Kumuandaa maiti punde baada ya kufariki dunia
Mambo Anayofanyiwa Mtu mara tu baada ya Kufa
Baada ya kushuhudia kuwa ndugu yetu ameshakata roho vyema tuseme na kuzingatia maneno yafuatayo kama alivyotufahamisha Allah (s.w)
β... Hakika sisi ni wa Allah na kwake tutarejea ...β (2:156).
Maneno haya ni ya msingi sana katika hali hii ya kufiwa, kwani yanawaliwaza wafiwa na kuwaepusha na fadhaa zinazoweza kutokea juu ya kifo cha marehemu. Ukizingatia maneno ya aya hii utaona kuwa kwa vyovyote iwavyo, kurejea kwa Allah ni jambo lisilozuilika. Hivyo, chochote kile kitakachokuwa ndio sababu ya kifo cha marehemu kitakuwa ni sababu tu ya kifo hicho aliyoiweka Allah (s.w)
Baada ya maliwazo haya maiti ile yapasa kufanyiwa yafuatayo:
1. Kwa taratibu rudishia mdomo usibakie wazi kwa kufunga kidevu kwa kitambaa na kukizungushia kichwani.
2. Funga macho ya marehemu kwa taratibu na huku ukisoma:
βKwa jina la Allah na kwa kufuata mila ya Mjumbe wa Allah. Ewe Mola wetu mrahisishie mambo yake ya sasa na msahilishie mambo yake baadaye. Na jaalia atakayokutana nayo yawe bora kuliko aliyoachana nayoβ.
3. Lainisha viungo vya maiti kwa kukunja na kukunjua pole pole sehemu zote zenye viungo katika mikono na miguu. Kama patakuwa na ugumu wowote katika kumnyoosha viungo hivyo, maji ya moto au mafuta yanaweza kutumika ili kulainisha. Baada ya kulainisha viungo, miguu na mikono inyooshwe na alazwe huku uso ukielekea Qibla kwenye kitanda kisichokuwa na godoro.
4. Maiti avuliwe nguo zote alizokufa nazo kisha kumgubikwa kwa shuka kubwa, pia ni vyema afungwe kitambaa tumboni au kuwekewa kitu chenye uzito kidogo juu ya tumbo ili lisifutuke sana.
5. Marashi na ubani vitumike sana mahali alipo maiti ili kuzima harufu ya uvundo itokayo kwa maiti.Mwanaadamu ni msafi sana anapokuwa hai. Lakini muda mfupi tu baada ya kufa huanza kutoa harufu kali ya uozo.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
π1 Tafasiri ya Riyadh Swalihina π2 Bongolite - Game zone - Play free game π3 Simulizi za Hadithi Audio π4 Kitau cha Fiqh π5 kitabu cha Simulizi π6 Sira ya Mtume Muhammad (s.a.w)
Post zinazofanana:
Taratibu za mahari katika uislamu
Hapa utajifunza taratibu za kutaja mahari katika uislamu.
Soma Zaidi...maana ya Eda na aina zake
Ni kipindi au muda wa kungojea mwanamke aliyepewa talaka (aliyeachwa) au kufiwa na mumewe kabla ya kuolewa na mume mwingine.
Soma Zaidi...maana ya uchumi kiislamu
Maana ya UchumiMfumo wa maisha wa Kiislamu humuelekeza binaadamu kujenga na kudumisha uhusiano wake na Al-lah (s.
Soma Zaidi...Jinsi ambavyo msafiri anatakiwa aswali akiwa safarini
Postvhiibinakwenda kukufundisha kuhusu swala ya msafiri na jinsi ya kuiswali.
Soma Zaidi...