Maana ya Swala(a)KilughaKatika lugha ya Kiarabu neno “Swalaat” lina maana ya “ombi” au “dua”. Katika Qur-an tunaamrishwa kumswalia Mtume, yaani kumuombea dua Mtume (s.a.w) katika aya ifuatayo:


“Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake wanamswalia Mtume (w anamtakia Rehema). Basi, enyi mlioamini mswalieni (muombeeni au mtakieni Mtume) Rehema na muombeeni amani”. (33:56)Vile vile katika Hadith, Mtume (s.a.w) anatuambia:
“Yule atakayealikwa kwenye karamu ya harusi aitikie wito huo, kama hataweza kuitika amswalie (amuombee dua) aliyemkaribisha. ” (Muslimu)(b)KisheriaKatika sheria ya Kiislamu, “swalaat” ni maombi maalumu kwa Allah (s.w) yanayofanywa kwa kufuata utaratibu maalumu uliowekwa na Allah (s.w) na kufundishwa kwa matendo na Mtume wake. Katika maombi haya maalumu mwili mzima huhusika katika maombi haya kwa kusimama, kurukuu, kuitidali, kusujudu, kukaa na kuzingatia yale yote anayosema katika kuleta maombi haya.