v

Na tumemuusia mwanaadamu afanye wema kwa wazazi wake.

v

Maadili katika surat Al-Ahqaf


Na tumemuusia mwanaadamu afanye wema kwa wazazi wake. Mama yake amechukua mimba yake kwa taabu na akamza kwa taabu. Na kubeba mimba yake hata kumwachisha ziwa; (uchache wake) ni miezi thelathini. Hata anapofikia baleghe yake na akawa mwenye umri wa miaka arubaini, (mtoto mwema) husema: "Ee Mola wangu! Niwezeshe nishukuru neema zako ulizonineemesha mimi na wazazi wangu, na niwezeshe nifanye vitendo vizuri unavyovipenda, na unitengenezee watoto wangu; kwa yakini ninatubu kwako; na hakika mimi ni miongoni mwa waliosilimu (walionyenyekea)." (46:15).


Hao ndio tunaowakubalia vitendo vyao vyema walivyovifanya, na tunayapita kando makosa yao, (tunayasamehe); (watakuwa) miongoni mwa watu wa Peponi: miadi ya kweli waliyoahidiwa. (4 6:16).



Na ambaye anawaambia wazazi wake: "Kefule nyi! Oh! Mnanitishia kuwa nitafufuliwa; na hali karne nyingi, (watu wengi) zimekwisha pita kabla yangu (wala hazikufufuliwa)?" Na hao (wazee wake) wawili huomba msaada wa Mwenyezi Mungu; (na humwambia mtoto wao:) "Ole wako! Amin (haya unayoambiwa). Hakika ahadi ya Mwenyezi Mungu ni kweli." Lakini yeye husema: "Hayakuwa haya (mnayoyasema) ila ni visa vya watu wa kale (tu si maneno ya kweli)."



Hao ndio ambao imelazimika hukumu juu yao (ya kutiwa Motoni, pamoja na mataifa yaliyopita kabla yao ya majini na watu, hakika hao ndio waliojitia khasarani. (46:17-18)
Kutokana na aya hizi tunajifunza kuwa:



(a)Hatunabudi kuwafanyia wema wazazi wawili na hasa mama ambaye anapata dhiki kubwa katika kutuzaa na kutunyonyesha mpaka kufikia umri wa miaka miwili.



(b)Hatunabudi kumshukuru Allah (s.w) kwa kutuneemesha kwa neema mbali mbali ikiwa ni pamoja na kuwapa wazazi wetu moyo wa huruma na mapenzi ya kutulea mpaka kufikia utu uzima.



(c)Pamoja na kumshukuru Allah (s.w), hatubabudi kuwashukuru wazazi wetu kwa kutulea kwa huruma na mapenzi. Shukrani zetu kwao tutazidhihirisha kwa kuwatii, kuwafanyia ihsani na kuwaombea dua na maghfira kwa Allah (s.w).


(d)Hatuna budi kujiepusha mbali na kuwafanyia wazazi wetu ufedhuli na jeuri. Tusisubutu hata kuwagunia.



(e)Hatunabudi kuomba kizazi chema na kumuomba Allah (s.w) atuwezeshe kukilea vyema kizazi chetu.



(f)Hatunabudi kufuatilia kwa makini usia mwema wanaotupa wazazi wetu.



(g)Hatunabudi kuleta toba na kuomba maghfira mara kwa mara (angalau kila siku mara mia moja).




                   


Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 185

Post zifazofanana:-

UTARATIBU WA KULEA MIMBA
Soma Zaidi...

VYAKULA VYA MADINI
Pata elimu juu ya afya hapa ukiwa na vitabu vyetu bila ya malipo yoyote Soma Zaidi...

tarekh
Soma Zaidi...

Ghasia na chokochoko za Makhawariji na kuuliwa kwa Ally
Soma Zaidi...

Ni mambo gani yanaharibu na kutengua udhu?
Soma Zaidi...

HADITHI YA BINTI WA KWANZA NA MBWA
Download kitabu Hiki Bofya hapa HADITHI YA BINTI WA KWANZA NA MBWA. Soma Zaidi...

Madai ya Makafiri dhidi ya kuwepo kwa Allah (s.w) na Udhaifu wa Madai hayo.
2. Soma Zaidi...

maswali na majibu kuusu Afya, teknolojia na dini
Soma Zaidi...

Chemsha bongo namba 12
8. Soma Zaidi...

Haki na wajibu kwa masikini, mafukara na wasio jiweza
Soma Zaidi...

Historia ya Luqman mtu aliyesifika kuwa na Hikma
Luqman ni katika watu wema kabisa waliopita zama za nyuma. Soma Zaidi...

Penzi la Mitihani
MTIHANI PENZINI Sikuwa na wasiwasi maana niliamini kuwa nitafanikiwa tu. Soma Zaidi...