KISIWA CHA UOKOZI

KISIWA CHA UOKOZI

Download kitabu Hiki Bofya hapa KISIWA CHA UOKOZI Nikajisogeza vyema hata nikafika kwenye kivuli.

KISIWA CHA UOKOZI

pic
Download kitabu Hiki Bofya hapa

KISIWA CHA UOKOZI

Nikajisogeza vyema hata nikafika kwenye kivuli. Na kwa kuwa miguu yangu haikuwa na nguvu nilibuluzika tu. Nililala bila ya kijitambua niliamshwa na maji yaliyokuwa yakinipiga miguuni kumbe maji yalikuwa yanajaa. Haukupita muda ghafla nikaona kuna kijahazi kinaingia kikiwa kina mifugo kadhaa. Walipofika pale kisiwani wakawafungulia mifugo yao na kuanza kuwaosha na kuwapaka dawa. Mmoja wao akaenda mbali kidogo akaja na majani mengi sana na kuanza kuchagua baadhi ya ngโ€™ombe na kuanza kuwapa majani yale.

Niliwafuata na kuwaomba msaada wa chakula. Wakanipa maziwa na mkate wa nyama. Nilipomaliza kula wakaniuliza habari yangu na eneo lile na nikawaeleza kila kitu. Basi wakaniambia kama ungekuja kesho usingetukuta na pengine ungefia hapa maana hakuna majahazi yanayokuja hapa ila ni sisi tu na huchukuwa miezi 3 ndo tunakuja tena. Na kisiwa hiki hakina chakula, hivyo pengine ungeishia kufariki hapa. Basi wakanipatia na nguo na nikawauliza pia sababa ya wao kuja hapa na ni kinanani wao.

Mkubwa wao akanieleza kuwa wao ni watumishi wa mfalme aliyepo karibu na eneo hili. Mfalme huyo amekiteua kisiwa hiki kama eneo la kutibia mifugo yake na amepanda majani maalumu kama dawa ya mifugo yake. Hivyo eneo hili hawaruhusiwi watu wengine hapa. Basi walipomaliza shuhuli zao walifunganya mizigo yao na kuchukuwa majani mengi na nikaondoka pamoja nao.

Tulipofika kwenye utawala wao wakanipeleka kwa mfalme wao na nikamueleza mimi ni nani na nini kazi yangu na kumueleza kuwa natokea baghdada nchini kwa sultan Harun Rashid. Basi mfalme yule nikamueleza mengi kadir alivyouliza na mimi sikuwacha kuu;liza mambo kadhaa. Kwa haraka zaidi mfalme yule alionekana kunipenda sanan na kunikubali. Basi alinifanya katika watu wa karibu yake na ni kama mshauri pia. Niliishi pale nikawa nafanya biashara chini ya mfalme yaani nilikuwa naendeleza bishara za mtoto wake wa kike.

Siku moja niligundua kuwa kuna kisiwa jirani ambapo kunasikika sauti za furaha kila siku. Nilipouliza nikajibiwa kuwa ni kisiwa jirani huwa wannafanya sherehe kila wanaporudi kutoka kutafuta lulu. Hicho ni kisiwa pekee kinachofahamika kwa kuwa ni wafanyabiashara wa lulu. Basi kwa kuwa sikuijua lulu ilibidi niumuombe ruhusa mfalme ili na mimi nikashuhudie sherehe zao na nipate kuijua lulu. Mfalme alikubali na akanipa msafara wa wafanyakazi wake waende pamoja nami.

Tulipofika kule nilifurahi kuiona lulu kwa mara ya kwanza na nikafurahia pia sherehe zao. Basi katika hali kama zile nilishangaa kuona kuwa watu wanashusha mizigo kutoka bandarini lakini katika ile mizigo kuna ambayo imeandikwa Sinbad, nilipoangalia kwa uzuri nikagundua kuwa nahodha wa lile jahazi alikuwa ni yule nahodha wetu. Hivyo kumbe zile mali zilikuwa ni zakwangu na lile jahazi lilikuwa ni lile letu. Nikamuita kijana mmoja na nikamuuliza habari zao na akanieleza kuwa walibahatika kuliokoa jahazi lao na watu wote walipona isipokuwa Sinbad ndo hakuonekana. Kijana huyu alizungumza bila ya kunijuwa kama ndo mimi

Basi nikamfuata nahonda na kumueleza kuwa mimi ndo Sinbad na zile mali ni za kwangu. Basi nahonda alliponiona akanikumbuka na kutoa machozi kwa furaha maana walifahamu kuwa nimekufa. Nahodha akanikabidhi mali zangu na nikaziuza, nikapata habari kuwa jahazi letu litarudi Baghdad wiki ijayo. Nilichukua bidhaa zangu na kuuza baadhi na kurudi kwa mfalme na baadhi ya bidhaa. Nikamuelezea kilichotokea na alifurahi sana kwa kupata bidhaa zangu. Na hivi ndo Mwenyezi Mungu anavyowafanyia watu wenye subira.

Nikampatia mfalme bidhaa zilizobaki kama zawadi na nikamuomba ruhusa ya mimi kurudi nyumbani kwetu wiki ijayo. Kwa majonzi na kinyongo mfalme aliniruhusu na hata binti yake alikuwa na majonzi sana lakini haina budi โ€œmilima haikutani binadamu hukutanaโ€ ni maneno nilojisemea moyoni. Basi wiki ilipoisha mfalme alinipatia mali nyingi sana kama zawadi. Nilipata pia lulu kutoka kwenye kisiwa kile. Kwa hakika katika safari hii nilipata taabu na faida kubwasana.

Tulipofuka Baghdadi niliwaelezea ndugu zangu habari ya yalonikuta, kwakweli waliniambia niwachanena habari za biashara hii. Hata mimi nikajiapiza kwa yalonikuta kwa hakika sitarudia tena bishara hii. Basi nikatoa sadaka kutoka katika faida yangu na nikatoa na zaka muda ulipo fika. Nilitumia faida ile kujiendeleza kibiashara hata miezi mingi ikapiata. Nilisahau kabisa yalonikuta kwenye safari ile. Baada ya muda nahodha wetu wa mwanzo nilikutana nae, na katika mazungumzo yetu alinieleza kuwa wanatarajia kuanza safari wiki ijayo.

Kwa hakika nilivutiwa tena na biashara ile. Na kwa kuwa nilisahau machungu yalonikuta katika safari ya kwanza nikaazimia kuanza safari ya pili wiki ijayo. Mpaka kufikia hapa Sinbad kwa baharini akamaliza kusimulia hadithiya safari yake ya kwanza. Na kwa kuwa muda ulukuwa umekwenda hakuweza kuanza hadithi ya safari yake ya pili. Basi akampatia Sinbad mbeba mizigo zawadi nyingi na pesa kadhaa ya kutumia kama fidia ya kuvunja kazi zake. Na akamuahidi kesho awahi kuja maana safari ya pili ina mambo mengi na makubwa zaidi kuliko ya kwanza.


                   

Bongoclass
Download App Yetu

Jifunze zaidi, na wasiliana nasi ukiwa na App yetu. Bofya hapa chini kuipakua sasa!

Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

Nzuri            Mbaya            Save
Author: Rajabu image Tarehe: 1970-01-01 03:33:44 Topic: Aliflela1 Main: Burudani File: Download PDF Views 831

Share On:

Facebook WhatsApp
Sponsored links
๐Ÿ‘‰1 Madrasa kiganjani    ๐Ÿ‘‰2 Simulizi za Hadithi Audio    ๐Ÿ‘‰3 Bongolite - Game zone - Play free game    ๐Ÿ‘‰4 kitabu cha Simulizi    ๐Ÿ‘‰5 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)    ๐Ÿ‘‰6 Kitabu cha Afya   

Post zinazofanana:

Safari ya tano ya Sinbad
Safari ya tano ya Sinbad

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad

Soma Zaidi...
HADITHI YA MJI ULOGEUZWA MAWE
HADITHI YA MJI ULOGEUZWA MAWE

Download kitabu Hiki Bofya hapa HDITHI YA MJI ULOGEUZWA MAWE.

Soma Zaidi...
HADITHI YA MFALME NA WAZIRI WAKE
HADITHI YA MFALME NA WAZIRI WAKE

Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA MFALME NA WAZIRI WAKE Basi tambueni enyi rafikizangu kuwa mimi na waziri wangu huyu hatutokani na familia za kifalme wala mimi baba yangu hahusiani hata kidogo na ufalme.

Soma Zaidi...
MWANZO WA USALITI
MWANZO WA USALITI

Download kitabu Hiki Bofya hapa USALITI UNANZA HAPA Baada ya kukaa pale siku moja nahodha akaamrisha chombo kiondoke pale na kurudi nyumbani.

Soma Zaidi...
SAFARI YA TATU YA SINBAD
SAFARI YA TATU YA SINBAD

Download kitabu Hiki Bofya hapa SAFARI YA TATU YA SINBAD Siku ile ya pili Sinbad mbeba mizigo alivaa ngup zake safi alizonunua na kijipamba vyema na kuelekea kwenye kikao chao.

Soma Zaidi...
HADITHI YA SAMAKI WA RANGI NNE
HADITHI YA SAMAKI WA RANGI NNE

Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA SAMAKI WA RANGI NNE.

Soma Zaidi...
SAFARI YA MAJIBU JUU YA MASWALI MAWILI
SAFARI YA MAJIBU JUU YA MASWALI MAWILI

Download kitabu Hiki Bofya hapa SAFARI YA MAJIBU JUU YA MASWALI MAWILI.

Soma Zaidi...
MALIPO YA WEMA NI WEMA
MALIPO YA WEMA NI WEMA

Download kitabu Hiki Bofya hapa MALIPO YA WEMA NI WEMA Basi baada ya kupita kwa muda Zubeidaha akapewa chai na chakula safi na akawekwa kwenye kiti kilicho kizuri na akaambiwa msubiri atakuja sasa hivi.

Soma Zaidi...
KIAPO CHA SULTANI
KIAPO CHA SULTANI

Download kitabu Hiki Bofya hapa KIAPO CHA SULTANI.

Soma Zaidi...
Ndoa ya Sinbad na binti mfalme
Ndoa ya Sinbad na binti mfalme

Posti hii inakwenda kukupa muendelezo wa safari saba za Sinbad

Soma Zaidi...