Unataka kujuwa sababu za mjamzito kutokwa na damu, utelezi ama majimaji kwenye uke wake. Na dalili gani zinaashiriwa na majimaji haya

Majimaji yanayotoka ukeni wakati wa ujauzito (Damu na uteute)
Ni kawaida kwa mjamzito kushuhudia kwenye uke wake kutokwa na kama uteute na huongezeka kila mimba inapoendelea kukomaa. Wakatiflani anaweza kuona nguo zake zina madoa ya damu, ama akashuhudia matone kadhaa ya damu. Wapo pia wanaingia hedhi kwa damu chache. Sasa hebu tuangalie kwa ufupi hali hizi:-
1.Baada ya kutoka hedhi uke wa mwanamke unakuwa mkavu bila ya kuwa na utelezi telezi. Hiki ni kipindi ambacho mwanamke hawezi kubeba ujauzito. Katika kipindi hiki hata akitia kidole hakitoki na utelezitelezi. Kipindi hiki kinaweza kuchukuwa takribani siki tano hadi 10 inategemea na mzunguruko wa mwanamke. Huu ni kuda mzuri wa kushiriki tendo kwa wale ambao hawahitaji kulea ujauzito.
2.Zitakapoanza kuingia siku hatari mwanamke ataanza kuhisi uwepo wa uteute kwenye uke wake anapotia kidole kwa ndani. Siku hizi pia zinatofautiana kulingana na idadi ya mzunguruko. Ila zinaweza kuazia siku ya 11 hadi 14 inaweza pia kuwa chini ya papo lwa baadhi ya wanawake ama juu ya hapo.
3.Siku moja kabla ya kukomaa kwa yai na kuwa tayari kwenye mirija ya falopian tayari kutungisha mimba, uteute huu huongezeka zaidi. Sifa za uteute huu ni kuwa ni wenye kuteleza sana ila sio mzito na wenye kunatanata ama kuvutikana. Kwa wanaotumia njia za uzazi wa mpango hasa zile za homoni uteute wao upo muda wowote kwa hiyo ni ngumu sana kwao kuiona hali hii.
4.Siku ya hatario zaidi mwanamke atapata mabadiliko ya hamu ya kutaka kushiriki tendo la ndoa. Yaani hamu itaongezeka zaidi siku hii kuliko siku iliyotangulia. Hapa kwa wale ambao hawataki ujauzito sio siku salama kwao kushiriki tendo landoa.
5.Uteute huu katika siku hizi kuandaliwa kwa ajili ya kusaidia mbegu za kiume ziweze kusafiri vyema, kuogelea vyema na kulifikia yai. Pia kuhakikisha kuwa mbegu za kiume haziathiriwi na asidi ya tumboni kwa mama kwa kiasi kikubwa. Hivyo uteute huu katika kipindi hiki ni muhimu sana.
6.Kali hii inaweza kudumu kwa masiku kadhaa toka 14 hadi 17 kwa makadirio inaweza kupungua ama kuongezeka kulingana na mzunguruko wa mwanamke. Baada ya hapo kama mwanamke alibeba ujauzito majimaji haya yanaongezeka uzito saa na kuwa yenye kunata na kufanana na utelezi wa yai pindi unapolibanja. Baada ya mimba majimaji haya yataendelea kutoka na kuongezeka na kuwa mazito zaidi hadi atakapojifungua.
Katika ujauzito majimaji haya yanakazi ya kulinda njia ya kuingilia kwenye mji wa mimba dhidi ya mashambulizi na aambukizi ya bakteria. Yaani kuhakikisha kuwa hakuba bakteria ama fangasi atakayeweza kuingia na kumzuru mtoto tumboni.
7.Kama hakuna ujauzito uliobebwa majimaji yataanza kurudi kutoka hali yake ya kawaida na kuwa safi, yenye harufu kwa mbali ila si harufu ya kukera, pia yanaweza kuwa na rangi ya maziwa hivi.
Majimaji haya pia nayaweza kuashiria shida kwenye afya endapo yatakuwa na sifa hizi:-
A.Yana rangi ya njao, kijani ama buluu
B.Yana harufu kali mbaya
C.Yanakusababishia muwasho kwenye uke na mashavu ya uke
D.Yanakusababishia kuvimba kwa uke na mashavu ya uke
8.Ama kuhusu kutokwa na damu, ikiwa chache ni kawaida. Ikiwa unaambatana na maumivu makali ya tumbo, ama maumivi makali ya kichwa na homa, basi vyema kumuona daktari kwa ushauri zaidi. Kama nilivtotangulia kusema kuna wanawake wanapata hedhi wakiwa wajawazito. Wenyewe wanaita kupunguzia, kwa ufupi hii si hedhi na pia haiashirii kama kuna tatizo. Ila kama inatoka nyingi na kuambatana na maumivu yasiyo ya kawaida ni vyema kumuona daktari.
Umeionaje Makala hii.. ?
Share On:
Maumivu ya tumbo baada ya tendo la ndoa yanaweza kuwa ni dalili ya maradhi fulani, ama shida kwenye mfumo w uzazi. PID na UTI hutuhumiwa kuwa ni katika sababu hizo. Ila zipo nyingine nyingi tu. Kama ina hali hii vyema ukafika kituo cha afya
Soma Zaidi...Post hii inahusu zaidi kazi za homoni katika Mzunguko wa hedhi, katika kipindi hiki kuna homoni mbalimbali ambazo ufanya kazi kama tutakavyoona.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi dalili ambazo mwanamke hapaswi kufumbia macho.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi njia za uzazi wa mpango unavyofanya na mwanaume kushiriki, ni njia ambayo umfanye mwanaume awe mhusika hasa wakati wa kujamiiana.
Soma Zaidi...Jifunze sababu kuu zinazosababisha kuhisi maumivu makali ya tumbo wakati wa kushiriki tendo la ndoa
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu mbalimbali ambazo zinamfanya mama au dada kutobeba mimba. Kwa hiyo tutaziona hapo chini kama ifuatavyo.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu zaidi sababu za kupasuka kwa mfuko wa uzazi hasa mama anapokalibia kujifungua.
Soma Zaidi...Mtoto huweza kuzaliwa ndani ya miezi 6 na unaweza kupona. Na huyu mdoe mtoto njiti. Na anaweza kuzliwa kwa njia ya kawaida. Hakuna ushahidi unaiinyesha kuwa njiti hukabiliwanamatatizo ya kitalima kwenye ukubwa wako.
Soma Zaidi...Kuzaliwa kabla ya wakati humpa mtoto muda mdogo wa kukua tumboni. Watoto waliozaliwa kabla ya wakati, hasa wale waliozaliwa mapema, mara nyingi huwa na matatizo magumu ya matibabu.
Soma Zaidi...Posti hii inahusu namna unavyoweza kumtambua mtoto mwenye Ugonjwa wa Nimonia na tiba anayopaswa kupata mtoto mwenye Nimonia
Soma Zaidi...