Kuwa wenye shukurani mbele ya Allah (s.w)

Kuwa wenye shukurani mbele ya Allah (s.w)

Mwanaadamu ametunukiwa neema mbali mbali na Mola wake kuliko viumbe wengine wote kama tuanvyojifunza katika aya mbali mbali za Qur'an.

Kuwa wenye shukurani mbele ya Allah (s.w)

(a) Kuwa wenye shukurani mbele ya Allah (s.w)



Mwanaadamu ametunukiwa neema mbali mbali na Mola wake kuliko viumbe wengine wote kama tuanvyojifunza katika aya mbali mbali za Qur'an.


"Na hakika tumewatukuza wanaadamu na tumewapa vya kupanda barani na baharini, na tumewaruzuku vitu vizuri vizuri, na tumewatukuza kuliko wengi katika wale tuliowaumba, kwa utukufu ulio mkubwa (kabisa)." (17: 70)


β€œBila shaka tumemuumba mwanaadamu kwa umbo lililo bora kabisa." (95:4) Pamoja na neema zilizoainishwa kwa upeo mpana katika aya (17:70),


Mwanaadamu ameboreshwa kuliko viumbe wengine kwa kutunukiwa vipawa vya ziada vifuatavyo:



1. Akili inayomuwezesha kufikiri na kutafakari
2. Utambuzi wa ubinafsi unaomuwezesha kujitambua, kuyatambua mazingira yake na mahusiano yake na muumba na vile vyote Alivyoviumba
3. Kipawa cha elimu - uwezo wa kujielimisha na kuelimisha wengine.
4. Uhuru wa kuamua na kutenda.



Neema zote hizi ametunukiwa binaadamu ili aweze kufikia lengo la kuumbwa kwake ambalo ni kumuabudu Allah (s.w) katika kila kipengele cha maisha yake (Qur'an 51:56) na kisha kuwa Khalifa katika jamii. Hivyo, binaadamu atakuwa ni mwenye kumshukuru Allah (s.w) iwapo atamuabudu Allah (s.w) ipasavyo katika kila kipengele cha maisha yake na atakuwa ni mwizi wa fadhila endapo atatakabari na kuwaabudu wengine kinyume na Allah (s.w).



Anaye shukuru kwa kumuabudu Allah (s.w) ipasavyo anafanya hivyo kwa faida ya nafsi yake ya kuishi kwa furaha na amani katika maisha ya hapa duniani na kupata maisha bora zaidi huko akhera. Anayekufuru kwa kuacha kumuabudu Allah (s.w) iipasavyo, anaitia khasarani nafsi yake mwenyewe kwa kuishi maisha ya mashaka na khofu hapa duniani na kustahiki adhabu kali isiyo na mfano wake katika maisha ya akhera. Allah (s.w) hafaidiki kwa chochote kutokana na kushukuru kwetu na pia hapungu kiwi na chochote kutokana na kukufuru kwetu. Allah (s.w) ameliweka hili wazi mara tu baada ya kutufahamisha lengo la kuumbwa kwetu.


"Sikuwaumba majini na watu ila wapate kuniabudu. Sitaki kwao riziki wala Sitaki wanilishe. Kwa yakini Mwenyezi Mungu ndiye Mtoaji wa riziki, Mwenye nguvu, Madhubuti". (51:56-58).




                   


Zoezi la Maswali

Nyuma Endelea


Umeionaje Makala hii.. ?

       
Author: Rajabu Rajabu
Tarehe: 2024-05-10 14:53:23 Topic: Tawhid Main: Post File: Download PDF Views: 1727

Share On:

Share follows: 0 | Unique share links followed: 0
Sponsored links
πŸ‘‰1 ai web app     πŸ‘‰2 web hosting     πŸ‘‰3 Dua za Mitume na Manabii     πŸ‘‰4 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)     πŸ‘‰5 Bongolite - Game zone - Play free game     πŸ‘‰6 Kitau cha Fiqh    

Post zinazofanana:

Mtazamo wa Uislamu juu ya maana ya dini

Uislamu unaitazama dini katika nyanja zote za maisha ya mwanadamu. Hii ni tofauti na mtazamo wa kikafiri juu ya dini.

Soma Zaidi...
Elimu Yenye Manufaa

Kwenye kipengele hiki tutajifunza elimu yenye manufaa kwenye jamii na pia tutajifunza sifa za elimu yenye manufaa.

Soma Zaidi...
UMBILE LA MBINGU NA ARDHI

β€œKatika kuumbwa mbingu na ardhi na mfuatano wa usiku na mchana,ziko alama (hoja) za kuonyesha kuwepo Allah (s.

Soma Zaidi...
Kwa nini hakuna haja ya Mtume mwingine baada ya Muhammad

Na tukiutafiti Uislamu kwa makini kama mfumo kamili wa maisha tunaona unadhihiri ukweli wa aya hii ya Qur-an.

Soma Zaidi...