Moja katika changamoto za ujauzito ni kupata maambukizi na mashambulizi ya UTI ya mara kwa mara. Bakteria ni rahisi kuingia kwenye mirija ya mkojo na kukifikia kibofu, haya kwa wajawazito ni rahisi sana kuliko ambao sio wajawazito. Tafiti zinaonyesha kuwa asilimia 18 ya wanawake wajawazito wanasumbuliwa na UTI.
Dalili za UTI
1.Maumivu wakati wa kukojoa na kuhisi kama unaungua
2.Kukojoa mara kwa mara
3.Mkojo kuwa na mawingi mawingu ama kuwa kama na damu
4.Maumivu ya kwenye nyonga
5.Maumivu ya mgongo sehemu ya chini
6.Homa
7.Kichefuchefu
Njia za kujikinga na UTI
A.Kojoa kila unapohisi mkojo
B.Kunywa maji mengi
C.Wacha kutumia viungo vya uke (kusafisha uke kwa kemikali, eti kufanya uke ukaze, msafi na wenye kuvutia)
D.Wacha kutumia sabuni kali sehemu za siri.