Nia za kupima ujauzito ukiwa nyumbani, Njia kuu 10 za kiasili za kupima mimba changa

Kuna njia nyingi zinatajwa zinapima mimba kama chumvi, sukari, mafuta na sabuni. Hata hivyo zipo njia zaidi ya 10 za kiasili za kupima ujauzito. Utajifunza hapa zote

Nia za kupima ujauzito ukiwa nyumbani, Njia kuu 10 za kiasili za kupima mimba changa



JE NAWEZA UPIMA UJAUZITO KWA KUTUMIA CHUMVI NA SUKARI?




Haswa hili ni swali zuri, wanawake wengi wamekuwa wakitafuta makala hizi na wanazipata. Namna ya kupima ujauzito kwa kutumia sukari ama chumvi. Ila nikwambie kitu si sukari na chumvi tu balli zipo njia nyingine kama:-



Njia nyingine za kupima ujauzito ukiwa nymbani:-
1.Sukari
2.Chumvi
3.Sabuni
4.Mafuta
5.Delto
6.Shampoo
7.Dawa ya mswaki na yingine.



Nini kinafanyika. Unachanganya kiasi cha mkojo vyema ukawa wa asubuhi. Unaandaa chombo na kuweka moja kati ya hizo zilizotajwa juu. Unaweza kutumia kijiko kimoja kcha mkojo ama kikombe. Uwiyano wa vilivyotaja juu uwe zawa na mkojo, ama mkojo uziti kidogo. Kisha subiria kwa dakika 5 hadi 10. kama utaona mabadiliko yeyote ya rangi yametokea ama utaona kuna mapovu yanachemka basi takuwa ni mjamzito.



Je nji hizi ni sahihi?
Kwa ufupi njia hizi si sahihi kabisa. Haziwezi kukupa majibu ya kweli. Waandishi wengi wameandika lakini ukweli ni kuwa huu ni uwongo. Njia sahihi ni kwenda kupima kwa kipimo maalumu, vinginevyo utapoteza muda bure. Yes wakati mwingine unaweza kupima ukaona mabadiliko na ukawa ni mjamzito kweli. Lakini mabadiliko hayohayo utakayoyaona anaweza kuyaona hata asiye mjamzito.



Je watu wa zamani walikuwa wanapimaje ujauzito?





NJIA ZA KIASILI WALIZOTUMIA ZAMANI KUPIMA UJAUZITO:



1.Kukojoa kwenye nafaka (mbegu za ngano na shayiri)
Tafiti zilizofnywa na wavumbuzi wa mabo ya kale (archeologist) wamegunduwa kuwa yapata miaka 1350 KK kabla ya kuzaliwa Yesu kuwa wanawake wa Misri (Egypt) walikuwa wanapotaka kujuwa kama wamebeba ujauzito walikuwa wakichukuwa viroba vya ngano na shayiri (barley) kisha wanakojolea kiroba chote. Kama ngano itaota basi mwanamke ana ujauziti tena wa mtoto wa kike. Na kama shayiri itaota atakuwa na ujauzito wa mtoto wa kiume. Na kama nafaka hizi hazitaota basi mwanamke hana ujauzito.



Ni kuwa katika mwanamke mjamzito kwenye mojo wake kuna homoni ambazo zinachochea ukuwaji wa mbegu. Baada ya kukojolea pishori lile mbegu hazifukiwi, hivyo ztaota mulemule kwenye kiroba kile bila ya kufukiwa kwenye udogo. Miaka ya 1960 wanasayanzi wa leo walifanya tafiti wakagunduwa kuwa njia hii ni sahihi ya asilimoa 70%.



2.Kitunguu.
Njia hii ilifanywa na wagiriki mikaa ya zamani sana. Matabibu wa kigiriki walikuwa wanapotaka kujuwa kama mwanmke ana ujauzito walikuwa wakiinguiza kwenye uke wa mwanamke kitunguu na kukiacha humo kwa usiku mzima. Na kama ikifika asubuhi mwanamke akawa anatowa harufu ya kitunguu kwenye mdomo wake basi ana ujauzito. Wagiriki waliamini kuwa mwanamke akiwa na ujauzito uke wake unauwezo mkubwa wa kufyonza vitu. Tafiti hii haikuweza kuthibitishwa na sayansi hili leo.



3.Kwa kutumia funguo ama kitasa.
Njia hii ilifanya kwa namna hii, endapo mwanamke anajihisi ni mjamzito alikuwa anachukuwa fnguo ama kitasa kisha anaweka kwenye bakuli kisha anakojowa kiasi cha mkojo kuzamisha funguo ama kitasa kisha anaacha hivyo kwa muda wa masaa matatu. Kama akitowa hakuna mabadiliko ya michubuko ama rangi ana chochote basi mwanamke ni mjamzito. Njia hii [ia haikuweza kuthibitishwa hivi leo.



4.Kwa kuangalia rangi ya macho.
Moja katika matabibu wa zamani sana wa kifaransa aliyetambulika kama Jacques Guillemeau yeye aliamini kuwa macho ndio kioo cha mwili, hivyo unaweza kujuwa maradhi na hali ya mwili wa kutumia macho. Aliamini kuwa mwanamke mjamzito macho yake yameingia ndani kidogo, mboni ya macho yake imesinyaa kidogo na mishipa ya neva ilajitokeza pembezoni mwa macho. Wanasayansi wa leo pia wameshindwa kuthibitisha usahihi wa njia hii, ijapokuwa ni kweli mabadiliko yanaweza kutokea kwenye macho ila si kwa kipindi cha mwanzo.



5.Njia uliyojulikana kama Piss Prophets
Njia hii ilitumiaka miaka ya 1600, matabibu hawa walikuwa wakipima ujauzito kwa kutumia kuangalia mkojo. Hawa waliamini kuwa mkojo wa mjamzito unakuwa ni msafi naani hauna uchafu, una rangi ya limao bivu lililopauka lakini unakuwa na ukungu kwa mbali juu yake. Pia matabibu hawa hawakuishia hapa walikuwa wakiangalia uwepo wa maradhi engine kwa kuangalia mkojo. Wanasayansi wa leo pia wameshindwa kuthibitisha usahihi wa njia hii.



6.Kwa kutumia riboni:
Njia hii ilikuwa na mzunguruko kidogo, nikuwa mwanamke anapojihisi ni mjamzito anakwenda kwa tabibu. Tabibu atamwambia akojoe kwenye beseni, kisha tabibu atachukuwa riboni na kuitia kwenye beseni lenye mkojo. Baada ya muda ataitoa na kuikausha, kisha ataichoma mbele karibu na mwanamke. Kama harufu ya riboni itamfanya mwanamke ahisi kichefuchefu basi atakuwa ana ujauzito. Wanasayansi waleo pia hawakuweza kuthibitisha njia hii.



7.Kwa kutimia Sungura ama wanyama wadogo wadogo kama panya.
Njia hii iligunduliwa miaka ya 1900 na matabibu waliojulikana kwa majina ya Bernhard Zondek na Selmar Aschheim. Hawa miaka ya 1940 waliamini kuwa mkojo wa mjamzito ukiingizwa kwenye mwili wa vijinyama vidogo basi ovari zao huwa kubwa. Baadaye jaribio hili lilijikita sana kwa kutumia sungura. Wanasayansi wa leo walionyesha kuwa njia hii ilikuwa na ukweli kiasi japo sio njia nzuri maana ilihitajika kumuuwa sungura ili kuchunguza kama ovari zimekuwa kubwa.



8.Kwa kutumia chura.
Njia hii ilianza kutumika Afrika ya Kusini. Wao walikuwa wakutumia chura wa kike. Waliamini kuwa endapo chura wa kieke akichomwa sindano yenye mkojo wa mwanamke mjamzito, basi chura huyo atataga mayai ndani ya masaa 12.



Njia nyingine:
9.Kuangalia mwendo, yaani jinsi anavyotembea mjamzito ni tofauti na mwanamke asiye mjamzito.
10.Kwa kuaangalia ongezeko la mapigo ya moyo. Kama mapigo ya moyo yameongezeka basi mwanamke ana ujauzito.



Njia zilizotajwa hapo juu zilikuwa zukitumika katika nyakati zake na zilionekana kusaidia kwa wakati ule. Ni kweli njia hizo zina madhaifu makubwa lakini si kila wakati zilikuwa zikikosea. Wakati mwingine zilikuwa zikipatia, ni kwa sababu mwanamke alikuwa ni mjamzito kweli. Hata hivyo ilibidi pia kuangalia dalili nyingine za ujauziti ndipo tabubu alikuwa akitoa jibu.



Kama unahitaji kuuliza maswali Bofya hapa

Mwandhishi Tarehe 2018-08-01     Share On Facebook or Whatsapp Imesomwa mara 1601

Post zifazofanana:-

Chemsha bongo namba 25
26. Soma Zaidi...

Vyakula vizuri kwa vidonda vya tumbo
Hii ni orodha ya vyakula salama na vizuri kwa mgonjwa wa vidonda vya tumbo Soma Zaidi...

AMRI YA KUMFUATA MTUME (s.a.w9)
Amri ya Kumfuata Mtume (s. Soma Zaidi...

Kutuma sms ndefu
Jifunze matumizi ya simu yako na namna ya kutatua matatizo mbalimbali kwenye simu na kompyuta.. Soma Zaidi...

Kitabu Cha Hadithi ya kifo cha Damu
Kupata kitabu hiki download faili la PDF hapo chini na usome bila ya internet. Soma Zaidi...

Namna ya kuswali
2. Soma Zaidi...

Mafundisho yao kutoathiriwa na mazingira ya jamii zao
Takriban Mitume wote walitokea katika jamii zilizozama katika ujahili, lakini kamwe ujumbe wao haukuathiriwa na mitazamo ya ujahili kwa ujumla, walahawakuingizautamaduni wa kijahili katika dini ya Allah (s. Soma Zaidi...

quran na sayansi
2; mbegu ya uhai uliyo changanyikaUmbile la mwanadamu limepitia hatua nyingi sana kama tutakavyoendelea mbele kuonalakini ukiachilia mbali na hatua zote alizopitia mwanadamu wakati wa kuumbwa lakiniumbile la mwanadamu bado limebakia kuwa dhalili kama ALLA Soma Zaidi...

HADITHI YA KAKA WA NNE WA KINYOZI
Soma Zaidi...

Njia haramu za uchumi
Soma Zaidi...

HISTORIA YA NABII YUNUS
Soma Zaidi...

Upeo wa Elimu waliyokuwa nayo Mitume
Soma Zaidi...