sinbad “ au Sinbad mbeba mizigo. Yule mzee akamwambia jina zuri sana na inaonekana wewe ni wajina wangu. Mimi naitwa Sinbad au ukipenda niite Sinbad wa baharini.

 

Baada ya kutambulishana majina Sinbad wa baharini akaanza kumwambia Sinbad mbeba mizigo. “kijana nimekusikia maneno yako, ila sio kosa lako kusema maneno yale na wewe pia si wa kwanza. Kwani wapo wengi wamesema kama wewe. Sasa leo nataka nikueleze kuwa mimi sikupata mali zote hizi kwa kukaa hapa bila ya jasho. Kabla sijapata mali hizi nilipata tabu kubwa sana na pengine hakuna anayeweza kunifikia jasho na taabu nilizopata wakati natafuta malihizi”

 

Huu ni wakatii sasa wa mimi kula na kuulia kwani mchumia juani hula kivulini. Kabla ya hapo mimi nilikuwa ni mfanya biashara wa majini yaani nasafiri visiwa mbalimbali. Utajiri wote kuu umettoka na na taabu na mashaka yalonikuta. Nilisafiri safari SABA ambazo hizo nilipata taabu kubwa sana na sito sahau. Leo nitakueleza wewe na walokuwepo hapa yalonikuta kwenye safari hizo.”

 

Basi kabla hajaanza kusimulia Sinbad mbeba mizigo akamwambia Mkuu mimi nina mzigo wangu natakiwa niupeleke sehemu hivyo niruhusu niondoke. Palepale Sinbad wa baharini akamwambia nitakupa mtu umuelekeze apeleke yeye hiyo mizigo na nitakulipa pato la siku yako yote ila ukae na mimi leo upate kusikia hadithi saba za safari zangu saba. Basi palepale akamuagiza mtu apeleke mzigo ule na vinywaji na vyakula vialetwa. Watu wakakusanyika na kukaa tayari kusikiliza hadithi za safari saba za sinbad. Badi bila ya kuchelewa akaanza kusimulia hadithi ya safari zake kama ifuatavyo:-



Sponsored Posts


  πŸ‘‰    1 Magonjwa na afya       πŸ‘‰    2 ICT       πŸ‘‰    3 Jifunze fiqh       πŸ‘‰    4 Hadiythi za alif lela u lela       πŸ‘‰    5 Maktaba ya vitabu       πŸ‘‰    6 Mafunzo ya html kwa kiswahili    


Je! una maswali, mapendekezo ama maoni? tuma ujumbe wa meseji SMS hapo chini ili kuunganishwa na muhusika au bofya hapa

SMS SMS

Imeandikwa na Drsky Tags Burudani , simulizi , ALL , Tarehe 2021-11-08     Share On facebook or WhatsApp Topic school Zaidi Dini AFYA ICT Burudani Tags Uzazi maswali Afya mengineyo dini HIV Sira vyakula Matunda HTML php Alif Lela 1 Alif Lela 2 FANGASI Dawa SQL Tips Quran Sunnah fiqh DARSA Magonjwa Tajwid tawhid simulizi Dua Academy Wahenga chemshabongo WAJUWA Michezo ICT Imesomwa mara 1125



Post Nyingine


image Historia ya zamani
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi ya aladini na taa ya ajabu Soma Zaidi...

image Kisiwa cha uokozi
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa hadithi za safari saba za Sinbad Soma Zaidi...

image UFUPISHO WA ALIFU LELA ULELA KITABU CHA KWANZA
Posti hii inakwenda kukisimulia kuhusu hadithi za alifu lela ulela KITABU CHA KWANZA Soma Zaidi...

image Kukatwa mkono na kuurithi utajiri
Posti hii inakwenda kukupa muendelezo kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultani Soma Zaidi...

image NIMLAUMU NANI part 1
Post hii inahusu hadithi Moja ya kijana maaalufu aliyeitwa Frank, ni kijana aliyekuwa mwaminifu ila amekumbana na wasichana wengi wanamasaliti ukizingatia Frank alikuwa kijana mstaalabu na mwaminifu sana ila anafikia kufanya maamuzi magumu kufuatana na kusalitiwa mara kwa mara. Soma Zaidi...

image Binti huyu Ni Nani?
Posti hii inakwenda kukuendelezea hadithi kuhusu kifo cha mtoa burudani wa sultan Soma Zaidi...

image Kutokana kwenye kisima mpaka kuwa mfalme
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Hadithi ya chongo watatu wa mfalme na wanawake wa Baghdad
Posti hii inakwenda kukuletea hadithi za alifu lela ulela Soma Zaidi...

image Hadithi katika kijiji cha burugo
Β Posti hii inahusu zaidi jinsi ya watu walivyoishi katika kijiji cha burugo .tunajuwa hadithi ni sehemu mojawapo ya kubirudisha na kujifunza kitu flani kutoka kwenye jamii . Soma Zaidi...

image SAFARI YA MUUJIZA
Post hii inahusu hadithi moja iliyotokea Kwa mama mmoja mwenye familia ya watoto watano.ambapo mama aliolewa na mwanaume mwenye maambukizi ya virus vya ukimwi na kupata watoto bila maambukizi kusambaa kutoka Kwa baba kwenda Kwa mama. Soma Zaidi...