Sifa za wanafiki zilizotajwa katika surat Al-Imran
Na kuwapambanua wale waliokuwa wanafiki.
Sifa za wanafiki zilizotajwa katika surat Al-Imran
Na kuwapambanua wale waliokuwa wanafiki. Nao waliambiwa: "Njooni mpigane katika njia ya Mwenyezi Mungu au mzuie (maadui pamoja na sisi)" Wakasema: "Tungejua kuwa kuna kupigana bila ya shaka tungelikufuateni." Wao siku ile walikuwa karibu na ukafiri kuliko na Uislamu (japokuwa siku zote wakidhihirisha Uislamu wa uwongo). Wanasema kwa midomo yao yasiyokuwa nyoyoni mwao. Na Mwenyezi Mungu anajua vyema (yote) wanayoyaficha. (3:167)
Wale waliosema juu ya ndugu zao - na (wao wenyewe) wamekataa kwenda (hawakwenda) vitani: "Wangalitutii wasingeuawa." Sema: "Jiondoleeni mauti (nyinyi) wenyewe msife maisha ikiwa mnasema kweli." (3:168)
"Wala usiwadhani wale waliouawa katika njia ya Mwenyezi Mungu kuwa ni wafu (maiti). Bali wahai, wanaruzukiwa kwa Mola wao." (3:169).
Kutokana na aya hizi tunapata sifa za wanafiki zifuatazo:
(i)Hawako tayari kujitoa muhanga kupigania dini ya Allah (s.w) isimame katika jamii au kuihami isiangushwe baada ya kusimama kwake.
(ii)Wanasema kwa midomo yao yasiyokuwa nyoyoni mwao. Baada ya mapambano dhidi ya maadui wa Dini ya Allah (s.w) kwisha, wanafiki hujikosha kwa kusema uwongo kuwa hawakuwa na taarifa juu ya mapambano ya Waislamu dhidi ya maadui zao, vinginevyo wangelikuwa Pamoja katika vita hivyo hali ya kuwa walijificha wasiende vitani kwa kuogopa kufa.
(iii)Huwabeza na kuwalaumu wale wanaouliwa au kupata misuko suko katika kuupigania Uislamu.
Katika aya ya 168 na 169 (3:168-1 69), Allah (s.w) anawasuta wanafiki na kuwakatisha tamaa kuwa mtu hafi kwa kuwa amepigania dini ya Allah (s.w), bali kila mtu atakufa kwa ajali yake aliyopangiwa:
โโฆ Sema: (uwaambia wanafiki): "Jiondosheeni mauti (nyinyi wenyewe msife milele) ikiwa mnasema kweli."
Pia Allah (s.w) anawakatisha tamaa wanafiki na kuwatumainisha waumini kuwa hapana jambo lililozuri na bora kwa mtu kuliko kufa katika njia ya Allah (s.w) (kufa shahidi).
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
๐1 Dua za Mitume na Manabii ๐2 kitabu cha Simulizi ๐3 Madrasa kiganjani ๐4 Simulizi za Hadithi Audio ๐5 ai web app ๐6 Kitabu cha Afya
Post zinazofanana:
Fadhila za kujenga msikiti
Kuna malipo makubwa kwa ambaye amejenga msikiti kwa ajili ya kuoatavradhi za Allah.
Soma Zaidi...Nani Muadilifu na zipi sifa za mtu muadilifu kwenye uislamu
Uadilifu ni usimamiziย wa ukweli na kutoaย hakiย kwa kila anayestahikiย kulingana na ukweli.
Soma Zaidi...Umbwaji wa mwanadamu kutoka Nutfa (tone la mbegu za uzazi), alaqah (tone la damu, mudgha (pande la nyama) na kuwa mtu kamili
ุนููู ุฃูุจูู ุนูุจูุฏู ุงูุฑููุญูู ููู ุนูุจูุฏู ุงูููููู ุจููู ู ูุณูุนููุฏู ุฑูุถููู ุงูููู ุนููููู ููุงูู: ุญูุฏููุซูููุง ุฑูุณูููู ุงูููููู ุตูู ุงููู ุนููู ู ุณูู ...
Soma Zaidi...jamii somo la 35
Hutekeleza ahadi zao wanapoahidiana na wanaadamu wenziwao maadamu ni katika mipaka ya Allah (s.
Soma Zaidi...